Mwalimu mgeni aliingia darasani kwa mara ya kwanza na kuchora moyo ubaoni. Kwa vile hakuwa mchoraji mzuri ule moyo ukaonekana ovyo tu.
Kwa kujiamini akauliza wanafunzi nimechora nini?
Mwanafunzi 1.... makalio
Mwanafunzi 2..... umechora makalio mwalimu.
mwanafunzi 3. hayo ni makalio kabisa
Mwalimu kwa hasira akaenda kumuita mkuu wa shule kwa madai ya wanafunzi kufanya mzaha darasani.
Mkuu Wa Shule; kwa nini mnamfanyia mwalimu mzaha?
Wanafunzi; hatujafanya mzaha.
Mkuu wa Shule: Kama hamfanyi mzaha nani kachora makalio ubaoni?