Nani atafunga paka Kengele - Ndani ya CCM si shwari tena

Nani atafunga paka Kengele - Ndani ya CCM si shwari tena

Shocker

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2012
Posts
1,958
Reaction score
3,890
Ndani ya uongozi wa juu wa CCM hali si shwari tena, kumetibuka vumbi hawaonani na kila mmoja anamtazama Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Unguja.

Kamera nyingi zimewanasa viongozi wa CCM serikalini walio ndani ya Serikali ya Samia Suluhu, wakiwa wamemtolea mimacho kama waliopigwa shoti ya Umeme,macho yanayoomba kutaka kuonewa huruma.

Tiketi ya kugombea Urais Tanzania kupitia CCM ipo wazi (2025)na sasa ni mwendo mdundo ,kuna mivutano mikali uliojaa wanafiki wa kisiasa ,kila mmoja akijiona yeye ndio yeye.

Raisi Samia anaonwa kama amepita wrong turn na hatotaka kuendelea kugombea anaiwacha ngoma uwanjani.
 
Kama Mwigulu Nchemba na Ndugai jana walikuwa wanatoa mimacho ile hatarii
 
Kulikoni mnawakana ndugu zenu si mliwanunua kwa fedha zetu enzi za siasa chafu za hayati.
Hata Yuda Iskarioti vile vipande 30 vya fedha alizopewa ili kumsaliti masihi ziliishia kununua konde la mfinyanzi la kuzikia wageni!
 
Uchunguzi uanzishwe juu ya wale wahamiaji...Je ilikuwa dhamira yao au kuna kilichojificha? kama kulikuwa na blackmailing wasamehewe na warudishiwe fikra na uhuru wao waamue kwa fikra zao sasa.

Kama ni blackmailing, ukweli usemwe na wahusika wachukuliwe hatua.

Mama jitahidi kuruhusu watu waishi kwa fikra huru sasa....kupitia fikra huru ndio mbinu pekee inayoweza kuleta watendaji wenye akili, hekima na busara, tofauti na hapo jamii itaendelea kuona watendaji wanafiki na wafukuza upepo.
 
waache watoe hayo macho hadi ya dodondoke chini. It's not going to help them. another era.
 
Ndani ya uongozi wa juu wa CCM hali si shwari tena,kumetibuka vumbi hawaonani na kila mmoja anamtazama Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Unguja...
Madaraka yalivyo matamu kumung'unya usishangaa Bi.Mkubwa akashinikiza Katiba irekebishwe nae apate angalau 15 yake swaafi kunako Hatamu,

Msinitolee mimacho kwani Viongozi wa Afrika hamuwajui?
 
Back
Top Bottom