Elections 2010 Nani kuukwaa uwaziri mkuu?

Status
Not open for further replies.
KATIBA HAIMRUHUSU! Sio mbunge wa kuchaguliwa

Lazima uwe ni mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Nahodha ni mjumbe wa baraza la wawakilishi..................Hivyo, basi katiba haimruhusu JK kumteua au bunge kulipitisha jina hilo.....................................na hata wakiaamua kuchakachua hilo ni eneo ambalo mahakam yaweza kuombwa kufuta uteuzi huo na ikafanya hivyo bila ya zengwe.......
 
Great Thinkers kuna watu wanawechemsha na kweli mnachemkaa!!!
 
Mimi niye PM wenu,mmetaka ndiyo hivyo hamkutaka mtafuata tuu.Hapa hatwendi kimbuzimbuzi kwa kuvutana kamba ila tunaenda king'ombeng'ombe kwa bakora,mpo?!
 
Nahodha siyo mbunge bali ni mjumbe wa baraza la wawakilishi zanziba, hivyo hawezi kuwa waziri mkuu, kwani sifa moja ya waziri mkuu ni lazima awe mbunge aliyechaghuliwa jimboni!
 


Najua mkwere hawezi kumpanafasi Magufuli kwa sababu anapenda vilaza, waoga, wapenda majungu, mafisadi
 
Uwaziri mkuu wa mwaka huu lazima uwe na maana ya ufisadi wa 2015
 
Ni kweli kwa nini JK aumie kichwa kwa ajili ya kumteua WAZIRI MKUU MPYA,Pinda yupo. Kitendo cha kuteua waziri mkuu mpya ni kuliingiza TAIFA katika hasara ya kuwahudumia Mawaziri wakuu wengi
 
:hippie:anapenda akina ndio mzee, siunakumbuka Magufuli alipotenda kazi ikaonekana ktk wizara ya miundombinu na akawa gumzo katika mambo ya maendeleo. baada ya hapo akampototezea akampeleka ktk wizar xxxxx lakini nako akafanyakazi na ikaonekana. Huyo mkwere ni mswahili hana lolote kumbukeni Mkwere ni Mkware, teheteheee
 
Vuai kapewa uwaziri jana na Dr. Shein - jaribu tena jina lingine!

Sidhani....hebu soma vizuri

Dk Shein ameunda Wizara 16 na kuwateua Wajumbe wa Baraza la Mapinduzi, Mawaziri na Naibu.

Walioteuliwa ni Dk Mwinyihaji Makame (Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi), Omar Yussuf Mzee (Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais: Fedha, Uchumi, na Mipango ya Maendeleo) na Haji Omar Kheri Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utumishi wa Umma na Utawala Bora).

Wengine na wizara zao katika mabano ni Fatma Abdulhabib Fereji (Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais) na Mohammed Aboud Mohammed(Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais).

Aboubakar Khamis Bakary (Waziri wa Katiba na Sheria), Hamad Masoud Hamad (Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano) na Ramadhan Abdulla Shaaban (Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali).

Juma Duni Haji anakuwa Waziri wa Afya, Zainab Omar Mohammed (Waziri wa Ustawi wa Jamii na Maendeleo ya Wanawake na Watoto), Abdilahi Jihad Hassan (Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo) na aliyekuwa Naibu Waziri Kiongozi, Ali Juma Shamhuna anakuwa Waziri wa Ardhi, Makazi, Maji na Nishati.

Pia wapo Mansoor Yussuf Himid (Kilimo na Maliasili) Nassor Ahmed Mazrui (Biashara, Viwanda na Masoko), Said Ali Mbarouk (Mifugo na Uvuvi) na Haroun Ali Suleiman (Kazi, Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na Ushirika).

Mawaziri wasiokuwa na wizara maalumu wa Baraza la Mapinduzi ni Suleiman Othman Nyanga, Haji Faki Shaali na Machano Othman Said.

Naibu Mawaziri walioteuliwa ni: Issa Haji Ussi (Miundombinu na Mawasiliano), Zahra Ali Hamad (Elimu na Mafunzo ya Amali), Dk Sira Ubwa (Afya) na Bihindi Hamad Khamis (Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo).

Wengine ni Haji Mwadini Makame (Ardhi, Makazi, Maji na Nishati) na Thuwaiba Edington Kissasi (Biashara, Viwanda na Masoko).
 
Mtoto wa Mkulima, Kamanda Pinda aka Chozi la Albino, atarejea kuongoza shughuli za serikali Bungeni, namaanisha waziri mkuu.
 
Baada ya kuchakachua kura nadhani ili CCM irudishe imani japo, nasema japo kidogo wampe Magufuli...ila kwa mtazamo wa wangu...hilo tunaota..kwani CCM huwa hawataki wachapa kazi, wanapendelea watu wanaoweza kuwasujudia na ufisadi wao, kitu ambacho Magufuli hataweza. Kingine Magufuli akiwa PM JK anafunikwa na hatajulikana kama ndiyo raisi wa nchi...
 

Katiba hairuhusu kwa sababu PM lazima awe mbunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano ambaye amechaguliwa kutoka katika mojawapo ya majimbi hata kama ni Zanzibar. Vuai si mbunge wa bunge letu wa kuchaguliwa...So that's impossible.

Kwa hiyo, tetesi iliyoletwa hapa ni TOXIC!
 
SINA wasiwasi na utendaji kazi wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mheshimiwa Benard Membe. Yeye ni miongoni mwa viongozi wachapa kazi hodari ambao taifa limepata kuwa nao.
Napenda kuamini pia kuwa Mheshimiwa Benard Membe ni miongoni mwa viongozi wetu wachache ambao utendaji kazi wao ulikwenda sambamba na kaulimbiu ya 2005-2010 'Ari mpya, Nguvu mpya na Kasi mpya'. Hii ni kaulimbiu ambayo iikuwa haizungumzwi sana kwa ari, kasi na nguvu kama ilivyokuwa ikisikika wakati utawala wa awamu ya nne ulioiasisi ulipoingia madarakani miaka mitano nyuma. Kwa nini? Kila mmoja wetu ana tafsiri yake

Anyway tuachane na hayo mimi nataka kujua Hii siri ya JK imevuja, ni kuwa BM amekuwa Waziri, source ni mbea wa ikulu
 
Mtembezi katika tembea tembea yangu kama ilvyo ada nimefanikiwa kunusa KIGOGO mmoja aliyekaribu na IKULU anadai jina la waziri mkuu mpya ni SHAMSI VUAI NAHODHA wana jamvi mpo?

Hicho KIGOGO ulichonusa ni kigogo cha Bangi,maana kimekufanya uchanganyikiwe!!
 

tuwe na subira
 
Mtoto wa Mkulima, Kamanda Pinda aka Chozi la Albino, atarejea kuongoza shughuli za serikali Bungeni, namaanisha waziri mkuu.


Ila Mizengwe kama anarudia chaka lake ni lazima sasa awe "uso wa mbuzi" (serious) by vitendo asiwe waziri mkuu wa kunyenyekea nyenyekea kwa hao mafisi maji
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…