Nani hasa aliwaingiza Wakurya wengi Jeshini?

Nani hasa aliwaingiza Wakurya wengi Jeshini?

Hii story imejaa uongo kiasi,na hakuna utafiti uliofanya,sasa kipi ni kipi wakurya walikimbilia jeshini kwa sababu ya kukosa fulsa zingine za kiuchumi? Au wanalipenda jeshi? Maana kama kipindi hicho,wangepewa fulsa za elimu kama zilizokuwepo kwa wahaya,Chaga,na Wanyakyusa,je wangeenda jeshini?
Leo hii ukitoa nafasi 10000,kwa kila mkoa,unataka kutuaminisha kwa sababu wakurya wanapenda vita,basi hizo nafasi kwao zitakuwa chache,kwa wengine hata nusu haitafika?
Ndugu,ukiona maprofesa waliojaa UDSM ni wahaya,wachaga,Wanyakyusa,na hakuna hata mndengereko au mzaramu,mmakuwa,mmakonde,sio kwamba hayo makabila mengine hayapendi elimu,kutokuwepo kwao kwa wingi kwenye hiyo sekta,ni pamoja na sababu za kihistoria,
Kila jamii imesaidiwa au imedidimizwa na utamaduni wao,au historia ya kikoloni,
Uhayani mfumo wa shule za IATA,ambazo zinachangiwa na wakazi wa sehemu husika,ulianza kitambo sana,na makanisa yalichangia sana,
Kila MTU kutoka jamii yoyote kuanzia,mmakuwa wa masasi,mpaka mchaga wa moshi,mzaramo wa dar,hadi muha wa kigoma,anaweza kufanya kazi sekta yoyote,iwe JWTZ,TISS,au wasiojurikana,iwe sayansi,
Suala hapa ni fulsa tu,
Sasa HV ukitoa nafasi za JWTZ,kila mkoa,wapi zitajaa haraka,na kwa nini?,Lindi,Mtwara,Kigoma,Mara,Kagera,je ni kwa sababu watu wanapenda jeshi na vita,au vyuma vimekaza,hawa wengine kama hawakulipenda zamani,nini kinawafanya walipende sasa HV?,
Tusidanganyane,kipindi hiki,una angalia maslahi ya kifedha kwanza,mengine baade,
Mkuu kwani yeye kazungumzia kipindi hiki au kipindi kile afu mbona majibu yote kakupa hapo juu
 
Kabla sijaanza Kukujibu swali lako labda nami kidogo tu nikuulize ' Kajiswali ' haka kwamba hivi umeshawahi kujiuliza ni kwanini ukiingia Mikoa yote nchini Tanzania unakaribishwa na maneno ya ' Karibu Mkoa fulani ' ila ukiwa unaingia tu Mkoa wa Mara unakaribishwa na hili neno ' Sasa unaingia Mkoa wa Mara gangamala? ' Ukimalizia hako ' Kajiswali ' nakuongezea kingine kwamba umeshawahi kujiuliza ni kwanini ' Jando ' zote za Makabila ya Mikoa yote Mtoto wa Kiume akifanyiwa huwa anabembelezwa, anapewa Chips Mayai na Soda na anapigwa Ganzi ila Mtoto wa Kiume wa Mkoa wa Mara akiwa anafanyiwa ' Jando ' anakuwa amefungwa mikono yote nyuma huku Uume wake ukiwa umewekwa katika Jiwe na wale Wazee wanaukata na Kuutahiri kwa Panga au Kisu Kikali asubuhi tena bila Ganzi yoyote na kisha wanarejea jioni kabisa kumaliza Kazi yote?

Mikoa yote nchini Tanzania kuna Wanaume ila Mkoa wa Mara peke yake ndiyo kuna Wanamume na ndiyo maana katika Majeshi yote ya Ulinzi na Usalama pamoja na Taasisi zote ' Nyeti ' unazozijua Wewe huwezi kumkosa Mtu wa Mara na hata Watu wengine mkiwa nao na wakijua tu kwamba katika hilo Kundi lao ipo ' Njemba ' moja kutoka Mkoani Mara basi Watu huwa na furaha na wanaamini kwamba wapo au watakuwa salama.

Hakuna Mkoa ninaoupenda Tanzania nzima kama wa Mara ( Musoma )
 
Nimependa hii story. Binafsi nimeishi na Wakurya (Watimbaru na Wanyamongo), wale watu ni majembe. Natamani ningeishi huko jumla.
- Ni marafiki wazuri, wakarimu ila kuwa makini na mambo ya ovyo kama kutembea na wake zao, utapata mshahara on the spot.
- Unapoiba vitu kama ng'ombe au pesa na kuleta kwao wewe ni shujaa.
- Usijichanganye ukaiba kwao ukipeleka sehemu nyingine.
- Wanaogopa sana ushirikina zaidi ya panga.
- Ukibahatika kuzaa na mke wake mtoto (hasa wa kike ili apate ng'ombe baada ya kuolewa) mtoto ni mali yake hata akifahamu.
- Vijijini kilevi cha b...ngi ni maarufu kuliko pombe. Mtoto anaweza kupuriza mbele ya mzazi wake.
- Wana mfumo madhubuti wa kutunza siri. Mtu anaweza kuuawa watu wote wakiona ila hakuna mtu anayeweza kusema hadharani nani ameua.
- Kijana akishatahiriwa ni mtu mzima mwenzio. Anaweza kuchangamana na watu wazima na hata kuanzisha fujo (kisu kinakuwa mfukoni).
- Wengi wao ikimpa siraha (hata panga tu, anaamini anaweza kufanya chochote atakacho. Fikiria akipewa zile zana wanazotuoneshwa na TPDF uwanja wa taifa atajisiaje?)

Ninawapongeza siyo watu legelege. Kama waliingizwa jeshini kwa kigezo hiki, hakika hawakukosea.
 
bullar,
Mkuu,

Aiseeeeh,
Hiyo historia umesoma wapi mbona mimi tangia nazaliwa na kusoma nimeaminishwa kuwa hapo Tanzania kuna kabila au jamii ya wakurya!?

Zaidi, ya hapo nasikia kuwa hiyo jamii siyo watu wa kisportsport japo sijawahi kuongea hata na mmoja wao.

Hadi Miss Ritah , hataki kabisa hata kuwasikia wakurya maana anawaogopa!
Narudia mara ya mwisho hakuna kabila la wakurya, Wakurya ni mkusanyiko wa makabila mbali mbali kutoka mkoa wa Mara na hilo neno wakurya ni region ipo Kenya karibu na boarder ya Tanzania ina itwa Kurya county
kwahiyo wanaojiita wakurya wanakosea? haya wape jina lako sasa...
 
Asante kwa nyongeza nzuri sana na kiuhakika mfumo wa maisha yao umekaa katika hali kama unavyoona ya kijeshi kinidhamu na utekelezaji wa majukumu.
 
Kuna member mmoja amenifuata inbox kutaka kujua asili ya wakurya...sasa nimeamua kuitoa kiasi kwa jinsi nilivyosoma maandiko tofauti tofauti huko nyuma anaweza kuja huku na kuisoma pia.

HISTORIA YA WAKURYA NA ASILI YAO

Asili ya Wakurya ni Misri, walifika Congo kati ya 322. KK
Hapo zamani kulikuwa na mtu aliyeitwa monto, huyu ni mzazi wa wabantu wote.

Monto alizaa Range miongoni mwa wanae, Range alizaa Magaiwa, Magaiwa alizaa, alimzaa Mkurya.

Mkurya alizaa watoto watano ambao ni Nyanchage, Wangwe, Mongoso, Nano na Mendi.

Nyanchage aliwazaa Mtimbaru, Mosi, na Mosonga hawa ndio tunawaita inchage.

Wangwe aliwazaa Moracha, Mwirege, Keroba, Mugumbe na Gisiri. Hawa ndio tunaowaita Engwe, kemoramba yagesaka.

Watu walivyozidi kuongezeka ukoo wa Gisiri ulikimbilia umasaini nao huitwa Osiri hadi leo huko umasaini.

Kutokana na kosa alilolifanya Gisiri, (ni stori ndefu), ukoo wa Moracha ulibadili jina ukaitwa abanyamongo (wenye maghala ya chakula)
Ukoo wa Mugumbe ulibadili jina ukaitwa abalenchoka (wala nyoka, waliishi mlima wa nyoka).

Mongoso alimzaa Mkira, mtoto pekee. Huyu ndo mzazi wa abakira na maana ya MongoMongoso leo ni tembo dume.

Nano aliwazaa Mokenye, Musweta na Msimbete. Hawa ndio waitwao inano yaani nyani.
Kutokana na hawa waliibuka watu mbalimbali kama abakine, abarieri, abamera, abanyanccha na abangoreme.

Mendi alizaa mtoto mmoja tu Munchari, hawa hujiitia emendi yaani panya mdogo au irigeki.

KUHUSU MAJINA

Wakurya wana majina sita ya wazaliwa wa kwanza. Matatu ya kiume na matatu ya kike.

Naanza na ya kiume Mwita, Marwa na Chacha. Nitamaliza na ya kike Ghati, Bhoke na Rhobi

Mwita asili yake ni uguita, yaani kuua/Kifo. Wakurya kitu kinachowashinda kupambana nacho huamua kukienzi. Kifo kiliwashinda wakaamua wakienzi kwa kuwapa wazaliwa wa kwanza jina hilo ie to familiarize with that misfortune!!! Ili wakizoeee

Chacha asili yake zimekuja, ni jina walilopewa watoto wa kiume waliozaliwa wakati ng'ombe zimeibwa au zimeletwa toka umasaini au usukumani. Wakurya huamini ng'ombe wote ni wao, hivyo ni kama waliporwa, kwa hiyo vijana walipoenda kuiba ilikuwa sio kuiba ila kuzifuata na kuzileta. Zimekuja/Chacha.

Marwa ni pombe iliyoandaliwa na kunywewa kusherehekea ng'ombe zilizoletwa.

Kwa wanawake,
Bhoke ni asali, kitamu, kitu kilichopatikana bila jasho na kitakacholeta vitamu. Hupewa mtoto wa kike kwa sababu huleta ng'ombe bila jasho, ni baraka kwa familia. Linganisha ng'ombe anazoleta Bhoke na zile za kuiba, zinazopatikana kwa kumwaga hata damu. Kwa hiyo ni asali /Bhoke.

Rhobi hutokana na neno Erhobilo, hii ni shangwe inayofanywa na wanawake na wanaume kufuatia tukio zuri kama kurudisha ng'ombe zilizoibwa. Shangwe hiyo ikifanywa na wanaume pekee huitwa engoliga. Lkn wafata nyayo wanapofika nyumbani nyimbo zao huimbwa na wote, na hapo huitwa Erhobilo, ndo asili ya jina Rhobi

Ghati, hutokana na neno la kimaumbile yaani umbile la mwanamke (uke). Kilichofanya likastaajabiwa ni kuwa mke na mume hulala pamoja, inakuwaje mwanamke abebe ujauzito lkn sio mwanaume? Hivyo Ghati maana yake oghotia au kupasuka. Kwamba wamepasuka ndo maana wanabeba ujauzito. Hili ni jina la kuenzi umbile la wanawake

Ndoa za kimira. Kwa Wakurya.

Nyumba nthobhu, mwanamke aliyezaa watoto wa kike tu, ili atakapokufa baadae nyumba yake isitoweke huamua kuoa binti wa kuendeleza uzao wa nyumba yake

Nyumba mboke ni kama mwanamke hakuzaa kabisa iwe binti wala mvulana, huyu huoa ili apate uzao

Nyumba ntune ni kama kijana alizaliwa kwao na vijana wengine au peke yake, lkn bahati mbaya akafa kabla ya kuoa hasa kama alikuwa amepita umri wa utoto (ubhulisia). Hivyo familia hukaa na kupanga kuoa mke wa kufufua jina la kijana huyo aliyekufa

Nyumba nyana ni aina ya ndoa ambayo mwanaume anayeoa ni taahira au kilema au zezeta. Kwa kuwa jina la mwanaume halipotei ukuryani, basi ndugu wa familia huombwa kuoa na kuzaa watoto lkn watoto ni wa huyo kilema ambaye kwa kawaida anakuwa hawezi majukumu ya kutungisha au kulea

Nyumba nguru, inatokea kama familia haikubahatika kupata mtoto wa kiume mapema, lkn baadae akazaliwa wazazi wakiwa wazee na wamekata tamaa. Huyo mtoto huolewa mwanamke ambaye huja kuzaa kuendeleza uzao wa mtoto. Mtoto huyu akikua huchagua aidha kukubali huyo mke au vinginevyo lkn mwisho wa siku ni familia yake.

Eteto ni aina ya ndoa ya kawaida. Mwanaume anaoa mke wake au mke wa pili (okohareka).

Ikumbukwe Kuwa, awali mwanaume wa kuoa aina ya ndoa hapo juu ni yule aliyechaguliwa kutoka kwenye ukoo au familia ya wahusika.
 
Narudia mara ya mwisho hakuna kabila la wakurya, Wakurya ni mkusanyiko wa makabila mbali mbali kutoka mkoa wa Mara na hilo neno wakurya ni region ipo Kenya karibu na boarder ya Tanzania ina itwa Kurya county

bullar,
Mkuu

Haa haaa haaa haaa.

Ngoja kwanza nicheke.

Haa haaa haa haaa haaaa.

Nitarudi kukujibu badae.
 
bullar,
Mkuu,

Aiseeeeh,
Hiyo historia umesoma wapi mbona mimi tangia nazaliwa na kusoma nimeaminishwa kuwa hapo Tanzania kuna kabila au jamii ya wakurya!?

Zaidi, ya hapo nasikia kuwa hiyo jamii siyo watu wa kisportsport japo sijawahi kuongea hata na mmoja wao.

Hadi Miss Ritah , hataki kabisa hata kuwasikia wakurya maana anawaogopa!
Hujawahi kuongea nao hata mmoja? Mkuu ww unakaa Libya nini?
 
Tatigha ,
Mkuu,
Haa haaa haaa Libya pasikie tu mkuu kwenye vyombo vya habari n akusoma.kwenye atlas siyo kabisa.
Hahaha sasa inakuaje hujawahi kuongea na mkurya hata mmoja ,

Nikajua na wewe umezamia Libya maana huko bado wakurya hawajafika
 
Hahaha sasa inakuaje hujawahi kuongea na mkurya hata mmoja ,

Nikajua na wewe umezamia Libya maana huko bado wakurya hawajafika

Tatigha ,
Mkuu,
Maisha tu.
Labda huku nilipo sijawaona.

Nasikia kuwa watu wanawaogopa sana na wakiwa eneo wanajitambulisha kama.wajita au wajaluo
 
Kuna member mmoja amenifuata inbox kutaka kujua asili ya wakurya...sasa nimeamua kuitoa kiasi kwa jinsi nilivyosoma maandiko tofauti tofauti huko nyuma anaweza kuja huku na kuisoma pia.

HISTORIA YA WAKURYA NA ASILI YAO

Asili ya Wakurya ni Misri, walifika Congo kati ya 322. KK
Hapo zamani kulikuwa na mtu aliyeitwa monto, huyu ni mzazi wa wabantu wote.

Monto alizaa Range miongoni mwa wanae, Range alizaa Magaiwa, Magaiwa alizaa, alimzaa Mkurya.

Mkurya alizaa watoto watano ambao ni Nyanchage, Wangwe, Mongoso, Nano na Mendi.

Nyanchage aliwazaa Mtimbaru, Mosi, na Mosonga hawa ndio tunawaita inchage.

Wangwe aliwazaa Moracha, Mwirege, Keroba, Mugumbe na Gisiri. Hawa ndio tunaowaita Engwe, kemoramba yagesaka.

Watu walivyozidi kuongezeka ukoo wa Gisiri ulikimbilia umasaini nao huitwa Osiri hadi leo huko umasaini.

Kutokana na kosa alilolifanya Gisiri, (ni stori ndefu), ukoo wa Moracha ulibadili jina ukaitwa abanyamongo (wenye maghala ya chakula)
Ukoo wa Mugumbe ulibadili jina ukaitwa abalenchoka (wala nyoka, waliishi mlima wa nyoka).

Mongoso alimzaa Mkira, mtoto pekee. Huyu ndo mzazi wa abakira na maana ya MongoMongoso leo ni tembo dume.

Nano aliwazaa Mokenye, Musweta na Msimbete. Hawa ndio waitwao inano yaani nyani.
Kutokana na hawa waliibuka watu mbalimbali kama abakine, abarieri, abamera, abanyanccha na abangoreme.

Mendi alizaa mtoto mmoja tu Munchari, hawa hujiitia emendi yaani panya mdogo au irigeki.

KUHUSU MAJINA

Wakurya wana majina sita ya wazaliwa wa kwanza. Matatu ya kiume na matatu ya kike.

Naanza na ya kiume Mwita, Marwa na Chacha. Nitamaliza na ya kike Ghati, Bhoke na Rhobi

Mwita asili yake ni uguita, yaani kuua/Kifo. Wakurya kitu kinachowashinda kupambana nacho huamua kukienzi. Kifo kiliwashinda wakaamua wakienzi kwa kuwapa wazaliwa wa kwanza jina hilo ie to familiarize with that misfortune!!! Ili wakizoeee

Chacha asili yake zimekuja, ni jina walilopewa watoto wa kiume waliozaliwa wakati ng'ombe zimeibwa au zimeletwa toka umasaini au usukumani. Wakurya huamini ng'ombe wote ni wao, hivyo ni kama waliporwa, kwa hiyo vijana walipoenda kuiba ilikuwa sio kuiba ila kuzifuata na kuzileta. Zimekuja/Chacha.

