Nani anayekagua na kudhibiti ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG)?

Nani anayekagua na kudhibiti ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG)?

Duh, aisee, umegonga Ikulu, kwa kweli natamani hii iende hewani magazetini, kuna suala la Kikatiba hapa...nami nakupongeza sana sana
Mleta mada,

Ukiachilia mbali wanaokubeza kwa mada yako inabidi nikupongeze kwani umeleta kitu kikubwa kilichojificha kutokana na wengi wetu nikiwemo mimi tuko wavivu wa kusoma.

Katiba yetu iko wazi kabisa kuhusu CAG. Ibara ya 143 (i) inasema: {Kutakuwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali wa Jamhuri ya Muungano.}

Hapo hakuna matatizo. Jibu la swali lako linaweza kupatikana kwenye ibara ya 143(6) isemayo hivi: {Katika kutekeleza madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya (2), (3) na (4) ya ibara hii, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu hatalazimika kufuata amri au maagizo ya mtu mwingine yeyote au idara yoyote ya Serikali, lakini maelezo hayo ya ibara hii ndogo hayataizuia Mahakama nayo kutumia madaraka yake kwa ajili ya kuchunguza kama Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu ametekeleza madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii au sivyo.}

Hapo kwenye blue ni kwamba CAG si mwisho he/she is subject to court. Hivyo, CAG anaweza kushitakiwa mahakamani kama ameboronga.

Kikubwa kingine ambacho hukukileta lakini nakiona potential kwenye post yako ni kwenye ibara ya 143(4) isemayo hivi: { Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu atawasilisha kwa Rais kila taarifa atakayotoa kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya (2) ya ibara hii. Baada ya kupokea taarifa hiyo Rais atawaagiza watu anaohusika wawasilishe taarifa hiyo kwenye kikao cha kwanza cha Bunge kitakachofanyika baada ya Rais kupokea taarifa hiyo na itabidi iwasilishwe katika kikao hicho kabla ya kupita siku saba tangu siku ile kilipoanza kikao hicho. Iwapo Rais hatachukua hatua za kuwasilisha taarifa hiyo kwa Spika wa Bunge (au Naibu wa Spika ikiwa kiti cha Spika ki wazi wakati huo au ikiwa kwa sababu yoyote Spika hawezi Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania}

Hapa ndipo penye sakata ambalo inawezekana hujui lakini umelianzisha. Maana yake ni nini? Maana yake ni kwamba Rais ndiye anayepewa report ya madudu aliyogundua CAG wakati wa ukaguzi wake. Mara tu Rais anapoipata report hiyo anaipeleka kopi Bungeni.

Hivyo, mtiririko wa safari ya report ni kwamba inaanza kwa CAG, inaenda kwa Rais, kisha inaenda Bungeni. Hakuna mahala panapoonyesha kuwa Makamu wa Rais, au Waziri Mkuu au Waziri yoyote anapitia mlolongo wa kuipokea au kuigusa report ya CAG.

Kumbe, Waziri Mkuu na mawaziri wenzake, wanashtukia kuyasoma madudu yale report inaposomwa Bungeni. Hivyo, kwa utaratibu huu mtu pekee anayejua madudu ya report kabla haijaenda Bungeni ni Rais na CAG tu.

Kwa utaratibu huu, huwezi kusema Waziri Mkuu hakumshauri Rais kuhusu madudu yaliyomo kwenye report ya CAG wakati Waziri Mkuu hakupata nafasi ya kuiona kwani utaratibu uko wazi kabisa yeye anaijua report inaposomwa Bungeni.

Nakubali kwamba Pinda anaweza kuwa aliiona mapema, lakini kikatiba anapoiona Pinda ni kwamba ime-leak kwani hakutakiwa hadi aisikie ikisomwa Bungeni.

Hivyo, kikatiba huwezi kusema Pinda anapaswa kuwajibika kwa lolote lililotajwa na CAG. Eti hakumshauri Rais. Angemshauri vipi kwa jambo ambalo katiba yenyewe inasema kuwa hakutakiwa kulijua kabla report haijasomwa Bungeni na kuisikia kama tunavyoisikia sisi.

Hivyo, aliyeshindwa kuwawajibisha mawaziri kabla hata repirt haijaenda Bungeni ni Rais mwenye kikatiba na tuache ngonjera zingine za kisiasa ambazo hazitasaidia kuubadilisha ukweli huu wa kikatiba.

Someni ibara mbili za katiba yaani 143 na 144 ambapo ukweli ninaosema umeanikwa wazi hata primary school pupil anaweza kuusoma.

