Nani anaweza nisaidia jinsi ya kuverify location skrill

Nani anaweza nisaidia jinsi ya kuverify location skrill

Ni matumaini yangu lengo lako sio kuitumia Upwork kama mbadala wa Payoneer iliyoathiriwa na balaa la WireCard manake sidhani kama Skrill imesharudishwa Upwork baada ya biashara kati yao kufa 3+ years ago. Lakini kama kwa shughuli nyingine, ofcoz Skrill wasumbufu sana ku-approve docs manake nakumbuka kwangu hadi ku-approve ilikuwa mbinde kweli kweli. Kama bado hujafanikiwa, nenda benki ukawasimamie wa-edit anwani yako ili include location.

Kwa mfano, kama address yako ni: Nafaka bin Kunde
P.O. Box 4587,
Dar es salaam
Unachotakiwa kufanya, ingia hapa ili upate postcode ya eneo lako. Sasa assume unaishi Magomeni, Mtaa wa Suna ambao postcode yako ni 14101, na nyumba unayoishi ni #12, waambie benki wa-edit anuani ili iwe kama ifuatavyo:-
Nafaka bin Kunde
Magomeni Suna Street, #12
P.O. Box 4587
DSM1401

Dar es salaam.

Kwa upande mwingine, utakavyojaza address kwenye Skrill Form,
Address #1 weka hiyo Magomeni Suna Street, #12
Address #2 Andika Box #

Ukiangalia hii screenshot ya Fomu ya CRDB(assuming banker wako ni CRDB), utaona format yake ipo tofauti lakini itabidi waandike hivyo kwenye sytem, at least kwa muda ili hatimae uweze kupata bank statement yenye hiyo address format hapo juu. Kwavile hiyo staili yao, na inawezekana hawafahamu address formats za wenzetu zipo vipi, itakuwa vizuri sana ukifika tawini cha kwanza chukua fomu ya kufungulia akaunti kisha ijaze hayo menzo niliyojaza hapa chini kisha address waliyoandika wao kwenye system, wai-edit na ifanane kama utakavyokuwa umeandika.

View attachment 1492920
Hizo sehemu nyingine unaweza kujaza lakini kama format ya statement za CRDB hazijabadilika, hizo sehemu hata ukijaza hazitatokea kwenye statement kwahiyo hazitaathiri format wanayoitaka Skrill. Seehemu nyingine unayoweza ku-edit address ni kwenye utility bills, lakini huko mziki wake unaweza kuwa mkubwa ukilinganisha na benki.
Dah mwaka 2020 Hadi leo madini haya yanatumika,,,,,
Kweli jamiiforum ni kisima cha maarifa
 
Hizi ndo faida halisi na za msingi kwingine tunachilimua tu kusogeza maisha ktk uzi wa kula masihara na kampeni za kataa ndoa..ila madini kama haya yataishi
 
Kwasababu najaribu kujiregister sim bank App inakataa naomba mbadala aisee
IMG_20230926_141922.jpg


Edit tu tengeneza kama hiyo print piga picha
 
Acha utani yani uwatumie receipt skrill unawajua unawasikia?postcode iko wapi,Address iko wapi??
Mkuu nishaverify skrill, payoneer mpaka paypal kwa njoa hiyo
Na hiyo nimeitumia last week kuverify akaunti ya dogo. Isome vizuri ina physical address
 
Back
Top Bottom