MwanaFalsafa1
JF-Expert Member
- Feb 26, 2008
- 5,565
- 843
Jamani any updates za yanayo jiri bungeni? Uchaguzi wa spike muda gani na jina la waziri mkuu lina pendekezwa lini?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Injinia wa mambo haya ni JK wa sababu ufisadi ni jadi yake. Wakati wa kampeni amezunguka kote kwa mafisadi kuwanadi eti ni watu safi(nawashukuru Rombo walimgeuka). Kwa maana hiyo kwa sasa anaangalia nani atakuwa raisi wa Tz na anajua timu yake imechafuka na haisafishiki hata kwa jiki. Na anajua akiendelea kumpa Sita chance atazidi kuwachafua. Kwa hiyo mbaya wa 6 ni JK na ndo ubaya wa kuwa na Rais mnafikiLol !! Hiyo itakuwa garama kwa serikali kweli kweli, yaani kwa wakati mmoja wapate Spika mstaafu na Wazikiri mkuu mstaafu wote 80% ya mshahara, ulinzi magari eee mwaka huu kazi kweli kweli.
Suppose we dont have one, shall we miss anything?
Suppose we dont have one, shall we miss anything?
Na Mwandishi wetu
RAIS Jakaya Kikwete yupo kwenye hatua za mwisho kuunda serikali yake, ambayo wachambuzi wa mambo wanaeleza kwamba huenda ikawa na mabadiliko makubwa kuondoka kasoro zilizojitokeza miaka mitano iliyopita.
Mtihani mkubwa ambao unamkabiri Rais Kikwete katika kuunda serikali yake ni kumpata Waziri Mkuu ambaye atamsaidia kuongoza nchi katika kipindi chake cha mwisho cha miaka mitano ijayo.
Kwa mujibu wa shughuli za bunge, jina la Waziri Mkuu aliyeteuliwa na Rais litawasilishwa bungeni, kesho kutwa kwa ajili ya kuthibitishwa na wabunge kwa kupigiwa kura.
Wanaotajwa kwamba huenda wakaukwaa uwaziri mkuu katika ngwe hii ya pili ya Rais Kikwete ni pamoja na Waziri Mkuu anayemaliza muda wake, Mizengo Pinda.
Wachambuzi wa mambo ya kisiasa nchini wanasema kuwa Pinda anaweza kurejeshwa katika kiti hicho kutokana na rekodi yake ya uadilifu, kutokuwa katika makundi na kutohusika katika kashfa ya aina yoyote.
Pinda maarufu kama mtoto wa mkulima, amejipatia umaarufu kutokana na kutokuwa Waziri Mkuu anayependa matumizi mabaya ya fedha za umma, ikiwamo hatua yake ya kuzuia semina na safari za mara kwa mara za viongozi wa seriali nje ya nchi.
Mwingine ambaye anatajwa kuwa huenda akaupata uwaziri mkuu ni Spika aliyemaliza muda wake, Samwel Sitta.
Sitta ambaye ni Mbunge wa Urambo Mashariki, mkoani Tabora anatajwa kuwa anaweza kuupata uwaziri mkuu ikiwa ni njia ya Rais Kikwete kumfariji baada ya Kamati kuu ya CCM kumwengua kuwania uspika.
Lakini pia inaelezwa kuwa ni njia mojawapo ya kuupoza umma ambao umeonyesha kusikitika kwa kunyimwa nafasi ya Bunge, ili kurejeshea serikali yake imani kwa wananchi.
Sitta anakumbukwa chini kwa kuliendesha Bunge kwa kiwango cha hali ya juu na kuruhusu mijadala wazi na kuchangia kuibuka kwa kashfa ya Richmond ambayo ilitikisa serikali baada ya aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa kujiuzulu kwa kuwajibika na pamoja n mawaziri wawili walioiongoza Wizara ya Madini na Nishari kwa nyakati tofauti wakati wa mchakato kwa kuipitisha zabuni iliyoipa ushindi tata kwa Richmond.
Mijadala mingine ambayo ilitika nchi iliyojadiliwa bungeni ni wizi wa fedha za Mfuko wa Madeni ya Nje katika Benki Kuu (EPA) na mikataba mibaya katika sekta ya madini.
Habari kutoka Dodoma ambako kikao cha bunge kinaendelea zinaeleza kuwa gumzo kubwa sasa ni nani atateuliwa kuwa waziri mkuu.
Mtu mwingine ambaye anatajwa kuwa huenda akapewa nafasi hiyo kubwa ya utendaji wa serikali ni aliyekuwa Waziri wa Mifungo na Uvuvi, Dk John Magufuli ambaye anaheshimika kutokana na utendaji wake makini.
Magufuli ambaye ni Mbunge wa Chato mkoani Kagera ana rekodi nzuri ya kufanya vizuri katika wizara zote alizopangiwa na hana kashfa wala makundi ndani ya CCM.
Habari kutoka ndani ya serikali, zinaeleza kuwa pia Rais Kikwete anaelezwa huenda akafanya mabadiliko makubwa katika baraza lake la mawaziri ikiwamo kuunda baraza dogo la mawaziri ili kupunguza matumizi ya serikali na kuelekeza fedha nyingi kwenye shughuli za maendeleo.
Katika serikali iliyopita, Baraza la Mawaziri lilikuwa na mawaziri 27 pamoja na manaibu mawaziri 21.
Habari zilizolifikia gazeti hili kutoka kwa watu waliokaribu na washauri wa Rais Kikwete zinasema safari hii amekusudia kuunganisha baadhi ya wizara na kuunda zisizozidi 20.
Mkakati huo umeelezwa kwamba utafanywa ama kwa kuunganisha wizara au kuvunja na idara zake kuziweka chini ya wizara nyingine zinazolingana nazo kiutendaji.
Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita Rais Kikwete alijaribu kupangua baadhi ya wizara na kuhamisha baadhi ya idara kwa lengo la kuchochea ufanisi.
Miongoni mwa marekebisho aliyoyafanya kuisambaratisha iliyokuwa wizara ya Kilimo na Mifugo na kuzaa tatu, kilimo, chakula na ushirika, maji na umwagiliaji na maendeleo ya mifugo na uvuvi.
Rais Kikwete alifuta wizara mipango na Uchumi ambapo idara zilizokuwa zinahusiana na uchumi zilipelekwa kuwa chini ya Wizara ya Fedha na Mipango ikawekwa chini ya ofisi yake.
Wizara ya Sayansi, Teknolojia na Elimu ya juu pia ilisambaratishwa na Idara za Elimu ya juu kwenda Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi huku Teknolojia ikiunganishwa na Mawasiliano.
Baraza la mawaziri la serikali iliyopita lilikuwa na:
Waziri Mkuu alikuwa Mizengo Pinda akisaidiwa mawaziri wa nchi wawili ambao ni Philipo Marmo (Utaratibu wa bunge) na Celina Kombani Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) na Aggrey Mwanri (Naibu Waziri Tamisemi).
Ofisi ya Makamu wa Rais ilikuwa na mawaziri wa mchi wawili ambao ni Batilda Burian (Mazingira) na Muungano Muhammed Seif Khatibu.
Wizara ya Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo na manaibu wawili, Jeremia Sumari, Omari Yusuph Mzee.
Afya na ustawi wa jamii, Profesa David Mwakyusa, Naibu, Asha Kigoda; Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, John Chiligati na Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Jumanne Maghembe, Manaibu Gaudensia Kabaka na Mwantum Mahiza.
Mawasiliano, Sayansi na Technologia, Profesa Peter Msola na Naibu, Maua Daftari, Miundombinu, Dk Shukuru Kawambwa na Naibu, Ezekiel Chibulunje.
Habari, Utamaduni na Michezo, George Mkuchika; Naibu Joel Bendera, Kazi Ajira na Maendeleo ya Vijana, Profesa Juma Kapuya, Naibu Dk Milton Mahanga.
Maji na Umwagiliaji, Mark Mwandosya; Naibu wake ni Christopher Chiza. Kilimo Chakula na Ushirika, Stephen Wassira na Naibu Mathayo David Mathayo.
Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Magreth Sitta Naibu, Lucy Nkya; Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk John Magufuli na Naibu Dk James Wanyancha.
Maliasili na Utalii, Shamsa Mwangunga, Naibu Ezekiel Maige na Mambo ya Ndani, Lawrence Masha Naibu Hamis Kagasheki.
Wizara ya Katiba na Sheria, Mathias Chikawe, Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, Naibu Seif Ali Idi na Wizara ya Nishati na Madini, Wiliam Ngereje, Naibu Adam Malima.
Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Ally Mwinyi, Naibu Dk Emmanuel Nchimbi; Wizara ya Afrika Mashariki, Dk Diodorus Kamala na Viwanda na Masoko, Mary Nagu na Naibu Cyril Chami.
Katika kipindi cha kampeni za kugombea urais, moja ya sera zilizopigiwa debe na vyama vya upinzani ni kupunguza baraza la mawaziri ili kubana matumizi ya serikali.
Baada ya Rais Kikwete kutangaza mshindi, aliahidi kutekeleza baadhi ya sera za wapinzani ambazo zinaonekana kuwa nzuri na wachunguzi wa mambo wameeleza ni kwamba ni pamoja na hiyo ya kupunguza ukubwa wa baraza la mawaziri.
Bajeti za serikali kwa miaka mitatu iliyopita ni 2007/08 Sh 6 trilioni, 2008/09 sh 7.2 trilioni, 2009/10 sh 9.1 trilioni na 2010/11 Sh 11 trilioni.
Ingawa serikali imekuwa na mafanikio katika ya ukusanyaji wa mapato miaka ya karibuni na kupunguza utegemezi hadi kufikia asilimia 40, inaelezwa kuwa matumizi makubwa yamekuwa yakienda katika matumizi ya kawaida badala ya miradi ya maendeleo.
Chanzo: Gazeti la Mwananchi