Namalizia tena, hongera mleta mada, na kama magazeti yatapitia thread hii, hii ni habari mpya ya kubadilisha upepa wa suala zima ambalo sasa eti linachukua sura ya kisiasa wakati ni suala la kikatiba.
 
nadhani ulikuwa unahitaji jibu hili-ofisi yake huwa inakaguliwa na PWC.

sasa mbona matokeo ya ukaguzi ktk ofisi yake hayatolewi publicaly, nahakika hata ktk ofisi yake madudu yapo ila hatupati fursa ya kuyajua
 
Mkuu Report ya CAG kwenda bungeni ni matakwa ya Kikatiba. Imekuwa ikienda bungeni miaka yote. Tatizo ni kwamba miaka ya nyuma ilikuwa report zinachelewa sana. Kwa mfano ungweza kukuta report ya 2007/2008 inasomwa bungeni mwaka 2012 kwa hiyo zikawa zinakosa impact. Ila miaka ya hivi karibuni ukaguzi umekuwa ukifanywa kwa wakati na repott kwenda bado ya motomoto kama hii ya juzi.

Imetulia na majibu yanajitosheleza vizuri.

Naomba kuongezea kuwa ripoti zile zilikuwa zinapitia ukiritimba mwingi ili ku-neutralize sumu yake. Sina shaka uwepo wa wapinzani makini ktk hizo Kamati za kudumu za bunge umesaidia sana mabadiliko ya uwasilishaji wa ripoti za CAG.
 
Kwa wenye kujua naombeni msaada wenu. Hivi sasa anakagua 'madudu' ya akina Mhando wa TANESCO.Yeye anakaguliwa na nani? Isije ikawa yeye ndiye fisadi nambari wani...
 
Kubenea tafadhali pitia huko utupatie data kwani huenda jamaa huyu anajikagua.
 
Kwa wenye kujua naombeni msaada wenu. Hivi sasa anakagua 'madudu' ya akina Mhando wa TANESCO.Yeye anakaguliwa na nani? Isije ikawa yeye ndiye fisadi nambari wani...

Hilo nalo swali zuri si yeye tu je na makampuni mengine ya ukaguzi yanakaguliwa na nani?????
 
Nimemwona akijigamba kwenda kukagua TANESCO - kilichotokea kwenye issue ya Jairo siwezi kumwani Utouh, wala ofisi ya CAG mpaka huyu bwana aondoke.
 
Hivi mmepata kujiuliza kwanini Blandina Nyoni wakati wake akiwa CAG ufisadi haukuwepo? wadau mnasemaje, huyu mama.... mhhh
 
nyie vipi mbona mapolisi wanajichunguza wenyewe hawaundi tume huru...na yeye ana haki ya kujikagua mwenyewe
 
Sawa na Ikerege wa TBS, kutoa vibali vya ubora lakini hakuna ofisi wala kibanda cha kukagulia.
 
nimesahau section ila CAG anatakiwa kukaguliwa kama ilivyoelezwa kwenye Public Audit Act 2008 na kwa sasa ofisi ya CAG inakaguliwa na TAC ASSOCIATES
 
Hivi mmepata kujiuliza kwanini Blandina Nyoni wakati wake akiwa CAG ufisadi haukuwepo? wadau mnasemaje, huyu mama.... mhhh
duh we mkali! Blandina Nyoni HAJAWAHI kuwa CAG...kwa mujibu wa katiba ukiwa CAG huruhusiwi kufanya kazi nyingine yeyote serikalini
 
Hivi mmepata kujiuliza kwanini Blandina Nyoni wakati wake akiwa CAG ufisadi haukuwepo? wadau mnasemaje, huyu mama.... mhhh
Usichanganye mambo Nyoni hajawahi kuwa CAG. Alikuwa Accountant General. Maana yake ni Mhasibu Mkuu wa serikali.
 
Hivi mmepata kujiuliza kwanini Blandina Nyoni wakati wake akiwa CAG ufisadi haukuwepo? wadau mnasemaje, huyu mama.... mhhh
RUTAJUMBUKIRWA kwa taarifa Blandina Nyoni hakuwahi kuwa CAG; yeye alikuwa Accountant General. Swala kwamba kabla ya Uttoh hakukuwa na ufisadi si kweli tofauti iliyopo ni kuimarika kwa uhuru wa vyombo vya habari tofauti na kipindi cha Mkapa. Tofauti na huko nyuma, siku hizi taarifa ya CAG huwekwa hadharani na hata kamati za kudumu za hesabu za Serikali Kuu, Serikali za mitaa na Mashirika ya umma zimeanza kuongozwa na wapinzani awamu hii ya Kikwete (Kazi nzuri ya Hon. Samweli Sitta) hivyo kupunguza uoga uliokuwepo wa kuhoji matumizi ya serikali na taasisi zake.
 
Last edited by a moderator:
Hilo nalo swali zuri si yeye tu je na makampuni mengine ya ukaguzi yanakaguliwa na nani?????
Lu-ma-ga kampuni za ukaguzi zinawajibika kuwasilisha hesabu zilizokaguliwa TRA kwa mujibu wa Sheria ya Mapato ya mwaka 2004 kama mapato yanazidi 20 million. Vile vile zinawajibika kujiwekea utaratibu wa kupitia ubora wa kazi zao (Cold review) na vile vile kukaguliwa na "regulator" kwa kile kinachoitwa Audit Quality Review (AQR). Kwa maana ingine kazi ya ukaguzi inayofanywa na kampuni ya ukaguzi inaweza kupitiwa na mtu mwingine katika zoezi la Audit Quality Review.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom