Wadau;
Kuna tetesi kwamba Ikulu imesita kupeleka jina la PM mteule (ilikuwa liende Dodoma asubuhi hii), badala yake litapelekwa alasiri kwa Spika wa Bunge ambaye ataliwakilisha kwa Wabunge wamuidhinishe kuwa PM!
Kuna habari kwamba Mwandosya, Magufuli, Tibaijuka na Pinda ni majina yaliyokuwa katika meza ya Mheshimiwa Rais. Kulikuwa na tetesi pia kwamba Edward Lowassa na Dr. Harrison Mwakyembe walipigiwa chapuo na makundi mawili tofauti yenye ushawishi katika siasa za Tanzania.
Mwakyembe:
Alionekana ana uwezo, msomi aliyebobea na ambaye CCM wapiga debe wake (kundi linalomtetea) wamekuwa wakishinikiza apewe nyundo kumaliza ufisadi maana wananchi walivutiwa sana na jinsi kamati yake ilivyokuwa mstari wa mbele kushughulikia issue ya UFISADI. Kwa bahati mbaya ameondolewa kwa kuhofia upinzani atakaoupata kutoka kwa wababe wa siasa za bongo wakiongozwa na EL, RA na wafanyabiashara wanaoisaidia CCM
Lowassa:
Anajulikana kwa makeke yake; haiba na mvuto kwa jamii. Ni swahiba wa JK na ana ushawishi mkubwa sana ndani ya CCM. Kinachomkwaza JK kumchukua, japo anatamani sana kumrejesha tena ni ile kashfa ya Richmond! Inasemekana JK anataka kutumia kigezo cha idadi nyingi za kura alizopata jimboni kwake kuonyesha kwa watanzania kuwa bado EL anakubalika. Kuna kundi linaloongozwa na viongozi wastaafau wanaopinga hili kutokea....JK anahofia kwamba akimchukua CCM itamomonyoka!
Pinda:
Ndiye PM kwa sasa, kulingana na hali ya kisiasa ilivyop, jinsi CCM ilivyoaibishwa kwenye uchaguzi JK anaona Pinda si mtu wa aina anayoitaka pale. Anadhani Pinda ni muoga na mkimya sana, anataka mchapakazi, anayeogopewa na mwenye ushawishi katika siasa za Bongo! Kitendo cha PM kulia bungeni, kudeclare kwamba anawaogopa mafisadi nk vinamfanya JK akose imani na Pinda. Inasemekana pia kwamba wakati wa kampeni za urais Pinda yeye hakujishughulisha kukisaidia chama, aliamua kukaa pembeni kutokujihusisha na uchakachuaji, kitu ambacho JK anakiona kama ni usaliti! Kinachomfanya aendelee kumfikiria ni kwamba kama atamtosa sasa ina maana ataongeza ma-ex PM, itakuwa ni kama kuongeza mzigo wa bajetio ya serikali, ameshauriwa aendelee naye hadi 2015 ambapo Pinda mwenyewe atastaafu kwa hiari!
Mwandosya:
Vyanzo vyetu vinadai kwamba Mark Mwandonsya hana ushawishi kwa baadhi ya vigogo wa chama chake, na kwa wananchi. Washauri wa JK wameona kumpa nyundo huyo kutadhoofisha makali ya Serikali na kumuongezea mzigo JK....kitu ambacho kitaexpose weaknesses za president....
Tibaijuka:
Hadi sasa anaongoza katika list, JK anataka kumpa nyundo mama huyu nguli amabaye ameonyesha ukomavu wa kisiasa na mwenye upeoo mkubwa sana katika anga za kimataifa! Kundi kubwa la vigogo wa Chama wanamtaka mama huyu amabaye anakubalika sana pia katika maeneo ya maziwa makuu. Inasemekana JK anatatizwa na kitu kimoja tu...tayari Dr. Asha Rose Migiiro ametajwa na ameshaombwa kuja kuomba urais kupitia CCM (2015) na tayari ameonyesha nia;sasa endapo PM akiwa Tibaijuka itakuwa vigumu kwa Rais na PM wake wote kuwa wanawake 2015!! Mbaya zaidi inasemekana pia Tibaijuka ana mpango wa kuomba kiti cha urais 2015!! Kwa taarifa tu ni kwamba uamauzi wa Dr Migiro ndiyo utaamua kama Tibaijuka apewe u-PM au la! Endapo atakuwa PM ina maana Dr. Migiro hatarejea kugombea 2015...ili kumpisha Tibaijuka abanjuke na upresidaa!!
Magufuli:
JK, washauri wake, CCM na wapinzani hawana hoja against huyu jamaa. Kila mmoja anajua kwamba ni mchapakazi, msomi na hana woga! Anakubalika sana na wananchi na upande wa wapinzani pia. JK anafahamu kwamba jamaa ni jembe na akimpa mpini basi chombo kitakaa mrama! TAtizo ni moja; JK anaogopa kufunikwa na Magufuli na inasemekana ana bifu naye binafsi.! Pia mafisadi wanahofia akipewa u-PM itakuwa mwisho wa wao kuichezea nchi hii, na mawaziri wanamuogopa, inasemekana kuna njama zinafanyika aondolewe hata kwenye baraza la mawaziri!! Tatizop wanajua wananchi watapiga kelele na itakuwa aibu kwao....Uwezekano wa yeye kupata u-PM ni endapo tu kama mama Migiro ataendeleza msimamo wake wa kuwania urais 2015.....
Tusubiri tuone