Nani hasa aliwaingiza Wakurya wengi Jeshini?

Mkuu kwani yeye kazungumzia kipindi hiki au kipindi kile afu mbona majibu yote kakupa hapo juu
 
Kabla sijaanza Kukujibu swali lako labda nami kidogo tu nikuulize ' Kajiswali ' haka kwamba hivi umeshawahi kujiuliza ni kwanini ukiingia Mikoa yote nchini Tanzania unakaribishwa na maneno ya ' Karibu Mkoa fulani ' ila ukiwa unaingia tu Mkoa wa Mara unakaribishwa na hili neno ' Sasa unaingia Mkoa wa Mara gangamala? ' Ukimalizia hako ' Kajiswali ' nakuongezea kingine kwamba umeshawahi kujiuliza ni kwanini ' Jando ' zote za Makabila ya Mikoa yote Mtoto wa Kiume akifanyiwa huwa anabembelezwa, anapewa Chips Mayai na Soda na anapigwa Ganzi ila Mtoto wa Kiume wa Mkoa wa Mara akiwa anafanyiwa ' Jando ' anakuwa amefungwa mikono yote nyuma huku Uume wake ukiwa umewekwa katika Jiwe na wale Wazee wanaukata na Kuutahiri kwa Panga au Kisu Kikali asubuhi tena bila Ganzi yoyote na kisha wanarejea jioni kabisa kumaliza Kazi yote?

Mikoa yote nchini Tanzania kuna Wanaume ila Mkoa wa Mara peke yake ndiyo kuna Wanamume na ndiyo maana katika Majeshi yote ya Ulinzi na Usalama pamoja na Taasisi zote ' Nyeti ' unazozijua Wewe huwezi kumkosa Mtu wa Mara na hata Watu wengine mkiwa nao na wakijua tu kwamba katika hilo Kundi lao ipo ' Njemba ' moja kutoka Mkoani Mara basi Watu huwa na furaha na wanaamini kwamba wapo au watakuwa salama.

Hakuna Mkoa ninaoupenda Tanzania nzima kama wa Mara ( Musoma )
 
Nimependa hii story. Binafsi nimeishi na Wakurya (Watimbaru na Wanyamongo), wale watu ni majembe. Natamani ningeishi huko jumla.
- Ni marafiki wazuri, wakarimu ila kuwa makini na mambo ya ovyo kama kutembea na wake zao, utapata mshahara on the spot.
- Unapoiba vitu kama ng'ombe au pesa na kuleta kwao wewe ni shujaa.
- Usijichanganye ukaiba kwao ukipeleka sehemu nyingine.
- Wanaogopa sana ushirikina zaidi ya panga.
- Ukibahatika kuzaa na mke wake mtoto (hasa wa kike ili apate ng'ombe baada ya kuolewa) mtoto ni mali yake hata akifahamu.
- Vijijini kilevi cha b...ngi ni maarufu kuliko pombe. Mtoto anaweza kupuriza mbele ya mzazi wake.
- Wana mfumo madhubuti wa kutunza siri. Mtu anaweza kuuawa watu wote wakiona ila hakuna mtu anayeweza kusema hadharani nani ameua.
- Kijana akishatahiriwa ni mtu mzima mwenzio. Anaweza kuchangamana na watu wazima na hata kuanzisha fujo (kisu kinakuwa mfukoni).
- Wengi wao ikimpa siraha (hata panga tu, anaamini anaweza kufanya chochote atakacho. Fikiria akipewa zile zana wanazotuoneshwa na TPDF uwanja wa taifa atajisiaje?)

Ninawapongeza siyo watu legelege. Kama waliingizwa jeshini kwa kigezo hiki, hakika hawakukosea.
 
Narudia mara ya mwisho hakuna kabila la wakurya, Wakurya ni mkusanyiko wa makabila mbali mbali kutoka mkoa wa Mara na hilo neno wakurya ni region ipo Kenya karibu na boarder ya Tanzania ina itwa Kurya county
kwahiyo wanaojiita wakurya wanakosea? haya wape jina lako sasa...
 
Asante kwa nyongeza nzuri sana na kiuhakika mfumo wa maisha yao umekaa katika hali kama unavyoona ya kijeshi kinidhamu na utekelezaji wa majukumu.
 
Kuna member mmoja amenifuata inbox kutaka kujua asili ya wakurya...sasa nimeamua kuitoa kiasi kwa jinsi nilivyosoma maandiko tofauti tofauti huko nyuma anaweza kuja huku na kuisoma pia.

HISTORIA YA WAKURYA NA ASILI YAO

Asili ya Wakurya ni Misri, walifika Congo kati ya 322. KK
Hapo zamani kulikuwa na mtu aliyeitwa monto, huyu ni mzazi wa wabantu wote.

