Nani anatakiwa abadilike mimi au mke wangu?

  • Thread starter Thread starter PI
  • Start date Start date
Aaa wapi, unatuchezea akili weye. Hiyo si ndio post ya kwanza ya IP? Hahahaha1 Timekustukia.
Sasa Mkuu chrispin umemstukia nani huyo IP au nani? Si umeona hapo post yake ndo ya kwanza baada ya kuambiwa na mumewe asome maoni ya wadau ndo akamua kujiunga atoe na yeye upande wa shilingi? au hujamuelewa?
 
Hapo wa kubadilika ni mama. Lazima aende na wakati bana. Kama hawezi swahiba tafuta anayeendana na hali halisi ujivinjari naye. Asikuletee za kuleta.
Binamu kwa shortcuts sikuwezi!

Kabla ya kumshauri mleta hoja pls hebu niambie ilikuwaje miaka yote wakati mnakatiza makontinents na kupanda ngazi moja hadi nyingine..ina maana mlikuwa hampo wote hadi ukamwacha kiasi hicho? Ninasema hivi kutokana na uzoefu katika mambo haya.Watu wengi huanza from humble begginings wakiebadilika kuanzia umri hadi status... na katika mchakato huo wa mabadiliko wote wawili mnapitia transformation - kuanzia kujifunza lugha mpya, kujifunza ettiquete na ustaarabu wa sehemu mbalimbali, kuanzia uvaaji, makulaji, mikao, mapose n.k. Ina maana wewe ulibadilika ghafla bin vuuu yeye akiwa wapi mpaka sasa unashtuka kuwa anahitaji kubadilika?
 

 
Sasa Mkuu chrispin umemstukia nani huyo IP au nani? Si umeona hapo post yake ndo ya kwanza baada ya kuambiwa na mumewe asome maoni ya wadau ndo akamua kujiunga atoe na yeye upande wa shilingi? au hujamuelewa?

Ukweli ni kwamba, hamna cha mke aliyeandika hapa. Aliyeandika hii ni huyohuyo aliyeandika ile, anataka kutupima akili zetu. Stuka kimey.
 
Wadau,
Hili ni tatizo lililopo kweli lakini si kama tunapigana. Nimeona nimwambie mke wangu aweze kusoma maoni ya wengine pia. hata registration hakuwa anaweza nimemsaidia. Bado naomba ushauri maana tunaongelea hali halisi na wala hakuna chochote cha kutunga wala mchezo. Hakuna sababu ya mchezo maana hakuna faida kwa hilo. Zaidi ingetupotezea wakati sisi kwa kuandika mambo yote haya.
Ukweli kwa kujibu hoja ya MAMSAP naomba arejee ukweli kwamba ni siku 4 kwa sababu leo ni JUMATANO na tuliongea JUMAPILI , therefore we have J2, J3, J4, na J5 .
Hoja ya kuwa pamoja ni kweli wakati nasoma M Sc. yeye alikuwa TZ. Na baada ya hapo tumekuwa wote tu na nimejaribu kuelimisha mengi ambayo alishindwa nilitupilia mbali.
1) Kuhusu kutembea: kuna ubaya gani kusema mwanamke fulani anatembea kwa kujiamini? hili wajamani kwa mamsap ni kosa la jinai. haya niliacha.
2) TV show, ukweli sijasema mtu apende show fulani. lakini, nilikuwa nina watch shows ninazopenda na kuzitetea jinsi zinavyo pendeza hilo kosa! Ikabidi niwe na TV bed room. Wakati nataka ku_watch Trumph the celebrity, yeye angalie anachopenda. Nilikubali.
3) Kunenepa: unene una madhara yake wengi wanajua. Sasa kosa langu ni nini?
Tukumbuke kuwa elimu ya ndoa haifundishwi shule wala kusoma si lazima kuwa na elimu ya uhusiano wa ndoa.
Mwisho naomba kwa vile amesema yake na mimi nimesema, tuwaachie wadau wachangie ili haki itendeke.
 
hapo juu kama ni kweli mtu na mumewe shewea shuwea khaaa.....
 


eeeeh pole sana ndugu yangu mie nashindwa kuelewa kwa nini akina mama tunakuwa hivi jamani ...? nashindwa nitoe ushauri gani hapa
 
Mbona katika thread sijaona jamaa akisema mke wake anajihusisha na magroup ya umbea? au hizi pre judgement zako unaziweka vp? Mbona nyie mnao jiita classic ndo mnaongea sana umbea huko kwenye masalooni yenu ya classic? au umbea wenu tofauti?
hahhahahahhahahaaaaaa tena hujawahi ona , labda tofauti yao ni kwamba wambea wa classic saloon wanapiga umbea wa 'Bossip' but celebrities wa kibongo, miss nani kafanya nini, marketing manager wa kampuni flani anatoka na demu flani, beyonce inasemekana anamcheat 'camel' na jamaa gani.
lakini all in all wote wambea.
ila la muhimu ni kwamba huyo kaka hajasema kama mkewe ana magroup ya umbeya .
 
