Nani anavuruga kitanda changu nikiwa nimelala?

SAYVILLE

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2010
Posts
7,895
Reaction score
12,975
Leo nakuja na mada fikirishi.

Nikiwa nalala peke yangu, huwa nahakikisha shuka limechomekwa vizuri kitandani kabla sijalala ila nikija kuamka nakutaga kitanda kimevurugika, shuka nililotandika limefolonyolewa kabisa na wakati mwingine nalikuta sakafuni.

Kuna mara nasema ngoja nilale kwenye kochi sebuleni nione nini kitatokea, nakuta tena shuka lote limechomolewa.

Nikilala na shemeji yenu hayo wala hayatokei.

Nini mnadhani huwa kinatokea enyi wana wa Adamu maana dunia hii ina siri nyingi.
 
Zile ndoto zako kuwa unakimbizwa na mbwa unadhani zinakuacha salama..!

Laiti unavyolaza ubavu wako ukiwa umeelekea kaskazini ingekuwa unavyo amka unakuwa kwenye hali ile ile basi hili swali lingekuwa na mantiki..

Kuhusu ukilala na huyo mwenzako mbona inakuwa tofauti hii kwa sababu unabanwa nafasi ya kujigalagaza kama ukiwa peke yako
 
Cha ajabu huwa sina ndoto mbaya sijui za kukimbizwa na fisi
 
Huyo demu ni mwanga!, itakuwa Huwa anakuja kimazingara mnapigana mikito....pasipo wewe kujua
Dah kuna mambo yake huwa yananifikirisha sana. Anaweza kupiga ma perfume chumbani mida ya usiku utadhani anatoka halafu huyoo anaenda kulala.
 

Labda ni mwenye nyumba[emoji849][emoji849][emoji849]
 
Ni shuka tu zinatolewa au na nguo zinachojolewa ?kuwa muwazi kijana usaidiwe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…