Upekuzi101
JF-Expert Member
- Aug 28, 2020
- 478
- 1,025
Nani amtoe Mwigulu sasa🤔Hapo kwa Charles Kimei hapana.
Seriously sijaona... Yaani ni sawa na gagulo kuukuu lililochoka unatoa kiraka kibovu unapachika kibovu tenaLet's assume kuwa SSH ana nia ya dhati ya kuiletea maendeleo Tanzania na anataka kumantain speed ya utekelezaji wa miradi kama kipindi cha mwendazake ila anakwamishwa na wasaidizi wake ikiwemo mawaziri, ukizingatia mama ni mtu wa madaftari mambo ya field hata hajui. Unadhani waziri gani anapaswa kuachia ngazi na nani kuchukua nafasi yake. Mimi nikianzia na:
1. January Makamba out - Kalemani in
2. Mwigulu Nchemba out- Charles Kimei in
Ongeza list yako na wewe.....
Nadhani wapo wachumi wazuri katika Baraza la Mawaziri la sasa atafutwe mmoja wao.Nani amtoe Mwigulu sasa🤔
Mama anasubiri kuletewa majina ya watu na waletaji ndo wale wale. Labda kuwe na mfumo kidogo utaowahusisha watu wasiofungamana na upande wowote kisiasa au kimimaslahi kupendekeza watu kwa kuzingatia ufanisi wao kule walipo, bila kuangalia PhD ambazo tumezingundua ni nonsenseNadhani wapo wachumi wazuri katika Baraza la Mawaziri la sasa atafutwe mmoja wao.
Ikishindikana waende ndani ya Bunge ikiwa ngumu anyofoe nje ya mfumo kabisa.
Lakini yote hii ni KAMAIssue siyo nani awe replaced na nani..
Issue ni MFUMO WETU WA AJIRA HIZI NA UTUMISHI WA UMMAH KWA UJUMLA UNA MAPUNGUFU.... Nadhani kwanza tungeanza na kufanya yafuatayo:
1. Mawazi wawe wanapendekezwa na RAIS kuwa approved na bunge kwa kuhojiwa na kamati husika LIVE na kuidhinishwa na MKUTANO MKUU WA BUNGE.
2. Kamati husika za BUNGE/Bunge liwe linapata nafasi ya kuwahoji mawaziri kwa maswali ya papo kwa papo ili kuwafanya kuwa WATENDAJI na wafuatiliaji wa majukumu yao na BUNGE LIWE NA NAFASI YA KUWAWAJIBISHA.
3. Mawaziri wasiwe wabunge wa kuchaguliwa ili kuwafanya kujikita zaidi kwenye majukumu yao na sii kuanza kuwaza MAJIMBO yao kitu kinachosababisha kukosa ufanisi katika majukumu yao.
4. Akithibitika Waziri ame-underperform anatenguliwa na mshahara unakoma na kiinua mgongo kitategemea alichochangia na muda wa utumishi wake[yaani inaunganishwa na michango MINGINE ya kabla au baada]
5. Kuwe na Utamaduni wa mawaziri kila baada ya miezi 6 kufanya press conference na kutoa taarifa ya utekelezaji wa wizara zao na kujibu maswali ya waandishi wa HABARI ili kujua utendaji wao na wawe rated kulingana na alivyoperform.