Kwani umeshindwa hata kutafuta spare tyre mkuu mbona shazi sana.
 
Mkuu umeamua kuhamia tukuyu kiujumla?

Hahahaha Tukuyu nilisha chapa mwendo mbona muda naonja radha tofauti tofauti nitakuja na majumuisho mkuu then nahamia kanda ya ziwa nako.
 
Hahahaha Tukuyu nilisha chapa mwendo mbona muda naonja radha tofauti tofauti nitakuja na majumuisho mkuu then nahamia kanda ya ziwa nako.

Lol! Mkuu utapata ladha za pande zote. Ulinibania, hukunipa contacts za looser flani.
 
Hahahaha yule aliwahi mpwao Yo Yo nikaamua kubana.

Siku nyingine unifikirie veterani mwenzako bana. Haifai kulazana njaa wakati tuna apetaiti ya aina moja.
 
Mbadilishe kimya kimya, mara leo umemnunulia kimini,kesho kitop, keshokutwa suruali mara kikaptula huku ile mikanga unaificha au siyo mukubwa......
 
Nimepitia maisha ya aina mbalimbali nchi mbalimbali magharibi na mashariki. Mwisho nimefika mahali ambapo ninaheshimika. Nimejaribu pia mke wangu abadili mtazamo wake kwa maisha ya leo. Bahati mbaya hataki kubadili mtazamo wako.

Hapo kwenye nchi mbali mbali ulikuwa naye huko???

Jibu:
tatizo, alipoondoka kwenda US alikaa huko miaka 3 aliporudi ndo akaanza 1) mimi mnene nipungue 2) Nitembee kama so and so. 3) Nipende show fulani fulani TV, zote



Na hapo juu man mmh kweli JF kiboko. Yaani wewe kwenda US kimasomo unarudi after 3yrs unaanza kumkandia mamsapu eti abadilike kwa kuwa umekuja na u know u knows zako. Afadhali huyu IP amejitokeza kwani wewe huku-display all material facts kama hii kuwa ulikuwa US for 3 yrs na ukawa umemwacha huku and then unakuja simply wewe umeona akina XXL, XL etc huko US nawe unataka wife achange.



Another point ambayo namkubali huyu mamsapu.

Mume wangu nakupenda tu hivyo ulivyo. Nitakusaidia ubadilike.
Note: I was not an idler that's why I am not a begger!
IP

Very Big point though!


Kweli JF kiboko inaweza imarisha NDOA za watu!!
 
eeeeh pole sana ndugu yangu mie nashindwa kuelewa kwa nini akina mama tunakuwa hivi jamani ...? nashindwa nitoe ushauri gani hapa

asante dada...
natamani na mimi nimweke hapaJF apate shule kidogo...
na nitafanya hivyo...
Thanks
 
Wote mnatakiwa kubadilika, wewe kama mwanaume unatakiwa kumpeleka mkeo akafanye shopping, mchukue mwende wote na umuonyeshe mavazi gani wewe unapendelea yeye avae. Umweleweshe kwa upendo kwamba mke wangu napenda uvae hivi uwende na wakati, kama mwanamke anayetaka ndoa yake idumu atabadilika tu.

Vile vile kwa upande wa mwanamke anaweza kabisa kubadilika, hata kama ana miaka 50, mie nimeona wamama wana miaka zaidi ya 50 na wanachange kabisa, wanaenda kutokana na wakati ili kulinda ndoa zao. Wapo wanawake wanafanya hadi style za kisasa kwa wanaume zao ili kulinda ndoa zao. Wewe mama IP kuwa makini na mumeo, ukifanya mchezo mumeo atachukuliwa na wadada wanaoenda na wakati.
Tena shukuru mumeo anakwambia mapungufu yako, wapi ubadilike. kuna baadhi ya wanaume hata hawasemi kwamba ubadilike, hao wanatoka kimya kimya tu nje.
 
Ukweli ni kwamba, hamna cha mke aliyeandika hapa. Aliyeandika hii ni huyohuyo aliyeandika ile, anataka kutupima akili zetu. Stuka kimey.

True Chriss,anataka kucheza na akili zetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…