Marwa ni pombe iliyoandaliwa na kunywewa kusherehekea ng'ombe zilizoletwa.

Kwa wanawake,
Bhoke ni asali, kitamu, kitu kilichopatikana bila jasho na kitakacholeta vitamu. Hupewa mtoto wa kike kwa sababu huleta ng'ombe bila jasho, ni baraka kwa familia. Linganisha ng'ombe anazoleta Bhoke na zile za kuiba, zinazopatikana kwa kumwaga hata damu. Kwa hiyo ni asali /Bhoke.

Rhobi hutokana na neno Erhobilo, hii ni shangwe inayofanywa na wanawake na wanaume kufuatia tukio zuri kama kurudisha ng'ombe zilizoibwa. Shangwe hiyo ikifanywa na wanaume pekee huitwa engoliga. Lkn wafata nyayo wanapofika nyumbani nyimbo zao huimbwa na wote, na hapo huitwa Erhobilo, ndo asili ya jina Rhobi

Ghati, hutokana na neno la kimaumbile yaani umbile la mwanamke (uke). Kilichofanya likastaajabiwa ni kuwa mke na mume hulala pamoja, inakuwaje mwanamke abebe ujauzito lkn sio mwanaume? Hivyo Ghati maana yake oghotia au kupasuka. Kwamba wamepasuka ndo maana wanabeba ujauzito. Hili ni jina la kuenzi umbile la wanawake

Ndoa za kimira. Kwa Wakurya.

Nyumba nthobhu, mwanamke aliyezaa watoto wa kike tu, ili atakapokufa baadae nyumba yake isitoweke huamua kuoa binti wa kuendeleza uzao wa nyumba yake

Nyumba mboke ni kama mwanamke hakuzaa kabisa iwe binti wala mvulana, huyu huoa ili apate uzao

Nyumba ntune ni kama kijana alizaliwa kwao na vijana wengine au peke yake, lkn bahati mbaya akafa kabla ya kuoa hasa kama alikuwa amepita umri wa utoto (ubhulisia). Hivyo familia hukaa na kupanga kuoa mke wa kufufua jina la kijana huyo aliyekufa

Nyumba nyana ni aina ya ndoa ambayo mwanaume anayeoa ni taahira au kilema au zezeta. Kwa kuwa jina la mwanaume halipotei ukuryani, basi ndugu wa familia huombwa kuoa na kuzaa watoto lkn watoto ni wa huyo kilema ambaye kwa kawaida anakuwa hawezi majukumu ya kutungisha au kulea

Nyumba nguru, inatokea kama familia haikubahatika kupata mtoto wa kiume mapema, lkn baadae akazaliwa wazazi wakiwa wazee na wamekata tamaa. Huyo mtoto huolewa mwanamke ambaye huja kuzaa kuendeleza uzao wa mtoto. Mtoto huyu akikua huchagua aidha kukubali huyo mke au vinginevyo lkn mwisho wa siku ni familia yake.

Eteto ni aina ya ndoa ya kawaida. Mwanaume anaoa mke wake au mke wa pili (okohareka).

Ikumbukwe Kuwa, awali mwanaume wa kuoa aina ya ndoa hapo juu ni yule aliyechaguliwa kutoka kwenye ukoo au familia ya wahusika.
Oghambele bhuya monto weito. Nobhamanyere abhakurya bhuyaa muraa
 
Tatigha ,
Mkuu,
Maisha tu.
Labda huku nilipo sijawaona.

Nasikia kuwa watu wanawaogopa sana na wakiwa eneo wanajitambulisha kama.wajita au wajaluo
Duuuuu sio kweli yaani mkurya ajitambulishe yeye mjita au mjaluo??

Mbona mimi huwa sijitbulishi hivyo.....
 
Naomba niwapatie ukweli ninaoujua kwa kutafiti na kufuatilia kuhusu uwepo wa Wakurya wengi jeshini na madai kwamba Nyerere aliwapeleka jeshini

Kwanza niseme hivi, ni kweli kwamba Wakurya ni wengi sana jeshini kulinganisha na makabila mengine ya Tanzania ingawa katika miaka ya karibuni wamekuwa wakipungua kutokana na sababu nyingi ambazo hapa si mjadala wake.

