Nani asiyejua kwamba Ihefu imechoka?

Mr Alpha

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2018
Posts
273
Reaction score
765
Nani asiyejua kwamba ihefu imeshachoka? Acheni kujisahaulisha hata Namungo anaweza ipiga 5

Ukweli usemwe tu ushindi huu wa Yanga hakuna cha kushangaza nan asiyejua kwamba Ihefu imechoka na kuyumba msimu huu hususan siku za karibuni kabisa? Hiki ni kichekesho aisee Nashangaa kuna watu bila aibu wanashangilia Yanga kuifunga Ihefu goli tano, timu iliyovunjika na kusambaratika iliyokuwa Mbeya ikahamia Arusha iliyopita mabadiliko ya wachezaji na viongozi iliyoyumba

Wakongwe wa hizi kazi wala hatushangai maana hata Barcelona ilipoyumba ilipigwa goli 8 na Bayern Munich nan asiyejua?

Manchester United ilipoyumba ilipigwa goli 7 na Liverpool kuna cha kushangaa kwa Ihefu au tunajitoa tu ufahamu na kuwa wepesi kusahau ndugu zangu?
 
Nani asiyejua kwamba ihefu imeshachoka? acheni kujisahaulisha hata Namungo anaweza ipiga 5

Ukweli usemwe tu ushindi huu wa Yanga hakuna cha kushangaza nan asiyejua kwamba Ihefu imechoka na kuyumba msimu huu hususan siku za karibuni kabisa?...
Kama Ihefu imechoka na imepigwa 5 na Yanga kama ilivyopigwa 5imba, basi 5imba nayo imechoka..!! Maana wote wamelishwa 5.!!
 
Unataka kusema kwamba imechoka kisa imefungwa tano (05)! Simba ilifungwa 05 na Yanga na pia imefungwa 02 na Prisons, je imechoka! Ifike pahali tuuheshimu mpira wa miguu na kujifunza kuthamini jasho la wachezaji uwanjani.
 
Kwa staili hii ligi yetu inaenda kupoteza mvuto kabisa
 
Nani asiyejua kwamba ihefu imeshachoka? acheni kujisahaulisha hata Namungo anaweza ipiga 5

Ukweli usemwe tu ushindi huu wa Yanga hakuna cha kushangaza nan asiyejua kwamba Ihefu imechoka na kuyumba msimu huu hususan siku za karibuni kabisa?...
Wanashangilia ushindi, ushindi una raha yake inawezekana pia hukuuangalia mpira ama unatatixo la uti wa mgongo
 
Ntakuja kukumbusha siku mkicheza nayo! Hii ihefu ya leo simba hamuwezi ifunga
 
Kwa hiyo siyo GSM tena! Dah!! Mashabiki wa simba mtuache tupumzike sasa.
 
Haiwezekani Yanga B iifunge Yanga OG, nitakuwa wa mwisho kuamini

Cha msingi maelekezo ya Boss yaendelee
 
Uzuri kipimo walichopimiwa Ihefu ndicho walichopimiwa na Mikia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…