Nani kuchukua ndoo ya La Liga 2021?

Nani kuchukua ndoo ya La Liga 2021?

BJB FC

JF-Expert Member
Joined
Aug 25, 2015
Posts
2,064
Reaction score
2,312
Habari wakuu, wapenda soka, hususan li kule kwa kina Berlin (Andrés de Fonollosa).

Moto unaendelea kuwaka huko Spain. Mminyano wa hali ya juu kati ya timu nne za juu, Atletico Madrid, Real Madrid, Barcelona na Sevilla.

Wakati mashabiki wa Barca, wakitegemea kuwa kileleni kwa mara ya kwanza tangu msimu uanze, Granada wanapindua meza, na kutoka na point zote 3 ndani ya Camp Nou.

Real Madrid naye akitoa sare mechi zake mbili za mwisho, huku Cholo akila kichapo kutoka kwa Bilbao.

Sevilla, akiwa hatajwi sana, katika nyuzi pendwa humu za Barca na Madrid, amejikusanyia points zake 70 huku ametulia tulii kama hayupo vile.

Hapa tutapeana updates za mechi zilizobaki mpaka bimgwa apatikane. Kiunazi, karata yangu kwa Real Madrid, Moyoni Atletico Anachukua Ndoo.

Mechi tano zimebaki kwa kila mmoja, wakati msimamo ukiwa hivi [30.04.2021].

Screenshot_2021-04-30 Barcelona (Sky Sports).png
Screenshot_2021-04-30 Atletico Madrid (Sky Sports).png
Screenshot_2021-04-30 Real Madrid (Sky Sports).png
Screenshot_2021-04-30 Sevilla (Sky Sports).png
Screenshot_2021-04-30 LaLiga on Instagram “🍿 #LaLigaSantander 🍿 atleticodemadrid are still on ...png
 
Binafsi mimi ni mpenz wa atletico na ninatamani kuona el cholo anabeba ndoo hii kwa mara nyingine..

Tatizo atletico wamekuwa na homa ya vipindi hapa kati na kama pumzi zimewakatikia vile.. Game ya barca kwao itawapa muelekeo wa kubeba ndoo au lah! Huku wakiomba barca na madrid wapoteze point ktk game zao ngumu.

Barca ana game mbili za kumuamulia ubingwa game na valencia na ile ya atletico akikusanya pointi 6 humu atakuwa kawasha turbo.

Madrid naona ana game kadhaa ngumu naona ana sevill, bilbao na villareal.. Hizi ni timu ambazo zinaweza kumpa madrid presha, japo katika hizi 2 yupo nyumbani.. Akipata pointi 9 humu kwa asilimia kubwa anaenda kuchukua ndoo.

Sevilla siwapi saana nafasi ana game 4 mfululizo ngumu, anapiga na bilbao, kisha madrid, kisha valencia, kisha villareal, itakuwa ni maajabu ya dunia akipata pointi 12 humu.
 
Kwakasi walioanza nayo wananchi leo! Hakika wanachukua ndoo, nyuma mwiko mbele milele.
 
Atletico Hawezi kubeba hilo kombe ,Ingekuwa wakubeba angesha tangazwa hadi sasa, walikuwa wakiongoza kwa utofauti wa point zaidi ya 14 ujinga ujinga umewafikisha hapo nadhan target yao ni big 4 na sio kombe
 
Naona Messi amekubali kurekebishiwa kupunguziwa dau lake nono analolamba pale Barcelona ili ikusanywe pesa ya kumnunua Håland wa Dortmund..

Wakati huohuo man city wamepanga kumpiga bei Raheem Starling ili kukusanya pesa ya kumnunua Håland....

Håland [emoji91]
 
Ligi ya mwaka huu tamu sana kimasihara madrid anabeba kauli mbiu ya mwenye nacho huongezewa

Huko ufaransa lille na paris moto unawaka. Hapa napo mwenye nacho huongezewa

Italy inter [emoji817] nasikitika na gundu linalowaandama milan wapo nje ya top sasa hivi na inaelekea wanamaliza nje ya top 4 kimaajabu
 
Naona Messi amekubali kurekebishiwa kupunguziwa dau lake nono analolamba pale Barcelona ili ikusanywe pesa ya kumnunua Håland wa Dortmund..

Wakati huohuo man city wamepanga kumpiga bei Raheem Starling ili kukusanya pesa ya kumnunua Håland....

Håland [emoji91]
Halafu huyu haland kila nikimtizama naona kuna muda upepo wae utakata.. Kuna timu itajuta kumchukua..

Aende timu ambayo inatengeneza nafasi za kutosha, kwakuwa anajua kujiposition na analijua goli, ataendelea kufunga mpaka dunia inaisha

Ila akienda timu tia maji, macho kwake, atapata tabu.
 
Ligi ya mwaka huu tamu sana kimasihara madrid anabeba kauli mbiu ya mwenye nacho huongezewa

Huko ufaransa lille na paris moto unawaka. Hapa napo mwenye nacho huongezewa

Italy inter [emoji817] nasikitika na gundu linalowaandama milan wapo nje ya top sasa hivi na inaelekea wanamaliza nje ya top 4 kimaajabu
AC Milan wamezingua sana.
 
Back
Top Bottom