Nani anatoa vibali vya kupiga picha kwenye lecture

Status
Not open for further replies.

Mphamvu

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2011
Posts
10,702
Reaction score
3,319
Naona huu utaratibu umekuwa sugu hapa State University, leo Prof. Kihore anafanya muhadhara hapa Yombo 5, amekuja na mzungu wake, anafanya video shooting. Napata mkanganyiko kidogo, Profesa hajaomba ridhaa yetu ili apige picha., na mchakato unaendelea pasi na wasi.
Naombeni mwongozo wenu wadau...
 
State University ya wapi, na huyo Profesa Kihore ni nani. Hata hivyo angalia tena makaratasi uliyosaini wakati unaingia hao State University. Vyuo vingine vina utaratibu wa kuchukua video wakati waalimu wanafundisha ilivideo hizo zitumike katika kutuoa mafunzoa kwa waalimu kuboresha mbinu zao za kufundisha.
 

State University ya Tanganyika i.e UDSM. Prof Kihore ni mwalimu wa Kiswahili hapa...
Huo utaratibu sidhani kama upo katika chuo hiki, ni mgeni kabisa. And much painful ni kuwa cameraman alikuwa mzungu...
 
Pamoja na kwamba namheshimu sana Prof. Kihore, nina mashaka sana na wazungu maana wenzetu hao mra nyingi hawana jema utashangaa mzungu anarudi kwao na hizo picha zinatumika kukusanya michango kuisaidia UDSM alaisifike kama ilivyokua inafanyika huko Dafur, Sudan. Hivyo basi siku nyingine ukiona jambo kama hilo ukiwa kama mzalendo halisi mfuate aliyekuja naye umwambie kwa utaratibu tu kuwa anahitaji ridhaa yenu kwanza na pili kama huyo bwana yuko mwenyewe haraka piga simu au ukaripoti kwa auxiliary police maana hiyo hairuhusiwi bila kibali kutoka utawala.
 
Mambo mengine bana....hata kuchangia inakuwa ngumu!
 

natamani ningehoji, ila unaufahamu ustaarabu wa kuigiza hapa UD, ukihoji wewe ndo unaonekana hauko civilized.
 
Kupiga picha Africa ni Kitu cha ajabu sana, kwanini we unaogopa kupigwa picha. unatatizo gani, America au Ulaya watu wanapiga picha popote
 
Kupiga picha Africa ni Kitu cha ajabu sana, kwanini we unaogopa kupigwa picha. unatatizo gani, America au Ulaya watu wanapiga picha popote

sio bila ridhaa ya mhusika. Hata kwenye matukio makubwa waandishi huvaa vitambulisho vilivyoandikwa 'PRESS' na vijambakoti maalum, rahisi kuwatambua. Ati picha kokote?
 
Kwanini hamkuhoji hapo hapo?. Yeye kuw Prof hakukuzuii wewe kuuliza yale unayohisi ni haki yako kuyajua.
 
Kwanini hamkuhoji hapo hapo?. Yeye kuw Prof hakukuzuii wewe kuuliza yale unayohisi ni haki yako kuyajua.

Watu walifanya ka-protest kadogo, ila kombe likafunikwa mwanaharamu akapita!
 

n thats whats up...
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…