Nani anatakiwa kulipa mahari? Aneyeoa au mzazi wake?

Nani anatakiwa kulipa mahari? Aneyeoa au mzazi wake?

Mwachiluwi

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2022
Posts
25,258
Reaction score
48,589
Hellow,

Hivi karibuni kumezuka mzozo mkubwa sana katika familia, chanzo kaka yetu anataka kuoa lakini mahari anasema mzazi wetu ndio atoe, kisa huyo mchumba wake amemuambia kuwa mahari yako kisheria anatakiwa atoe mzazi wako na sio wewe.

Na yeye bila kujiongeza kashupalia kweli kuwa yeye asitoe mahari yaani tumtolee sisi hii imekaaje kwani mzazi ndio anaenda kukaa na huyo mke? Naomba kujua ukweli wa hili jambo limekaaje

Mimi nipo upande wa yeye kuitafuta hela alipe hiyo mahari na sio kumtegemea mzazi tena au sisi
 
Kama ingekua 50/50 kushirikiana kazi za nyumbani wanaume msingekubali kutoa mahari. Ila sio umchukue binti wa watu halafu ukamgeuze punda bure bure
Hivi hawa watu wa haki za Wanawake na women empowerment hawaoni kuwa kulipa mahari kwa mwanamke ni dhana ya kitumwa, yaan ni kama kununua barmaid tofauti ni muda wa kuwa naye tu.

au hili hawalioni??
 
Kama unataka kuoa hakikisha unauwezo wa kumrisha mwanamke, kumlinda, una nguvu za kiume za kumtosheleza, mwisho mali ni makubariano ya nyinyi wawili iwe bure au pesa, wazazi hawahusiki
 
Kama ingekua 50/50 kushirikiana kazi za nyumbani wanaume msingekubali kutoa mahari. Ila sio umchukue binti wa watu halafu ukamgeuze punda bure bure

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] dah na niny mgetoa mahari siyo?
 
Kuna basdhi ya makabila hata sisi wachaga ni matusi kwa mzazi ukatoa mahari wewe. Nina rafiki yangu msukuma alilipa maharishi baba yake aliwaka sana. Kifupi ilikuwa mtiti kuwa kamdharau na kumtusi vibaya mno kuwa hawezi lipa mahari yeye wakati bado yupo hai. Angeshindwa kulipa basi ingemlazimu amruhusu atoe yeye mtoto. .

Wakati naoa niliona mambo yasiwe mengi nikamshirikisha Mzee wangu kuwa nataka oa na utaratibu wa mahari tunafanyaje. Nakumbuka alinipatia hela niongezee kwenye mahari. Ila wale wamasai waliniweza nikalipa million 4 cash sidaiwi. Niko huru kuwala kimasihara 😀
 
Kuna sura mbili katika hili.
Mimi si mjuzi ila nitasema kile ninachoamini ndicho sahihi na ambacho ninakijua.

Kwenye Uislama,
Muongozo ni kuwa Mahali inatamkwa na anaetarajiwa kuolewa
(Yaani binti) kwamba mie nataka hivi, ama hivi na hivi.
Kumbuka inaweza kuwa katika Pesa ama Kitu/Vitu.
Sasa kama mnafahamiana vyema bila shaka atakuwa anajua kipato ama uwezo wako wewe mwanaume hivyo basi upo uwezekano wa kutamka kile ambacho anajua dhahiri kuwa wewe mwanamme unao uwezo wa kukipata pasi mahangaiko sababu mnaoana kwa mapenzi si kwa Mali.

Hatahivyo, Mahari bora zaidi katika Uislam, ni ile ambayo haimkomoi mtoaji na inayoshauriwa zaidi inaweza kuwa hiyohiyo au hiyo pamoja na vingine lakini ikimpendeza mpewaji basi ikiwa mojawapo ya nyenzo za kuendeleza Imani ikiwemo Kitabu kitukufu cha 'Al Qur'an' Karim (Mashafu) hata hiyo pekeyake inatosha sana kuwa Mahali kwa binti na 'ikaswih'.

Lakini sasa yanapokuja mambo mengine ya Kidunia yasiyohusiana na alivyoagiza Mwenyezimungu,
Zinaingia Tamaduni, Mila, Desturi,Mazoea na longolongo mia kidogo zikiwemo zenye muelekeo wa kishetanishetani.

NANI ANAPASWA KUILIPA MAHALI?
Narudia tena mimi si mjuzi sana wa mambo haya ila,
Nazungumza uzoefu na Mazoea;
Ni kuwa Mahali analipiwa kijana na mzazi wake au Mlezi (Kwa Ndoa ya kwanza)

Ukitaka Kuoa tena (Mke wa pili) Hicho ni Kiranga,-makalio yako unatakiwa ulipe mwenyewe hiyo mahari.

SHIDA KUBWA:
Familia zetu watu maisha yakiwapiga, mmefulia, choka mbaya kila mmoja atakwepa na atatokwa na Povu kujitetea na kusema KUTOA MAHALI ni jukumu la mwingine ilimradi tu zigo lisimdondokee yeye.

Ila, nadhani, Inafaharisha na kufariji kwako wewe Mzazi kuona kuwa Umetoa Mahari wewe kwa ajili ya mwanao kupata Jiko, Mawazo yangu tu.

Sijui nimeeleweka?
 
Kuna basdhi ya makabila hata sisi wachaga ni matusi kwa mzazi ukatoa mahari wewe. Nina rafiki yangu msukuma alilipa maharishi baba yake aliwaka sana. Kifupi ilikuwa mtiti kuwa kamdharau na kumtusi vibaya mno kuwa hawezi lipa mahari yeye wakati bado yupo hai. Angeshindwa kulipa basi ingemlazimu amruhusu atoe yeye mtoto. .

Wakati naoa niliona mambo yasiwe mengi nikamshirikisha Mzee wangu kuwa nataka oa na utaratibu wa mahari tunafanyaje. Nakumbuka alinipatia hela niongezee kwenye mahari. Ila wale wamasai waliniweza nikalipa million 4 cash sidaiwi. Niko huru kuwala kimasihara [emoji3]

Nimekupata sana
 
Kwasisi tulioshilika mapokeo ya kiyahudi na kimila MZAZI anawajibika kumuoza mwanawe huku MTOTO akiwajibika kumzika mzazi wqke.

Ndio kusema baba hapaswi kufa bila kumtolea mahari mtoto wake huku mtoto anapaswa kuhakikisha hafi mpaka amzike babaake.
 
Nakataa uho ujinga
 
Back
Top Bottom