Monto alizaa Range miongoni mwa wanae, Range alizaa Magaiwa, Magaiwa alizaa, alimzaa Mkurya.

Mkurya alizaa watoto watano ambao ni Nyanchage, Wangwe, Mongoso, Nano na Mendi.

Nyanchage aliwazaa Mtimbaru, Mosi, na Mosonga hawa ndio tunawaita inchage.

Wangwe aliwazaa Moracha, Mwirege, Keroba, Mugumbe na Gisiri. Hawa ndio tunaowaita Engwe, kemoramba yagesaka.

Watu walivyozidi kuongezeka ukoo wa Gisiri ulikimbilia umasaini nao huitwa Osiri hadi leo huko umasaini.

Kutokana na kosa alilolifanya Gisiri, (ni stori ndefu), ukoo wa Moracha ulibadili jina ukaitwa abanyamongo (wenye maghala ya chakula)
Ukoo wa Mugumbe ulibadili jina ukaitwa abalenchoka (wala nyoka, waliishi mlima wa nyoka).

Mongoso alimzaa Mkira, mtoto pekee. Huyu ndo mzazi wa abakira na maana ya MongoMongoso leo ni tembo dume.

Nano aliwazaa Mokenye, Musweta na Msimbete. Hawa ndio waitwao inano yaani nyani.
Kutokana na hawa waliibuka watu mbalimbali kama abakine, abarieri, abamera, abanyanccha na abangoreme.

Mendi alizaa mtoto mmoja tu Munchari, hawa hujiitia emendi yaani panya mdogo au irigeki.


KUHUSU MAJINA


Wakurya wana majina sita ya wazaliwa wa kwanza. Matatu ya kiume na matatu ya kike.

Naanza na ya kiume Mwita, Marwa na Chacha. Nitamaliza na ya kike Ghati, Bhoke na Rhobi

Mwita asili yake ni uguita, yaani kuua/Kifo. Wakurya kitu kinachowashinda kupambana nacho huamua kukienzi. Kifo kiliwashinda wakaamua wakienzi kwa kuwapa wazaliwa wa kwanza jina hilo ie to familiarize with that misfortune!!! Ili wakizoeee

Chacha asili yake zimekuja, ni jina walilopewa watoto wa kiume waliozaliwa wakati ng'ombe zimeibwa au zimeletwa toka umasaini au usukumani. Wakurya huamini ng'ombe wote ni wao, hivyo ni kama waliporwa, kwa hiyo vijana walipoenda kuiba ilikuwa sio kuiba ila kuzifuata na kuzileta. Zimekuja/Chacha.

Marwa ni pombe iliyoandaliwa na kunywewa kusherehekea ng'ombe zilizoletwa.

Kwa wanawake,
Bhoke ni asali, kitamu, kitu kilichopatikana bila jasho na kitakacholeta vitamu. Hupewa mtoto wa kike kwa sababu huleta ng'ombe bila jasho, ni baraka kwa familia. Linganisha ng'ombe anazoleta Bhoke na zile za kuiba, zinazopatikana kwa kumwaga hata damu. Kwa hiyo ni asali /Bhoke.

Rhobi hutokana na neno Erhobilo, hii ni shangwe inayofanywa na wanawake na wanaume kufuatia tukio zuri kama kurudisha ng'ombe zilizoibwa. Shangwe hiyo ikifanywa na wanaume pekee huitwa engoliga. Lkn wafata nyayo wanapofika nyumbani nyimbo zao huimbwa na wote, na hapo huitwa Erhobilo, ndo asili ya jina Rhobi

Ghati, hutokana na neno la kimaumbile yaani umbile la mwanamke (uke). Kilichofanya likastaajabiwa ni kuwa mke na mume hulala pamoja, inakuwaje mwanamke abebe ujauzito lkn sio mwanaume? Hivyo Ghati maana yake oghotia au kupasuka. Kwamba wamepasuka ndo maana wanabeba ujauzito. Hili ni jina la kuenzi umbile la wanawake

Ndoa za kimira. Kwa Wakurya.

