Nani karuhusu uharibifu wa misitu kwa hawa wafugaji

Nani karuhusu uharibifu wa misitu kwa hawa wafugaji

ndomyana

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2012
Posts
5,630
Reaction score
2,169
Huku Katavi pori la Hifadhi ya Katavi. Kuna hawa wasukuma wanafuga na kulima.

Ukianzia sitalike Kwenda kibaoni majimoto wamevamia katikati ya Mapori wamejenga na kukata miti kuandaa shamba. Upande wa kizi kuja mpaka lyamba nako wamevamia mapori misitu na kukata miti na kuanzisha mashamba.

Inasikitisha kuona wanaangaliwa tu je kwa hali hii tunalilia mvua kila siku ila tunaharibu. Misitu. Inamaana hawa watu wamekosa maeneo ya kufunga na kulima mpaka waaribu mapori yetu urithi wa wanetu. Nani kawaruhusu hawa watu waharibifu. Au wanataka na hii mikoa iwe jangwa kama kwao shinyanga.

Tunawapenda wafugaji na wakulima ila kwa huu uharibifu hapana. Serikari iliangalie hili lasivyo Katavi itakua jangwa hivi karibuni.
 
SHAMBA LA BIBI MKUU KILA MMOJA HIVI SASA ANAJIAMULIA KUFANYA ATAKAVYO
 
Back
Top Bottom