Nani kuondoka na kiatu cha ufungaji bora NBCPL;Aziz KI au Feisal

Nani kuondoka na kiatu cha ufungaji bora NBCPL;Aziz KI au Feisal

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Wachezaji hao ndio vinara wa magoli kwenye NBC Premier League ambapo mpaka sasa wamefunga magoli 15 kila mmoja na hadi sasa timu zote zimesaliwa na michezo 3 pekee kutamatika kwa ligi kuu msimu huu

Msimu uliopita hadi ligi inatamatika wachezaji wawili wa Yanga na Simba ambapo ni Fistoni Mayele aliyefunga magoli 17 sawa na Saido Ntibazonkiza naye alifunga magoli 17,ila kwenye usiku wa tuzo za ligi wote walipata kiatu cha ufungaji bora

Ila kwa msimu huu ni Feisal Salum wa Azam Fc na Aziz Ki wa Yanga

Hadi sasa Mabingwa ni Yanga ambaye ameutetea Ubingwa wake kwa mara 3 mfululizo hapo msimu huu kikosi hicho kikiwa chini ya kocha Gamond
Screenshot 2024-05-16 150116.png
 
Fei Toto ni mpambanaji. Hongera kwake. Akichukua itapendeza, Aziz K pia anastahili, akichukua ni sawa.
 
Mwenye magoli machache ya Penalti ndo ataondoka na kiatu
 
atakayekuwa na goli nyingi ligi itakapomalizika, wakiwa sawa utaratibu umeuelezea kwenye uzi tayari ukitolea mfano msimu uliopita, kwan tff wamebadili kanuni?
 
atakayekuwa na goli nyingi ligi itakapomalizika, wakiwa sawa utaratibu umeuelezea kwenye uzi tayari ukitolea mfano msimu uliopita, kwan tff wamebadili kanuni?
Hizo kanuni huwa zinabadilka kila msimu. Kanuni siyo sheria.
 
ephen_ alisema kiatu apewe feisal Salum.

Inshaaalah mungu Akubariki saana Feisal

Uzalendo
 
Aziz ki sina tatizo nae ila natamani tu kuona kiatu anachukua Feisal...
 
Back
Top Bottom