Nyumba nthobhu, mwanamke aliyezaa watoto wa kike tu, ili atakapokufa baadae nyumba yake isitoweke huamua kuoa binti wa kuendeleza uzao wa nyumba yake

Nyumba mboke ni kama mwanamke hakuzaa kabisa iwe binti wala mvulana, huyu huoa ili apate uzao

Nyumba ntune ni kama kijana alizaliwa kwao na vijana wengine au peke yake, lkn bahati mbaya akafa kabla ya kuoa hasa kama alikuwa amepita umri wa utoto (ubhulisia). Hivyo familia hukaa na kupanga kuoa mke wa kufufua jina la kijana huyo aliyekufa

Nyumba nyana ni aina ya ndoa ambayo mwanaume anayeoa ni taahira au kilema au zezeta. Kwa kuwa jina la mwanaume halipotei ukuryani, basi ndugu wa familia huombwa kuoa na kuzaa watoto lkn watoto ni wa huyo kilema ambaye kwa kawaida anakuwa hawezi majukumu ya kutungisha au kulea

Nyumba nguru, inatokea kama familia haikubahatika kupata mtoto wa kiume mapema, lkn baadae akazaliwa wazazi wakiwa wazee na wamekata tamaa. Huyo mtoto huolewa mwanamke ambaye huja kuzaa kuendeleza uzao wa mtoto. Mtoto huyu akikua huchagua aidha kukubali huyo mke au vinginevyo lkn mwisho wa siku ni familia yake.

Eteto ni aina ya ndoa ya kawaida. Mwanaume anaoa mke wake au mke wa pili (okohareka).

Ikumbukwe Kuwa, awali mwanaume wa kuoa aina ya ndoa hapo juu ni yule aliyechaguliwa kutoka kwenye ukoo au familia ya wahusika.
 
Narudia mara ya mwisho hakuna kabila la wakurya, Wakurya ni mkusanyiko wa makabila mbali mbali kutoka mkoa wa Mara na hilo neno wakurya ni region ipo Kenya karibu na boarder ya Tanzania ina itwa Kurya county

bullar,
Mkuu

Haa haaa haaa haaa.

Ngoja kwanza nicheke.

Haa haaa haa haaa haaaa.

Nitarudi kukujibu badae.
 
Hujawahi kuongea nao hata mmoja? Mkuu ww unakaa Libya nini?
 
Tatigha ,
Mkuu,
Haa haaa haaa Libya pasikie tu mkuu kwenye vyombo vya habari n akusoma.kwenye atlas siyo kabisa.
Hahaha sasa inakuaje hujawahi kuongea na mkurya hata mmoja ,

Nikajua na wewe umezamia Libya maana huko bado wakurya hawajafika
 
Hahaha sasa inakuaje hujawahi kuongea na mkurya hata mmoja ,

Nikajua na wewe umezamia Libya maana huko bado wakurya hawajafika

Tatigha ,
Mkuu,
Maisha tu.
Labda huku nilipo sijawaona.

Nasikia kuwa watu wanawaogopa sana na wakiwa eneo wanajitambulisha kama.wajita au wajaluo
 
Oghambele bhuya monto weito. Nobhamanyere abhakurya bhuyaa muraa
 
Tatigha ,
Mkuu,
Maisha tu.
Labda huku nilipo sijawaona.

Nasikia kuwa watu wanawaogopa sana na wakiwa eneo wanajitambulisha kama.wajita au wajaluo
Duuuuu sio kweli yaani mkurya ajitambulishe yeye mjita au mjaluo??

Mbona mimi huwa sijitbulishi hivyo.....
 
Naomba kutofautiana na wewe! Historia ya recruitment jeshini ilianza mara baada ya Tanganyika kuwa chini ya utawala wa waingereza. Kwa wanaojua historia ya waingereza walivyo wako "very tradtional". Wanaamini kabisa kuwa asili ya mtu ndiyo hatima yake kimaisha. Yaani kama wewe asili ya ukoo wako ni wakulima hakuna jinsi unavyoweza ukaepuka kuwa mkulima siku za usoni.
Kwa hiyo katika miaka ya mwanzo ya ukoloni wa Uingereza yalifanyika maandalizi ya kuandaa askari ambao wataingizwa kwenye Jeshi la KAR. Waingereza walifanya utafiti kwa misingi hii kwamba ni makabila gani katika historia ya Tanganyika ambayo hayakuingiliwa kirahisi na watu weupe. Kwenye utafiti huo Wakurya au watu wa mkoa wa Mara walikuwa either namba 1 au namba mbili na wahehe sina kumbukumbu sahihi hapo.
Recruitment officer alikuwa anatoka Uingereza na kazi yake ilikuwa ni moja tu : kutafuta askari material wa KAR. Kwenye "brief" alikuwa anapewa mikoa gani anatakiwa achague na mikoa gani apite tu kama hana habari. Mikoa kama ya Pwani aliambiwa apitilize tu. Aende Mara, Iringa, Songea na kidogo Tabora. KAR imeanza na askari wengi kutoka mikoa hii. The last recruitment officer nakumbuka alikuwa anaitwa Major Callaghan miaka ya 60. Utaratibu huu ulisitishwa na Nyerere ambaye aliruhusu makabila yote kuingia TPDF na ndiyo mpaka leo utaratibu ni huo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…