Rev. Kishoka
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 4,526
- 1,540
Mkuu hapa tatizo umeshindwa kuangalia mambo kwa upana wake, hatukatai kwamba vitu vimepanda bei. Na wanafunzi wamekuwa na akili hawajakugomea wewe maana najua wewe kama huna daladala basi rafiki yako analo.
Wanafunzi wanajua kabisa aliyezembea mambo yakaharibika hapa ni serikali, maswala ya vitu kupanda na kushuka bei ni maswala ambayo serikali inatakiwa iyajue kabla ya madhara na ndio maana kuna wataalamu wa uchumi kwa ajili ya economic forecasts. Kazi yao ni kujua mwaka kesho hakuna chakula kwahiyo serikali itenge fungu la chakula, kuna uwezekano wa vita middle east kwahiyo mafuta yatapanda na serikali inatakiwa kufanya jambo kukabiliana na madhara, mabenki ya kigeni yanahujumu uchumi kwahiyo yabanwe kwa njia gani ili uchumi wetu usitetereke na mengine mengi kama hayo.
Sasa hapa inaonekana hao wahusika wako bize kupanga namna ya kula faranga ambazo hata ziliwekwa hazina kama insurance incase of emergency, sasa unadhani watapata wapi muda wa kufikiria kwamba jiji linakua, huduma zinahitajika zaidi tena za kisasa zaidi? watapata wapi muda wa kufikiria kwamba shule na wanafunzi wanaongezeka kila kukicha? hawana muda. Pinda alisema JK yuko bize hasa baada ya kupewa jukumu la AU, maana yake mkiona mambo mengine yanakwama mjue JK yuko bize na AU, Darfur, Zimbabwe etc...
Tanzania kichwa cha mwendawazimu, we never plan for future,we toy around with present and never learn from the past!