Elections 2010 Nani kuukwaa uwaziri mkuu?

Status
Not open for further replies.
Kama mnafuatilia utetezi wa CCM kumwengua SITTA walisema kinamama waliomba wapewe fursa aidha ya kutoa Waziri Mkuu au Spika, wakakubaliwa kutoa Spika hivyo nafasi ya Waziri Mkuu haiwezi kwenda kwa mwanamke. Prof. Anna Tibajika yeye atapewa wizara inayosimamia shirika la nyumba la Taifa.
 

Kapwani inawezekana we are expecting the unexpected
 

ze following user says senki you so much for zis usifuli posti...bob giza (today), 16th.nov at 9:48
 

Hivi huko siyo kuvunja katiba ya nchi kweli? Kuna mahali popote inaposema wakina mama wawe na haki ya kutoa maamuzi au madai kama hayo? kama ndivyo kweli ilivyotokea kuchaguliwa huyo Mama, basi sina shaka kuwa katiba ilivunjwa makusudi na kundi la viongozi wetu limekuwa kama darasa la chekechea. Hatukatai mwanamama kuwa Spika lakini watu wagombee na wateuliwe kwa umakini wao kufuatana na umuhimu wa nafasi ile. Sidhani kama ni sawa kutoa nafasi ya uspika kama zawadi. ITS A SHAME!!
 
Habari kutoka Dodoma zinasema kuwa kati ya Tibaijuka na Magufuli mmojawapo atateuliwa kuwa Waziri Mkuu. Awali kulikuwa na candidates watatu mezani kwa Kikwete; akiwemo Mwandosya, ambaye sasa jina lake limeondolewa.
Akitambua bayana kuwa serikali yake haina haiba wala mvuto wa kutosha kuungwa mkono na wananchi, Kikwete amesema anataka waziri Mkuu "kukuru-kakara" atakayeweza kuburuza hybrid policy katika kilimo, viwanda (manufacturing) kwa ajili ya kuleta impact katika ajira. Huu ni mkakati wa ku-mobilize vijana amabo wanaonekana kuitupa mkono CCM, hasa kutokana na uzoefu wa CCm kutoungwa mkono na vijana wengi wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa 2010.
Nwasilisha. Tuendelee kutega masikio yetu.
 

CCM inajumuiya zake mojawapo ni kinamama (UWT) ambapo ndani ya chama chao UWT waliomba kuongoza mmojawapo wa mihimi mitatu, kwa hiyo haya yalikuwa maamuzi ndani ya chama na si ya kiserikali. Sidhani kama Katiba ilivunjwa kwani ni CCM waliamua kumsimamisha mwanamke na hawakulazimisha vyama vingine na vyenyewe vimsimamishe mwanamke ndio maana CHADEMA wao walimsimamisha mwanaume
 

Nakuunga mkono, ongezea na yafuatayo ili kuweka record vizuri na sahihi
(i) Aliadabisha na kufukuza wahandisi wazembe 224 Wizarani
(ii) Alizifuta kampuni hewa za makandarasi zaidi ya 1000
(iii) Alirudisha magari, mitambo na pikipiki zikiwa mali za serikali zaidi ya 21,000 na kuyasajili upya mfano PT,DFP,STK, US n.k zoezi hili liliigwa na Kenya na Uganda
(iv)Alimwadabisha mkandarasi aliyekuwa akijenga barabara ya Dsm-Bagamoyo kwa kutotii mkataba kitu kilichompelekea kufilisika
(v) Aliahidi kusafiri kutoka Mtwara kwa taksi mpaka Bukoba-ndoto imetimia
(iv) Leo hii Wizara ya Mifugo n Uvuvi inaingiza billioni 200 kwa mwaka baada ya wajapani kuingia mkataba wa kuvua samaki bahari ya hindi-Tanzania tofauti na mwanzo iliitwa shamba la bibi
(Vi) Na mengine mengi mtayaongezea

Huu ndio uzalendo tunaoutaka " matumizi mazuri ya hela ya walipa kodi" hakuna ubishi watanzania wameiona kazi yake!
 
hapo akipewa magufuli ndo mawaziri watajua nini maana ya kuwa waziri...yaani huyo hana longolongo ni kunyosha mstari
 

Lisemwalo lipo kama halipo basi laja, ila kwa serikali ya mkwere unaweza ukaletewa mtu hadi ukachoka mwenyewe
 

Hii imekaa vema kwa nchi zinazoendelea ambako uadilifu na uwezo wa mtu unathaminiwa....vi nchi vyetu hivi tuna vigezo tifauti kidogo...niliwahi kusikiwa baba yake mzinda.....alikuwa mganga wa rais fulani.....unadhani wazungu walivyotutukana kuwa mila na tamaduni zetu za kishenzi walikosea??? walitusoma wakatuelewa...conclusion yao naikubali daima

mix with yours
 
Nina wasiwasi kwa Magufuli, kwa sababu anawekuwa remotely controlled, but Tibaijuka ni mwanamke wa shoka.
 
Kuna jina moja tu ambalo halitajwi na litawashangaza wengi. Hii safi ya JK ni ya kumuandaa mrithi wake 2015 next PM atakuwa BENARD MEMBE (mbunge wa Mtama) Mark my word
 
Kama Tibaijuka watampa u-PM basi Magufuli wampe kwenye Madini.....!! Lakini wote hao ni watu wa kazi!
 
If so tumekwisha finest......maana heri nusu shari kuliko shari kamili
mix with yours

Ndio pale umma utakaposhangaa maana kuna majina ambayo ukiangalia utendaji wao wa kazi ni mzuri sana lakini litakuja jina ambalo haukuwahi kufikiria hata siku moja ndiyo hivyo serikali ya mkwere ilivyo tusubirie jioni ifike ili huu utabiri tunaoufanya hapa tuone kama utatimia
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…