Kuna sura mbili katika hili.
Mimi si mjuzi ila nitasema kile ninachoamini ndicho sahihi na ambacho ninakijua.
Kwenye Uislama,
Muongozo ni kuwa Mahali inatamkwa na anaetarajiwa kuolewa
(Yaani binti) kwamba mie nataka hivi, ama hivi na hivi.
Kumbuka inaweza kuwa katika Pesa ama Kitu/Vitu.
Sasa kama mnafahamiana vyema bila shaka atakuwa anajua kipato ama uwezo wako wewe mwanaume hivyo basi upo uwezekano wa kutamka kile ambacho anajua dhahiri kuwa wewe mwanamme unao uwezo wa kukipata pasi mahangaiko sababu mnaoana kwa mapenzi si kwa Mali.
Hatahivyo, Mahari bora zaidi katika Uislam, ni ile ambayo haimkomoi mtoaji na inayoshauriwa zaidi inaweza kuwa hiyohiyo au hiyo pamoja na vingine lakini ikimpendeza mpewaji basi ikiwa mojawapo ya nyenzo za kuendeleza Imani ikiwemo Kitabu kitukufu cha 'Al Qur'an' Karim (Mashafu) hata hiyo pekeyake inatosha sana kuwa Mahali kwa binti na 'ikaswih'.
Lakini sasa yanapokuja mambo mengine ya Kidunia yasiyohusiana na alivyoagiza Mwenyezimungu,
Zinaingia Tamaduni, Mila, Desturi,Mazoea na longolongo mia kidogo zikiwemo zenye muelekeo wa kishetanishetani.
NANI ANAPASWA KUILIPA MAHALI?
Narudia tena mimi si mjuzi sana wa mambo haya ila,
Nazungumza uzoefu na Mazoea;
Ni kuwa Mahali analipiwa kijana na mzazi wake au Mlezi (Kwa Ndoa ya kwanza)
Ukitaka Kuoa tena (Mke wa pili) Hicho ni Kiranga,-makalio yako unatakiwa ulipe mwenyewe hiyo mahari.
SHIDA KUBWA:
Familia zetu watu maisha yakiwapiga, mmefulia, choka mbaya kila mmoja atakwepa na atatokwa na Povu kujitetea na kusema KUTOA MAHALI ni jukumu la mwingine ilimradi tu zigo lisimdondokee yeye.
Ila, nadhani, Inafaharisha na kufariji kwako wewe Mzazi kuona kuwa Umetoa Mahari wewe kwa ajili ya mwanao kupata Jiko, Mawazo yangu tu.
Sijui nimeeleweka?