Nani awatetee wahusika wa mtoto wa Box?

Nani awatetee wahusika wa mtoto wa Box?

Stream line

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2015
Posts
393
Reaction score
239
Ijulikane kuwa wahusika wa,mtoto wa box wamefungwa kwa miaka 15. Kwa kosa la kuua bila kukusudia. Naapa mbele ya Yahu Eloi wetu Jaji Feleshi hakitoa hukumu ya haki na ya kitaalamu au kisayansi ya sheria.

Kwa nini nasema hivyo; haihitaji kujua kuwa mtoto wa box ameishi ktkt mazingira hayo kwa mda labda wa miaka yote lakini hakufa!! Iweje leo anapotolewa ktk mazingira hayo mtoto wa box anafariki!

Ushauri wangu; Adhabu yao ya kusababisha mateso ndiyo ilikuwa haki yao ya ukiukaji wa haki za binadamu. Mfano, ni dhahiri mtoto alikuwa akijisaidia, na ni lazima ilikuwa kazi kweli ili kumsafisha, hayo ni mateso.

Nani basi aliyemuua mtoto wa box; ni dhahiri aliyemuua mtoto huyo ni wale waliomtoa ktk mazingira yake zoefu na kumpeleka ktk mazingira mapya bila kuzingatia sayansi ya mazingira.

Mfano. Tuitazame hali ya wachimba madini waliookolewa huko Amerika ya kusini. Wale waliandaliwa mazingira (chumba maalumu) kilichofanana na kule shimoni walipokuwa. Mifano ni mingi, kuwa ukimtoa mtu ktk mazingira aliyoyazoea kwa ghafla basi tegemea mtu huyo kufa. Asante.

Mwisho nashauri waokozi wa mtoto Nasra wachukuliwe hatua kali sana kisheria ili kwamba kitu kama hiki kikitokea bali ile sayansi tuliyojifunza mashuleni ifanye kazi na si kukimbilia kufanya kama waliyoyafanya kwa Nasra na kumtisha kwa midoli mtoto.
 
Nayo yaelekea kuwa kama kuna ukweli unaoweza kuungwa mkono. Kwamba kama alipokuwa kwenye boksi hakufa licha ya mazingira magumu na machafu na badala yake anafia kwenye hospitali mikononi mwa wataalam wa afya!
 
Nayo yaelekea kuwa kama kuna ukweli unaoweza kuungwa mkono. Kwamba kama alipokuwa kwenye boksi hakufa licha ya mazingira magumu na machafu na badala yake anafia kwenye hospitali mikononi mwa wataalam wa afya!

Kuna hoja ya msingi hapa, kuna watu wamebeba dhambi za wengine...
 
Back
Top Bottom