NANI ALIWAINGIZA JESHINI

1. Wakurya waliingizwa jeshini kwa mara ya kwanza na Waingereza wakati wa kuandaa jeshi la kikoloni ambapo ilipotokea vita ya pili ya dunia, Waingereza walikwenda vijijini kwa Wakurya na kuwakamata ama kuwahamasisha vijana wao waingie jeshini ili kwenda kupigana. Baadhi yao waliporejea walikataa kuingia jeshini wakisema wana mali nyingi na wakaenda kuangalia ng'ombe zao. Hawa walipigania nchini Burma huko Asia. Utamaduni huu wa kuingia jeshini ukaanzia hapo na kuendelea.

2. Kwa nini Waingereza waliwachukua Wakurya wengi kwenda jeshini? Ni kwa sababu ya dhana kwamba makabila ya Waafrika yana vipaji tofauti na kwamba ili kuwatawala Waafrika kwa urahisi, inabidi kuvitumia vipaji hivyo. Mfano, Waingereza walisema kwamba ukitaka madaktari wengi watiifu na wapole wachukue Wasukuma kwa sababu ya upole wao na utiifu na kweli tunao wengi sana. Waingereza wakasema tena, wafanyakazi wazuri wa ndani ni Wanyasa - kweli, wafanyakazi wa ndani wa balozi na maofisa ubalozi wa Uingereza hata sasa hivi ni Wanyasa kwa sababu ya uaminifu wao. Walisema pia kwenye elimu weka Wachaga na Wahaya na ni kweli hadi leo waliobobea shuleni zaidi nchini na nani? Tunajua wote! Wakasema, kule Kenya, ukitaka wasomi chukua Wajaluo na Uganda wakasema ukitaka wasomi chukua Waganda. Kwenye uaskari walisema kwamba kwa Uganda chukua Walango, Waacholi na ikibidi sana Wakakwa (kabila la Idi Amin). Nchini Kenya walisema kwamba kwa askari bora uchukue Wakamba. Kwa Tanganyika wakasema chukua Wakurya na ongeza Wangoni na Wahehe. Wakaongeza zaidi na zaidi kwenye mpangilio wao. Ipo orodha ndefu. Waingereza walifanya utafiti mzuri na walipoondoka walimwachia kila kiongozi wa Afrika (makolonini) matokeo ya utafiti wao ingawa akina Nyerere hawakuzifuata.

MATOKEO YA SERA YA WAINGEREZA

3. Nini matokeo ya mpangilio huu wa Waingereza? Kule Uganda karibu wanajeshi wote wakati Amin anaichukua nchi (walikuwa 8,000 hivi), walikuwa Walango, Waacholi na Wakakwa lakini kwa kuhofia kupinduliwa akaanza kuwaua Waacholi na Walango na kuwajaza Wakakwa na baadaye akawaweka mpaka Wazaire na Wanubi wa Sudan kusini na kaskazini mwa Uganda. Kule Kenya hadi kesho, majeshi ya Kenya yamejaa Wakamba na kwa mnaofuatilia mtamkumbuka Jenerali Muringe. Kwa kuwa Wakikuyu wamekuwa wakishika dola, Wakamba waliminywa kwenye vyeo vya chini lakini wamejaa majeshini Kenya kupita kiasi, hasa kutokana na umaskini wa nchi yao ya Ukambani ambayo ni kame pia.

NYERERE KUUNDA JWTZ 1964

4. Kwa Tanganyika Wakurya walijaa jeshini mno wakati tunapata uhuru kiasi kwamba Nyerere akasema hili ni tatizo. Alipovunja Kings African Rifles na kuunda JWTZ baada ya maasi ya 1964, Nyerere aliamua kuweka sera kimya kimya kwamba jeshi hili litakuwa na watu wa makabila yote. Ilikuwa kazi ngumu kwake kwa kuwa waliokuwa wanakuja kujiandikisha kwa wingi walikuwa ni Wakurya zaidi kutokana na utamaduni wa kawaida wa Wakurya wa kupenda kupigana, vita, ukakamavu, umwamba, n.k. Wakurya, kama Wakamba, Waacholi, Walango, na Wakakwa waliitwa na Waingereza "Marshal Tribes" - yaani makabila ya wapiganaji. Hata hivyo, Nyerere alifanikiwa kuwapunguza mno lakini bado alibakia nao wengi kutokana na utamaduni, historia na ukweli wa mambo, kwamba ukitaka askari mzuri chukua anayependa vita, siyo mtu mwoga. Kama si Nyerere, jeshi lingekuwa wakurya watupu, siyo wakurya wengi, bali wao wenyewe kwa hata 90%.

