Nani anawalinda waliovamia na kupora Meku’s bar?

Nani anawalinda waliovamia na kupora Meku’s bar?

Joined
Jun 25, 2022
Posts
12
Reaction score
8
APRI 29 mwaka 2019 tukio kubwa na aina yake lilitokea mjini moshi baada yakundi kubwa la watu wakiwa na silaha za moto kuvamia na kupora mali kwenye mgahawa maarufu wa Meku’s Bristol Bar and Restaurant .

Wavamizi hawa ambao walikuwa na kila aina ua jeuri baada ya uvamizi huo waliondoka na mali za malioni ya fedha za kwenda kuificha kusikojulikana na hakuna hatua yoyote ilioyochukuliwa dhidi yao na mamlaka za serikali.

Peter Kaale aliyekuwa akiendesha mgahawa huo pamoja na kituo cha mafuta cha Oryx alijikuta akiwa mkiwa asiwe na usaidizi wowote na hivyo kumwachia mungu ashughulike na wabaya wake.

Kaale ambaye ni kijana mwenye taaluma ya uhandisi wa ndege na aliyeishi nchini Marekani kwa miaka mingi,aliamua kurudi nyumbani kufnaya uwekezaji wa migahawa akiamini anachokifanya ni kwa manufaa yaker na taifa kwa ujumla lakini haikuwa hivyo.

Kijana huyo amehangaika kwa muda mrefu akipigania haki yake na juhudi hizo zikazaa matunda hivo karibu na kuziamsha mamlaka za uchuguzi kuingia kazini na kuanza kuwasaka waharifu hao.

Taarifa kutoka ndani ya jeshi la polisi zinadai kuwa tayari watu kadhaa wamekamatwa wakihusishwa na tukio hilo akiwamo mfnayabiashara August matemu maarufu wa jina la Makele mkazi wa Soweto mjini moshi.

Habari zinadai kuwa polisi baada ya kumtia nguvuni Makele na kufanya upekuzi nyumbani wake wamefanikiwa kukamata mali za malimioni ya shilingi zinazodaiwa kuporwa kwenye tukio hilo ambako baadhi ya mali hizo amekuwa akizitumia kama mali yake halali.

Taarifa za kukamatwa makelele na watu wengine kutoka kampuni ya Oryx zinadhibitishwa na kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro (ACP),Simon Marwa Maigwa alipozungumza na wanahabari hivi karibuni mjini moshi.

Kamanda Maigwa akasema wavamizi hao hawakuwa nas uhalali wowote kisheria kufanya walichokidanya akimaanisha hawakuwa na nyaraka halali za kimahakama kuhalalisha uvamizi huo.

Uvamizi huo pamoja na uporaji ulifanywa isivyo halali kwa mujibu wa kamanda Maigwa na chimbuko lake ni mgogoro wa kibiashara kati ya Kampuni ya Oryx na Kampuni ya Community Petroleum ya Kaale iliyokuwa ikiendesha mgahawa huo pamoja na kituo hicho cha mafuta.

Ikumbukwe kuwa aliyekuwa mkuu wa mkoa huo ambaye kwa sasa ni marehemu ,Anna Mghwira wakati wa uhai wake aliwahi kutamka wazi kuwa uvamizi huo haukuwa halali kutokana na kutokuwepo nyaraka kutoka mahakamani za kuingia kwenye eneo hilo na kufnaya uharibifu huo.

Kwa upande wake Kaale ameweka wazi kuwa uvaqmizi huo ni uharifu kama ulivyo uharifu mwingine na anavitaka vyombo vya uchunguzi kufanya kazi yake kwa weledi ili waharifu hao waweze kufikishwa kwenye vyombo vya sheria na sheria ichukue mkondo wake.

Akasema kuwa wavamizi hao walidai kutoka makampuni ya ulinzi ya a Essama Security na kampuni moja ya udalali ya MEM ambako walipewa nguvu na mmoja wa wakurugenzi wa Kampuni ya Oryx Sophonie Babo huku wkaiwa na silaha za moto ambako waliwaamulu wafanyakzi wake kuondoka eneo hilo mara moja na pasipo kubeba kitu chochote.

Pamoja na uvamizi huo kutokuwa na Baraka za mahakama yapata miaka mitatu sasa vyombo vya uchunguzi vilikaa kimya kana kwamba hakuna jambo la kutisha hii ina maana walifumbia macho tukio hilo lililokuwa na kila aina ya uharifu uanoangukia kwenye jinai.



Kazi kwenu vyombo vya uchunguzi
 
Hivi matajiri kama mo,,huwa wanatumia mbinu gani mpaka maduka yao yenye kupokea mamilioni ya pesa kila siku hayavamiwi na majambazi
 
Hivi matajiri kama mo,,huwa wanatumia mbinu gani mpaka maduka yao yenye kupokea mamilioni ya pesa kila siku hayavamiwi na majambazi
Mo tajiri wa Nini mbona sijawahi kuona ata kiwanda chake
 
Hivi matajiri kama mo,,huwa wanatumia mbinu gani mpaka maduka yao yenye kupokea mamilioni ya pesa kila siku hayavamiwi na majambazi
Hawa wana viwanda Mkuu, hawapokei hela keshi, unalipia benki unaletewa mzigo mahali ulipo.
 
Peter Kaale mwenye taaluma ya uhandisi wa ndege na aliyeishi nchini Marekani una matatizo ya kuzidisha kuvuta bangi na ina kufanya kichaa Kumbe bangi zinakuendesha.

Ukumbuke dada yako anayeitwa Sia ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya kukopesha ya Heritage hapa Arusha aliuza nyumba ya familia ya Maiko huko kijenge Arusha, kwa kudhulumu kama ulivyodhulumiwa Wewe.

2. Pale ulianzisha night club na hotel na bar ndani ya shell eneo lenye mafuta ya Petrol tena lililopo mjini sheria ya EWURA uliwahi kuisoma?

3. Unapambana na Orxy Ili ikufidie ujinga uliokuwa unaundesha mjini ukisema ni mhandisi wa ndege na uliishi marekani?

4. Eneo hilo ulipangisha kwa Nani na kwa mkataba gani?

5. Ulikuwa na leseni ya night club kutoka moshi manispaa?

6. Eneo hilo lilikuwa hatarishi kwa biashara ulizozianxisha bila cibali Muhimu na kwa Usalama wa mji wa moshi ukizingatia Eneo hilo ni shell.

7. Weka nakala ya mikataba hapa Ili kumtidhisha RPC Kilimanjaro.

8. Pamoja na maelezo yako Elena mlikofikia mahakamani kwani dhell imefungwa huu ni mwaka wa 3 sasa achana na mambo ya kipolisi kwa hatua hii.
 
Peter amekuwa mhandisi wa ndege mabwaku. Pole kwa yaliyokukuta Petwa mpambanaji.
 
Back
Top Bottom