Nani hasa aliwaingiza Wakurya wengi Jeshini?

Nani hasa aliwaingiza Wakurya wengi Jeshini?

Kuna member mmoja amenifuata inbox kutaka kujua asili ya wakurya...sasa nimeamua kuitoa kiasi kwa jinsi nilivyosoma maandiko tofauti tofauti huko nyuma anaweza kuja huku na kuisoma pia.

HISTORIA YA WAKURYA NA ASILI YAO

Asili ya Wakurya ni Misri, walifika Congo kati ya 322. KK
Hapo zamani kulikuwa na mtu aliyeitwa monto, huyu ni mzazi wa wabantu wote.

Monto alizaa Range miongoni mwa wanae, Range alizaa Magaiwa, Magaiwa alizaa, alimzaa Mkurya.

Mkurya alizaa watoto watano ambao ni Nyanchage, Wangwe, Mongoso, Nano na Mendi.

Nyanchage aliwazaa Mtimbaru, Mosi, na Mosonga hawa ndio tunawaita inchage.

Wangwe aliwazaa Moracha, Mwirege, Keroba, Mugumbe na Gisiri. Hawa ndio tunaowaita Engwe, kemoramba yagesaka.

Watu walivyozidi kuongezeka ukoo wa Gisiri ulikimbilia umasaini nao huitwa Osiri hadi leo huko umasaini.

Kutokana na kosa alilolifanya Gisiri, (ni stori ndefu), ukoo wa Moracha ulibadili jina ukaitwa abanyamongo (wenye maghala ya chakula)
Ukoo wa Mugumbe ulibadili jina ukaitwa abalenchoka (wala nyoka, waliishi mlima wa nyoka).

Mongoso alimzaa Mkira, mtoto pekee. Huyu ndo mzazi wa abakira na maana ya MongoMongoso leo ni tembo dume.

Nano aliwazaa Mokenye, Musweta na Msimbete. Hawa ndio waitwao inano yaani nyani.
Kutokana na hawa waliibuka watu mbalimbali kama abakine, abarieri, abamera, abanyanccha na abangoreme.

Mendi alizaa mtoto mmoja tu Munchari, hawa hujiitia emendi yaani panya mdogo au irigeki.


KUHUSU MAJINA


Wakurya wana majina sita ya wazaliwa wa kwanza. Matatu ya kiume na matatu ya kike.

Naanza na ya kiume Mwita, Marwa na Chacha. Nitamaliza na ya kike Ghati, Bhoke na Rhobi

Mwita asili yake ni uguita, yaani kuua/Kifo. Wakurya kitu kinachowashinda kupambana nacho huamua kukienzi. Kifo kiliwashinda wakaamua wakienzi kwa kuwapa wazaliwa wa kwanza jina hilo ie to familiarize with that misfortune!!! Ili wakizoeee

Chacha asili yake zimekuja, ni jina walilopewa watoto wa kiume waliozaliwa wakati ng'ombe zimeibwa au zimeletwa toka umasaini au usukumani. Wakurya huamini ng'ombe wote ni wao, hivyo ni kama waliporwa, kwa hiyo vijana walipoenda kuiba ilikuwa sio kuiba ila kuzifuata na kuzileta. Zimekuja/Chacha.

Marwa ni pombe iliyoandaliwa na kunywewa kusherehekea ng'ombe zilizoletwa.

Kwa wanawake,
Bhoke ni asali, kitamu, kitu kilichopatikana bila jasho na kitakacholeta vitamu. Hupewa mtoto wa kike kwa sababu huleta ng'ombe bila jasho, ni baraka kwa familia. Linganisha ng'ombe anazoleta Bhoke na zile za kuiba, zinazopatikana kwa kumwaga hata damu. Kwa hiyo ni asali /Bhoke.

Rhobi hutokana na neno Erhobilo, hii ni shangwe inayofanywa na wanawake na wanaume kufuatia tukio zuri kama kurudisha ng'ombe zilizoibwa. Shangwe hiyo ikifanywa na wanaume pekee huitwa engoliga. Lkn wafata nyayo wanapofika nyumbani nyimbo zao huimbwa na wote, na hapo huitwa Erhobilo, ndo asili ya jina Rhobi

Ghati, hutokana na neno la kimaumbile yaani umbile la mwanamke (uke). Kilichofanya likastaajabiwa ni kuwa mke na mume hulala pamoja, inakuwaje mwanamke abebe ujauzito lkn sio mwanaume? Hivyo Ghati maana yake oghotia au kupasuka. Kwamba wamepasuka ndo maana wanabeba ujauzito. Hili ni jina la kuenzi umbile la wanawake

Ndoa za kimira. Kwa Wakurya.