WAKURYA NA NYERERE

5. Wakurya hawakuwa na urafiki wowote na Nyerere kama watu wanavyodhani kutokana na fikra za Kiafrika kwamba kila kitu kina nguvu za siri nyuma yake, iwe baraka za Mungu, rushwa, udini, mapenzi, ukabila, uchawi, fitna, mkosi, n.k. Mwafrika haamini kwamba kitu kinaweza kutokea kwa sababu zake chenyewe bali mpaka kuwe na mtu mwingine anayekifanya kitokee. Kati ya watu waliotaka kumpindua Nyerere kwenye miaka ya 1960 mwishoni, kwa mnaofuatilia, walikuwepo akina Chacha (nahifadhi jina lake kamili), na kutokana na tabia ya Wakurya kumtukana Nyerere alipokwenda ziarani Tarime, aliamua kuacha kufanya ziara huko. Si hivyo tu, Nyerere alikwepa hata kuwapa nafasi za juu Wakurya na mkurya pekee aliyewahi kushika uwaziri katika miaka 25 ya Nyerere ni Bhoke Munanka ambaye walikorofishana hata hivyo (waziri pekee aliyemwambia kwamba huu ujamaa wako utaumiza watu na hakuna anayeutaka). Kama mjuavyo, Munanka alikuwa mfanyabiashara mkubwa katikati ya ujamaa.

6. Aidha, Rais Nyerere hakuwahi kumteua mkurya kuwa mkuu wa majeshi wala msaidizi wala chochote cha juu ingawa ukiongea na watu wanakwambia mambo mengine kabisa. Mkuu wa kwanza wa JWTZ alikuwa Sarakikya kutoka Meru; akaja Twalipo kutoka Songea; akaja Musuguli kutoka Bunda (si mkurya). Rais Mwinyi ndiye aliyekuwa wa kwanza kumteua mkurya kuwa Mkuu wa Majeshi, Jenerali Kyaro, na baadaye Mkapa akamteua Jenerali Waitara. Hata kwenye Vita ya Uganda, Nyerere hakumpa mkurya kuongoza vita ile ingawa kwenye makamanda wa chini Wakurya walijazana kama utitiri, achilia mbali askari wa kawaida. Ni Mwita Marwa pekee ndiye aliyekuwa kwenye makamanda wa kuongoza brigedia, lakini wengine wote walibanwa pembeni........Nyerere hakutaka taabu baadaye.

WAKURYA KUPENDA VITA/JESHI

7. Kwa wenye kumbukumbu na wanaofuatilia, tulipovamiwa na Amin Oktoba 31, 1978, na baadaye Nyerere kutangaza vita, serikali ilitoa mwito kwa wananchi kujiunga na mgambo/jeshi kwa hiari. Nafasi zilikuwa 2,000 kwa kila mkoa. Wakurya walilaani kitendo hicho cha kuweka ukomo wa idadi na wakatuma wajumbe kwenda kulalamika kwa Nyerere kwamba idadi ya 2,000 ni ndogo mno kwa mkoa wa mashujaa. Nyerere akasema hawezi kuondoa ukomo huo. Wakatuma tena ujumbe wa pili, na Nyerere akashauriwa na makamanda wake kwamba kwa kuwa mikoa mingine imeshindwa hata kufikisha 500 tu, basi ni heri Wakurya waachiwe waje tu. Nyerere akasema kwamba basi anaruhusu nafasi 4,000 kwa mkoa wa Mara. Hii imeandikwa kwenye vitabu na waandishi wasiokuwa Watanzania.

8. Wazee wa mkoa wa Mara walikerwa mno na uamuzi wa Nyerere wa kuweka ukomo mwingine wa 4,000 na wakaamua kwamba dawa ni rahisi sana, kwamba vijana wao waende kwenye mikoa ambayo ilikuwa imeshindwa kufikisha idadi ya 2,000 ya awali. Huu si utani. Kaka yangu alikwenda Morogoro. Baba yangu mkubwa alikwenda Moshi na ndugu yangu mwingine alikwenda Usukumani na wote wakaenda vitani na wakarejea kwa ushindi na furaha. Wote wapo hai hadi leo na kaka yangu huyu aliingia Magereza baadaye. Kwa kifupi, Nyerere aliwabana Wakurya wasiende vitani kwa wingi kama walivyotaka. Mjomba wangu Nyaronyo Kicheere alipata medani ya vita pia kwa kujitolea kwenda vitani akitokea JKT - yumo humu ukumbini muulizeni.

