Wanajua wanafanya nini, Kuna kitu kinaitwa mapenzi na hao wananchi bado wana mapenzi na mbunge wao. Sasa unapowahukumu kuwa hawajui chochote ni kufanya waendelee kuwa na mapenzi zaidi na mbunge wao.
wananchi wa kijijini wakimpigia makofi chenge jana.hawa ndio ambao hawajui tulipo na wanatutegemea sana sisi kuwaleza wapi tulipo na tunaelekea wapi
Jambo ambalo naweza kusema,Hawa wananchi wana mapenzi na chama chao na sio mapenzi na Bwana Chenge.Wanajua wanafanya nini, Kuna kitu kinaitwa mapenzi na hao wananchi bado wana mapenzi na mbunge wao. Sasa unapowahukumu kuwa hawajui chochote ni kufanya waendelee kuwa na mapenzi zaidi na mbunge wao.
Hakuna mtz ambae hajui nini maana ya ufisadi... Iwapo Bosi wake angemtimua kazi ya uwaziri kabla ya yeye kutamka kuwa anajiuzuru, na kuwepo kwa mapokezi ya namna hiyo kidogo kauli yako ingekuwa na nafasi. Lakini kwa sasa umeamua kuhukumu tu kwa utashi wako binafsi.
Jamco,Jamani ndo hali halisi, watu wamelala njaa lakini wanaamka asubuhi wanakuja kushangilia mzee wa vijisenti kwa kuwa yeye ni CCM na wamemwambia lazima aende. Kazi kubwa bado hipo ya kuwalimisha wananchi wa kawaida umuhimu wa kuachana na ushabiki wa kisiasa ambao CCM inacapitalize hapo.
Mimi nakwambia hata balali akirudi leo akagombea uraisi kupitia CCM watu watampa kura.
Kamanda Gembe:
Katika risala yao wamesema bayana kuwa wanapinga kauli ya Umoja wa Vijana(CCM) Tanga kwa kuwataka wale wote waliotuhumiwa na ufisadi wajiuzuru katika nafasi zao za ubunge. Hili unalichukulia vipi na aina ya mapokezi hayo?
Uoni kuwa kuwa tatizo katika kutekeleza majukumu kwa kiongozi wa juu kabisa ambae uteua mawaziri wake kukaa kimya kwa wamaziri hao kiasi cha kuwapa nafasi ya kujiuzuru na baade kwenda kujinadi upya kwa wapiga kura wao kuwa wamechukua hatua hizo kwa manufaa ya umma ilhali ni watuhumiwa?
Wananchi na hasa wanaoshiriki kwenye kupiga kura, mara nyingi wanaongozwa na mapenzi binafsi ya mgombea wao. Jinsi anavyojieleza na jinsi anavyoweza kutatua matatizo yao. Na Iwapo inatokea huyo walie mchagua kukumbwa na matatizo na akajiwahi kujitetea mbele yao mapenzi kwake uongezeka licha ya maneno ya chinichini kuwa wanakuwa mameandaliwa kufanya hivyo.
Kama kutojua kinachoendelea ni vema lawama hizo zikaelekezwa kwa bosi wake mkuu kwa kumpa nafasi ya kujiuzuru badala ya kumtimua kazi. Sidhani kama JK angetamka kuwa amemfukuza kazi kungekuwepo na mapokezi ya namna hiyo.
Kibunango,
1.Jk ni mtu mmoja wa ajabu sana kwa maoni yangu sababu ameshindwa kuyatolea majibu maswali magumu,watawala na wasaidizi wenzake wanamuita na kusema ni Mvumilivu,Ansbert ngurumo anasema ukitaka kumjua mtu angalia rafiki zake,atakuwa anafanana nao,Mie naungana na Ngurumo katika Hili,yeye ni kama wao ndio maana ina mchukua muda yeye kuwachukulia hatua sababu ni rafiki zake.Tabia ya Unafiki.
2.UVCCM na CCM ya mkoa wa Tanga ndiyo CCM ile ambayo iliachwa na Mwalimu,CCM ambayo ina fuata misingi ya Utu na ndio maana kila siku huwa wanampinga makamba katika mambo mengi,wanataka haki kwa ajili ya wafanyakazi na walimu.kwa maana nyingine hawataki CCM ya wafanya Biashara.wamejaribu kuwalazimisha wajiunge nao ila wameshindwa na kama unakumbuka ndio maana niliwahi kushinikiza makamba ajiuzuru. watu wakamtetea,ila hawa watu wa mfano wa makamba ndiyo wanawakumbatia hawa wala rushwa na Mafisadi.Kumbuka ni nani alimtetea Lowassa sisulubiwe mbele ya JK??
Omulangi,Wana JF naona kama seriousness inaanza kuwepo. Tunapohama toka katika kulalamika na kupanga mikakati. Tena kugundua lile ambalo mafisadi walilifahamu zamani na ku take advantage. Ukweli ni kuwa watanzania wa kawaida kijijini hawaelewi yote haya yanayoendelea maana yake nini na tafsiri yake kwa maisha yao ni ipi? Kulaumu wanavyopewa bia na khanga wakanunuliwa katika uchaguzi ni kuwaonea. Hawajui tafsiri yake kwenye maisha yao ya kila siku ni ipi. Hawajui kuwa kuna athari yoyote kwao. Wanadhani wamemkomoa mhesh. Mgombea. Na mbaya zaidi nguvu ya watu wa vijijini maskini wameiwekeza kwa vijana wao wakawasomesha baadhi yao nao wanapofanikiwa hawakumbuki lolote la kuwasaidia wazee na jamii zilizojitoa mhanga kuwatafutia elimu. Wasomi wetu wako wako Ulaya na Marekani wanakula kuku wakati waliohangaika kuwatafutia ulaji huu wamesahaulika. Ndiyo MH Gembe kampeni irudi kjijijini kuwaelimisha maana ya demokrasia ya vyama vingi ni nini. Vuguvugu lirudi huko kueleza kuwa wao ndio wenye nchi na sio watawala. Mfumo wa kichifu waliozoea uliwaweka wananchi kuwa mali ya watawala na raslimali zote zilikuwa za mfalme. Akifurahi anawagawia raia wake. Wananchi wengi wanadhani mfumo huu bado unaendelea...
Obe,Nani katuloga!
Sisi hatujalogwa ila ni wapuuzi na hasa ambao tuna macho tumekuwa wapuuzi sana. Mpuuzi hapa sio tusi ila ni namna mtu anavyoacha kufanya kitu cha maana na kuammua kufanya kile ambacho hakina maana
Ni kweli kabisa tunashabikia mambo ya kipuuzi na tukipewa kidogo tunakula na kulala bila kutambua kuwa tukiamka tumbo litadai halali yake.
Elimu iongezwa ndiyo jibu sahihi na hii itolewe na Mwalimu Mkuu
Tumerogwa, dawa zikiisha muda wake tutarudia fikara zetu