Mengi Ayoub
Member
- Apr 20, 2022
- 56
- 46
Habari zenu wakuu?
Bila shaka mu wazima wa afya... Leo hembu tukae tujadili hili , je ni nani yupo nyuma ya Haji Manara? Mara zote amekuwa akirudia jambo lile lile la kuzarau mamlaka husika.
Tuliona wakati ule anatoka Simba sc alitoa siri na maneno kadhaa yenye kuuzi kwa CEO na Rais wa heshima wa club hiyo ya Simba , lakini hao wote walikaa kimya.
Tukaona juzi amefungiwa kujihusisha na soka lakini hakuridhika akaita Press nakuongea mambo ambayo kimsingi nafkiri ni shutuma ambazo hazikupaswa kuwekwa wazi .
Chakujiuliza , je kuna mtu anaemtuma ili achafue watu fulani? Au kuna club ambayo iko nyuma yake inamtuma ili kuteka attention za watu?
Na je kuna ulazima wa kuelezea siri na mambo uliyofanyaga na mtu fulani enzi hizo mkiwa sawa lakini mnapohitilafiana basi uyaweke wazi?
Naomba kuwasilisha wakuu 🙏