Nyumba nthobhu, mwanamke aliyezaa watoto wa kike tu, ili atakapokufa baadae nyumba yake isitoweke huamua kuoa binti wa kuendeleza uzao wa nyumba yake

Nyumba mboke ni kama mwanamke hakuzaa kabisa iwe binti wala mvulana, huyu huoa ili apate uzao

Nyumba ntune ni kama kijana alizaliwa kwao na vijana wengine au peke yake, lkn bahati mbaya akafa kabla ya kuoa hasa kama alikuwa amepita umri wa utoto (ubhulisia). Hivyo familia hukaa na kupanga kuoa mke wa kufufua jina la kijana huyo aliyekufa

Nyumba nyana ni aina ya ndoa ambayo mwanaume anayeoa ni taahira au kilema au zezeta. Kwa kuwa jina la mwanaume halipotei ukuryani, basi ndugu wa familia huombwa kuoa na kuzaa watoto lkn watoto ni wa huyo kilema ambaye kwa kawaida anakuwa hawezi majukumu ya kutungisha au kulea

Nyumba nguru, inatokea kama familia haikubahatika kupata mtoto wa kiume mapema, lkn baadae akazaliwa wazazi wakiwa wazee na wamekata tamaa. Huyo mtoto huolewa mwanamke ambaye huja kuzaa kuendeleza uzao wa mtoto. Mtoto huyu akikua huchagua aidha kukubali huyo mke au vinginevyo lkn mwisho wa siku ni familia yake.

Eteto ni aina ya ndoa ya kawaida. Mwanaume anaoa mke wake au mke wa pili (okohareka).

Ikumbukwe Kuwa, awali mwanaume wa kuoa aina ya ndoa hapo juu ni yule aliyechaguliwa kutoka kwenye ukoo au familia ya wahusika.
Mkuu mimi ni mkurya (mwirege ) asante sana tena sana kwa kunifungua ufahamu kuhusu asili yangu. My God bless you, kama una vingine mkuu weka humu wengine hatujakulia ukuryani. So I know a little bit about my home.
 
Mkuu mimi ni mkurya (mwirege ) asante sana tena sana kwa kunifungua ufahamu kuhusu asili yangu. My God bless you, kama una vingine mkuu weka humu wengine hatujakulia ukuryani. So I know a little bit about my home.
Uwe unaenda home mura...

Wasaghane wasikufanye usahau om..

Au ukiona vipi uwe unaenda pande za kitunda kule ni kama uko tarime
 
Uwe unaenda home mura...

Wasaghane wasikufanye usahau om..

Au ukiona vipi uwe unaenda pande za kitunda kule ni kama uko tarime
Hata wewe ni mkurya kama nimesema uongo mwambie mod anipe ban[emoji23]
 
Jeshini kuna hitaji watu jasiri na shupavu, ndo maana wachaga huwaoni huko kwa wingi kwasababu ni walegevu mno.
Yaani kazi za kutumia misuli na mabavu kidogo kama kwenye majeshi, kabumbu nk ndugu zangu wachaga ni kuwatafuta kwa tochi huko,, adimu sana!!!!
 
Sisi wakerewe hayo hayatuhusu kazi yetu ni kuvua miselebende tu.
 
Be specific.....kuna wanajeshi wangapi tz.....orodhesha kila kabisa ndipo naweza angalau kuchangia sababu.....mi nnavojua wasukuma ndo wengi maana 85% ya wanajeshi nliowahi kukutana nao ni was....ukuma
 
Jeshini kuna hitaji watu jasiri na shupavu, ndo maana wachaga huwaoni huko kwa wingi kwasababu ni walegevu mno.
Yaani kazi za kutumia misuli na mabavu kidogo kama kwenye majeshi, kabumbu nk ndugu zangu wachaga ni kuwatafuta kwa tochi huko,, adimu sana!!!!
Vitengo vingi vya fedha na uhasibu pamoja na ugavi ndani ya majeshi vimeshikiliwa na wachaga....usiulize kwanini....madarasa wanayo katika hizo fani
 
Be specific.....kuna wanajeshi wangapi tz.....orodhesha kila kabisa ndipo naweza angalau kuchangia sababu.....mi nnavojua wasukuma ndo wengi maana 85% ya wanajeshi nliowahi kukutana nao ni was....ukuma
Umeeleweka kwa comment yako
 
Vitengo vingi vya fedha na uhasibu pamoja na ugavi ndani ya majeshi vimeshikiliwa na wachaga....usiulize kwanini....madarasa wanayo katika hizo fani
Acha kujitekenya mkuu
 
Uzi umenisisimua!

Inabidi niende nyumbani nikape baraka za wazee mwaka huu!

"SASA UNAINGIA MKOA WA MARA, BE STRONG"
 
Tatigha ,
Mkuu
Duuuuuuh.
Haaa haaaa haaa haaaa teeeh teeeeh teeeh teeeeh teeeh

Niliwahi kusikia kwamba Jenerali Mwita Kyaro alipokuwa akipita na gari yake na kumkuta askari anatembea kwa miguu na nafasi imo garini mwake aliwabeba.Pia nikasikia kuna siku alipelekewa magunia ya sukari akasema "Yote hii ya nini?". Akachukua kilo kadhaa kisha akawaambia: "Hii nyingine pelekea askari!". Hao watu waacheni bwana wako vizuri!
 
Narudia mara ya mwisho hakuna kabila la wakurya, Wakurya ni mkusanyiko wa makabila mbali mbali kutoka mkoa wa Mara na hilo neno wakurya ni region ipo Kenya karibu na boarder ya Tanzania ina itwa Kurya county
we nae ni hewa sana hujui hata kenya kuna kabira la wakurya...Mgumu na Tarime hamna kabila jingine tofaut na wakurya hao wengine ni wa kuja tu...maana kwa sasa wajaruo wanapatikana wilaya ya Rorya..
 
Back
Top Bottom