Naomba kuchangia mada.
Tangu jana usiku nimeona picha na nimesoma post mbalimbali ambazo kwa kiasi kikubwa zilikua zinaonyesha kwamba tamasha la Jide lilifana kuliko la MwanaFA. Sababu kubwa za tamasha la jide kufana inaonyesha ni idadi ya watu waliohudhuria na burudani.
Kwa upande wa Binamu, waliohudhuria walikua wachache na show ilipooza! Ni vigezo vipi unavyoangalia kumpa ushindi Binamu??
Hao mashabiki wastaarabu aliwachagua au walienda wenyewe? Kwa uelewa wangu wa muziki, hata uwe na masheikh na mapadri ukumbini, mziki ukiwa mzuri watakupa heshima yako kwa kuimba na wewe, kucheza, kukutuza au kupiga kelele ili mradi kuonyesha wanakuunga mkono.
Kama mashabiki wako watakaa kwenye viti mwanzo mpaka mwisho wa shoo, basi umeshindwa kuwapa kile walichokitegemea kwako, maana yake umefanya vibaya!
Unafkiri ni kweli mashabiki wa Binam walikua wastaarabu au ni kupooza kwa show ndo kuliwafanya wapooze?
Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
Aaaaaaah aaah wamepeta joto hasiraaaa.....