Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
KHALIMA BINT KHAMISI MMOJA WA WANAWAKE MSTARI WA MBELE KATIKA KUPIGANIA UHURU WA TANGANYIKA 1954
Kumbukumbu za wazalendo mfano wa Bi. Halima bint Khamis hazipo popote hata ukienda ofisi ya CCM Lumumba Avenue hutaona picha yake katika kuta wala hutaona picha ya yeyote katika wale waliopigania uhuru wa Tanganyika.
Bi. Halima Khamis kwao ni Bagamoyo na kabila yake Mmanyema. Halima Khamis ni mmoja kati ya wengi wazalendo waliofukiwa na historia.
Nimehudhuria shughuli za wanawake kwa kualikwa kama mzungumzaji nimekuta picha zilizowekwa kupamba ukumbi ni za akina mama wengine wengi tu.
Napitia picha moja baada ya nyingine kwa kutegemea labda nitaona picha ya Halima Khamis, Tatu bint Mzee, Hawa bint Maftah, Zarula bint Abdulrahman, Shariffa bint Mzee, Fatma bint Matola, Nyange bint Chande, Amina, Kinabo, Mama bint Mwalimu, Halima Selengia...
Anaeoneka katika picha hizi ni Bibi Titi Mohamed peke yake. Kuta zote zimejaa wazalendo akina mama wapya wa leo.
Kwa nini iwe hivi?
Hiyo picha hapo juu ni Bi. Halima Khamis akisalimiana na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mbele ya Ukumbi wa Diamond.
Bi. Halima na Mwalimu Nyerere walikuwa hawajaonana kwa miaka mingi sana. Wanasema ile nafasi ya Bibi Titi ilikuwa ama achukue Bibi Titi au Halima Khamis kwani vipaji vyao vikilingana kwa karibu sana.
Bahati ilimwangukia Bibi Titi.
Wakati ule wa harakati miaka ya 1950 Halima Khamisi alikuwa msichana mdogo chini ya miaka 30 akisomesha watoto Qur'an kwenye madrasa yake mwenyewe Mtaa wa Kariakoo na Livingstone si mbali na ofisi ya TANU Mtaa wa New Street na Kariakoo.
Hawa ndiyo wale akina mama wa mabaibui waliotajwa na Mama Maria Nyerere waliopigania uhuru wa Tanganyika.
Bi Halima Khamis
Bibi Titi Mohamed