Nani anastahili tuzo ya Nobel katika marais 6 tuliowahi kuwa nao Tanzania?

Umetufaa kwa viwango vilivyotukuka. Umepanua uelewa wetu, umeonyesha njia na namna ya kutanua mjadala. Ni kweli tuzo haijasitirika kwa wanasiasa pekee ila hao ndiyo wako kwenye global spotlight kwamba hadi sasa labda hatuna mwanasayansi aliyefanya ugunduzi wa kunyanyua nyusi za dunia.
 
always nyerere ni best, akifuatia na fulan simtaji ili kuondoa kelele za wale majamaa wa upande ule, na kuna vikundi vyakipuuzi hupenda kumbeza nyerer kuwa alifanya mambo ya hovyo ktk sakata la.......,

Hawa watu wanasahau kuwa nyerer alipambana sana kuhakikisha hii nchi inafika ilpofika leo, wakat huo mababa na mababu wa hawa walalamikaji, walikuwa bize maporini wakikimbizana nusu uchi na wanyamapori, sasa matoto yao leo hii yanajiona yamestaharabika wala hayana shukrani kwa wapigania uhuru, yanatusi na kushusha samani ya uhuru na amani hii.
 
Kuna mtazamo (perspective) wa warasimu kwamba riba na marejesho vilitumika kupanua wigo wa kudahili idadi kubwa ya wanafunzi wapya ili wasiendelee kubaki nyumbani. Nini maoni yako zaidi Bemendazole.
 
Kuna mtazamo (perspective) wa warasimu kwamba riba na marejesho vilitumika kupanua wigo wa kudahili idadi kubwa ya wanafunzi wapya ili wasiendelee kubaki nyumbani. Nini maoni yako zaidi Bemendazole.
Sio sawa kukunyang'anya ela yako ili kusomesha mtoto wa mwingine. Kwa nini nguvu yako ilee mtoto wa mwingine? Je wa kwako akikosa mkopo atasomeshwa na nani?
 
Ali Hassan Mwinyi Baba wa demokrasia. Aliondoa mifumo ya kijamaa na kuweka hii ya kisasa..
Na watu hawafahamu, huyu Mzee Mwinyi ni muasisi wa sera NYINGI za hayati Ben, ikiwemo na hiyo TRA. Huyu Mzee alkua mvumilivu lkn mwenye confidence, ssie na papara mwenye kupenda democracy. Huyu NDO aliruhusu vyama vingi, alipokea nchi ikiwa uchumi wake haujatengamaa kutokana na vita. Mambo mengi SANA tunayotumia Hadi Sasa ni kwasababu yake. Mwinyi ni Mwinyi, mwanaume na nusu.
 
Agufuli, kaendeleza nchi kimiundombinu kwa mda mchache sana
 
Kamaradi Ngaiwoye,

Ni Mzee Ruksa huyu ndiyo amemsifia JPM mara kadhaa bila kificho kwamba kafanya mengi mazuri kwa muda mfupi kiasi ambacho akamtamania urefu wa muda wa kukaa ofisini baada ya 2025! Unadhani Mzee Ruksa alikuwa sahihi? Tusaidie Kamaradi wetu.
 
Hakuna hata mmoja...kwan wote wanaamin CCM KWANZA WATANZANIA BAADAYE
 
Wakipata watakuwa wanastaili ila sababu hawaja pata kwa hiyo hawastaili
 

Hata kupendekezwa hawaja pendekezwa bahati mbaya hakuna anaye stahili
 
Mkuu samahani,naomba kuuliza..Hivi wewe unahisi tukipigana na Uganda leo hii 2021 kuna uwezekano kiasi gani wa kuwachapa tena?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama ingehusisha na Mawaziri Wakuu, basi Salim Ahmed Salim angekuwa kashaichukua
Katika mawaziri wakuu waliongoza Tanzania kipindi kifui basi Dr Salim ndiye namba moja kwahiyo uwezekano ni mdogo mno tukija kwa cheo alichokuwa nacho AU pale basi wamarekani wasingekubali maana kwa zile figisu alizofanyiwa na wamarekani baada ya kutaka kugombea ukatibu mkuu wa UN hakika hazikuwa ndogo na pengine angelikua mwafrika wa kwanza kushika wadhifa wa ukatibu mkuu wa UN.
 
Mkuu samahani,naomba kuuliza..Hivi wewe unahisi tukipigana na Uganda leo hii 2021 kuna uwezekano kiasi gani wa kuwachapa tena?

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahahahaaa swali la mtego hilo mkuu.

Kwa mujibu wa wavuti wa Global Firepower, UG ni 89th,out of 140, ours is ranked 112th. Jiangalizie mwenyewe kwenye link nyingine hapo chini.

Top 20 Most Powerful Militaries In Africa 2016

NB. Nadhani hao wengine wamescore nafasi nzuri kwasababu nchi zao ziko vitani kwa muda mrefu na hivyo wana mafunzo mengi na vifaa bora vingi.
Ila nadhani mara nyingi taarifa hizi zina usiri mkubwa kiasi kwamba wanaokusanya takwimu kwa ajili ya kulinganisha hawapewi taarifa za kutosha.
 
Punguza font mkuu, nimeshindwa kusoma
 
Wakati wa Nyerere inaonekana tulikuwa pia na intelijensia nzuri sana sisi Tanzania..

Do you think tunao watu sahihi kwenye idara zetu za ujasusu kwa kuangalia mambo yanavyoenda humu nchini na tunavyoshirikiana na nchi za jirani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…