KWA NINI WAKIMBILIE JESHINI

9.Nyerere ametoka kwenye urais mwaka 1985 lakini miaka 32 baadaye bado Wakurya wamejaa jeshini ingawa wananyanyaswa kutokana na maneno ya kipuuzi kama haya, je, Nyerere anahusika vipi na kuwepo kwao? Mkurya wa miaka 20 leo, aliyeko jeshini, anahusika vipi na Nyerere? Kwa ufupi ni hivi ........... Wakurya wanalipenda jeshi, basi! Nenda hata Kenya utawakuta jeshini, mpaka hapa Marekani wamo jeshini. Je, Nyerere aliitawala Kenya na Marekani?

10. Pili, kutokana na maendeleo kuwa nyuma sana mkoani Mara, sehemu pekee ya ajira ilikuwa jeshini kwa miaka mingi hadi walipoanza kuchimba dhahabu kwa wingi kule Nyamongo, na kuuza ng'ombe kwa magendo nchini Kenya. Wilaya ya Tarime, wakati ule wa Nyerere, ilikuwa kama sehemu ya Kenya kwani magharibi ilizibwa na Ziwa Viktoria, kusini na mbuga ya Serengeti, na kuja Mwanza kulikuwa na mto usiokuwa na daraja (Mwinyi alilijenga baadaye), kule mashariki na kaskazini ilikuwa nchi ya Kenya. Nyerere hakutaka hata kufanya ziara tu, achilia mbali kujenga walau shule moja. Hivyo, jeshi likawa kama kimbilio la ajira lakini hii ikiwa ni baada ya kuangalia kwanza hulka na silka ya Wakurya kwenye masuala ya kupigana/jeshi/ushujaa, n.k.

Ushahidi uliopo ni kwamba Nyerere hakuelewana na Wakurya hata mara moja na aliwabana wasiingie jeshini lakini akafika mahali akashindwa. Ushahidi ni wa kutosha na mkitaka nitawapa kwenye barua pepe zenu binafsi kwa kuwa hapa si vema kuyataja majina ya watu bila vibali vyao.

Wakurya wana vitu vitano wanavyovipenda sana: Kupigana, familia, ng'ombe, ukweli na utaifa. Ni fahari kubwa kwa mkurya kuingia jeshini, fahari kubwa mno.

Jeshi liko damuni kwa Wakurya!
Naomba kutofautiana na wewe! Historia ya recruitment jeshini ilianza mara baada ya Tanganyika kuwa chini ya utawala wa waingereza. Kwa wanaojua historia ya waingereza walivyo wako "very tradtional". Wanaamini kabisa kuwa asili ya mtu ndiyo hatima yake kimaisha. Yaani kama wewe asili ya ukoo wako ni wakulima hakuna jinsi unavyoweza ukaepuka kuwa mkulima siku za usoni.
Kwa hiyo katika miaka ya mwanzo ya ukoloni wa Uingereza yalifanyika maandalizi ya kuandaa askari ambao wataingizwa kwenye Jeshi la KAR. Waingereza walifanya utafiti kwa misingi hii kwamba ni makabila gani katika historia ya Tanganyika ambayo hayakuingiliwa kirahisi na watu weupe. Kwenye utafiti huo Wakurya au watu wa mkoa wa Mara walikuwa either namba 1 au namba mbili na wahehe sina kumbukumbu sahihi hapo.
Recruitment officer alikuwa anatoka Uingereza na kazi yake ilikuwa ni moja tu : kutafuta askari material wa KAR. Kwenye "brief" alikuwa anapewa mikoa gani anatakiwa achague na mikoa gani apite tu kama hana habari. Mikoa kama ya Pwani aliambiwa apitilize tu. Aende Mara, Iringa, Songea na kidogo Tabora. KAR imeanza na askari wengi kutoka mikoa hii. The last recruitment officer nakumbuka alikuwa anaitwa Major Callaghan miaka ya 60. Utaratibu huu ulisitishwa na Nyerere ambaye aliruhusu makabila yote kuingia TPDF na ndiyo mpaka leo utaratibu ni huo.
 
Back
Top Bottom