Nani Kapata kama hii

Zanta

JF-Expert Member
Joined
Apr 4, 2011
Posts
2,028
Reaction score
796
Wandugu nimepokea msg kwenye simu inasema hivi

"Habari, Ofisi ya (Diamite Inter Company) inapenda kukupa nafasi ya kipekee, Endapo utapendelea kutumia muda wako wa Ziada kuweza kujiongezea kipato. ama ndio tafadhali tumia number hii 0719152760. ili kupata maelezo kufika ofisini. Eva""

Sasa nani anawajua hawa jamaa kabla sijatumia kadola kangu kuwapigia? Isije kua ndio wale wa bidhaa za kuzungusha maofisini? Mwenye kuwajua atoe details hapa
 
Usipoteze muda wako kwenda, mara nyingi kama hizo huwa wanajishughulisha na uuzaji wa bidhaa hasa kichina (unapewa bidhaa muda ambao upo free unaziuza) ...Kuna jamaa yng alitumiwa txt kama hy kwenda kufatilia ndo akakuta mambo hayo.
 
Usipoteze muda wako, hao ni watu wa network marketing. Hawana lolote la maana zaidi ya kukupotezea muda wako.
 
Ndio wale wale...tianshi,forever,gnld nk....usipoteze muda
 
hao ndo wale wanaotoa semina za kutengeneza sabuni, mishumaa na mavitu kibao but unalipia like elfu kumi na tano baada ya hapo wanakwambia wao wanauza malighafi ya hivo vitu but wewe ununue utengeneze na utafute soko mwnyewe...partly ni nzuri kama unaweza kutafuta soko but tatizo wanafundisha juujuu tu
 
Waliwahi kunitumia SMS kama hiyo..kabla sijaenda nikawauliza kazi inahusisha kitu gani haswa..walikataa kbs kunitajia eti mpaka niende ofisini kwako.. Nikatupa kuleee..
 
....kwa kuongezea kuna ada ya kujiunga yaani utatakiwa kulipia pesa mara nyingi huwwa ni laki mooja na nusu kabla ya kupewa hizo bidhaa uziuze kama machinga.
 
Kumbe wasanii. Thanx all
 
hiyo ni GNLD kirefu chake hiyo D ya mwisho ndio Diamite International.
 
waongo wale we nenda ukajionee,watu walitoka sgd mpaka dar
 
Usipoteze muda wako kwenda, mara nyingi kama hizo huwa wanajishughulisha na uuzaji wa bidhaa hasa kichina (unapewa bidhaa muda ambao upo free unaziuza) ...Kuna jamaa yng alitumiwa txt kama hy kwenda kufatilia ndo akakuta mambo hayo.

Hivi wanapata wapi ruhusa ya kutuma matangazo kwenye simu zetu bila ridhaa zetu?
 
Waliwahi kunitumia SMS kama hiyo..kabla sijaenda nikawauliza kazi inahusisha kitu gani haswa..walikataa kbs kunitajia eti mpaka niende ofisini kwako.. Nikatupa kuleee..
Hahahaaha, wanaudhiii. Mie nilitumiwa SMS na my closest friend 'darling, there is something very important I think you should know. Plz njoo new Africa hotel as soon as you can and it has to be today' nikapanick, namuambia hatuwezi kuongea kwa simu? Anasema hapana. Acha nikimbie, na nilikuwa Kama 10 ams away. Nafika nakuta utumbo wa bio disk. Hata sikusikiliza, nikachukua kadi Yao nikaahidi kuwapigia. Kugoogle sijui kipendant ukivaa unakuwa na akili za ziada, nikafyonzaa nikasahau
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…