Nani Kadukua Mitandao ya Serikali ya Tanzania? Je, Vitisho vinasaidia?

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
28,132
Reaction score
64,416
Salaam

Tatizo la Polisi wa Tanzania wanaongoza kwa Vitisho wakihisi Wadukuzi wanawaogopa. Sasa watu wamedukua, badala muwekeze kwenye Ulinzi wa kimtandao, nyie mnatisha. Hadi mtu anadukua unadhani anakuogopa?


Lengo la mada ni kutaka kujua kama vitisho vitisho vitasaidia watu wasidukue.

Pili: Kwanini mitandao yote imedukuliwa kwa wakati mmoja? Je, inaendeshwa na mtu mmoja?

Serikali imetunga Sheria ya Faragha.. Je, data zetu zipo salama? Nasubiri tamko la TCRA

Sababu kwenye report yao wameweka Username na Passwords. Sasa faragha yetu ipo wapi?

Kwa mujibu wa ripoti ya TZ-CERT ya tarehe 28 Septemba 2026, Tanzania imekumbwa na kiwango kikubwa cha mashambulizi ya mtandao, ambapo mfumo wa ufuatiliaji wa TZ-CERT ulirekodi mashambulizi 106,858 dhidi ya huduma za mtandao (web attacks).

Mashambulizi hayo yalilenga maeneo mbalimbali ya mifumo ya tovuti za Serikali ikiwemo kurasa za kuingia kwenye mifumo na mafaili yenye taarifa nyeti.
 
Mtandao kama upi umeliwa kichwa? Watu wa security cyber wamelala mno, mwezi uliopita jamaa walikula kichwa mitandao yote, sasa wamerudia tena?
 
We jamaa kwanini siku hizi humalizii vitu vyako kwa MIA???
 
Hivi unaanzaje kumtishia mwizi ambaye ameshakuibia tayari. Kuna mambo yamepitwa na wakati.
 
wamekalia na hadaa za akina dudu baya za you bela watch your back wakizani watu wataondolewa kwenye mjadala wa mauwaji ya oc29
 
Jeshi la Polisi kanda malaamu ya Dar es salaam linapenda kukanusha taarifa za uongo zinazosambazwa na watu wenye nia ovu. Jeshi la polisi halitasita kumchukulia hatua mtu yeyote.

Mwisho wa kunukuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…