Elections 2010 Nani kuukwaa uwaziri mkuu?

Elections 2010 Nani kuukwaa uwaziri mkuu?

Status
Not open for further replies.
Habari za kuaminika nilizopata hivi punde ni kuwa Mzee Pinda anaendelea na kazi yake kwani anafaa. Waziri wa Fedha ndo Mh. EL, yaani hapo ndo nikachoka mbaya.

Duu huyu atakuja na mradi wa Ndege kutengeneza mvua za kichina...hapana za kithailand vile? hakya nani tumekwisha kwani safari hii anakula bila kunawa
 
Mmhhh mi yangu macho, nasuburi tu huyo Jk amtangaze, sina papara.
 
wazee wala msihangaike kupiga ramli Pinda anaendelea kama kawa kutokana na kukwepa garama.
ni ngumu sana kumtoa pinda wakati hajafanya mistake yeyote pia itakua mzigo kwa serikali kuwahudumia mawaziri wakuu wastaafu walioko mtaani kwa sasa.
wakati kikwete anaingia madarakani magofuli na mwandosya walikua ndo pendekezo but kikwete akawakataa kutokana na urafiki wake na lowasa na kama mnakumbuka siku ile ya kupeleka jina bungeni magufuli alianguka na kuzimia gafla so hata sababu hazikuwekwa wazi.
Kwa hiyo magofuli mkwere hawezi kumweka kwa sasa itakua aibu.
 
Hivi ni nini kilimwondoa Tibaijuka kule UN - Habitat? Nasikia aliingizwa na Kofi Annan kwa sababu ua uswahiba na pia alichemsha kwenye tender hapo nchini Kenya.
 
kaka tunashukuru umechambua vizuri sana....Ila please invisible tunaomba uziunganishe hizi topic za tetesi kuhusu waziri mkuu ili watu waweze kuchangia kwenye mada moja.
Cheers.
 
Wakuu, kikao kimeshamalizika. Pinda kapewa amalizie ngwe ya mwisho na JK. Kulikuwa na ki-debate cha hap na pale juu ya candidates wengine lakini imeonekana kubadilisha spika na wazri mkuu kwa wakati mmoja chini ya rais mmoja haitakuwa vizuri. Hizo ndo busara za wazee wa chama otherwise yangetokea ya kutokea. No more explanations.
 
nakuhakikishia jk hawezi kumteua magufuli kuwa pm. unakijua kilichopo kwa hawa wawili +lowasa?

unajua lowasa na kj walimfanya nini pombe mwaka 2005?

thubutuuu hata kwa dawa hawezi kumoa nafasi ile labda wawe wameanza kusalimiana jana
 
Hivi katiba hairuhusu waziri Mkuu ataazimwa kutoka nje? Maana nimeshtuka hapa hatuna mzalendo ndani ya CCM. Kama katiba inaruhusu mkuu achonge na Gadaffi atupe mtu.
 
Hivi ni nini kilimwondoa Tibaijuka kule UN - Habitat? Nasikia aliingizwa na Kofi Annan kwa sababu ua uswahiba na pia alichemsha kwenye tender hapo nchini Kenya.


Muda wake kule uliexpire
 
labda niseme hivi

jk ana bifu na magufuli pombe tangu kabla hata ya 2005. na tatizo kubwa alikuwa ni lowasa wakati ule lowasa ni waziri wa maji...

na kwa taarifa ni kwamba jk akikutana kwenye kona na magufuli hawasalimiani hali iko hivyo hata kwa lowasa

hawa watu hawasalimiani kabisa na chanzo cha jk kutofautana na magufuli ni pale magufuli alipovalia njuga mashine za kuchimia visima ambavyo lowasa alitaka kuvitaifisha na kuwa mali yake, yeye(lowasa) na jk ndo walikula dili hilli. so magufuli akalitibua mpaka kwa Ben mkapa na hapa dili likashindikana.

tangia hapo hwa watu waliingia bifu kubwa sana mpaka leo....
 
Habari kutoka Dodoma zinasema kuwa kati ya Tibaijuka na Magufuli mmojawapo atateuliwa kuwa Waziri Mkuu. Awali kulikuwa na candidates watatu mezani kwa Kikwete; akiwemo Mwandosya, ambaye sasa jina lake limeondolewa.
Akitambua bayana kuwa serikali yake haina haiba wala mvuto wa kutosha kuungwa mkono na wananchi, Kikwete amesema anataka waziri Mkuu "kukuru-kakara" atakayeweza kuburuza hybrid policy katika kilimo, viwanda (manufacturing) kwa ajili ya kuleta impact katika ajira. Huu ni mkakati wa ku-mobilize vijana amabo wanaonekana kuitupa mkono CCM, hasa kutokana na uzoefu wa CCm kutoungwa mkono na vijana wengi wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa 2010.
Nwasilisha. Tuendelee kutega masikio yetu.[/QUOTE
]
TATIZO NI KICHWA CHA TRENI NDIO KINA MAPUNGUFU, HATA MAWAZIRI WA WA AWMU YA KWANZA BAADA YA KUWATEUA AKWA ANAFANYA KAZI NA MAKATIBU WAKUU MOJA KWA MOJA KUPITIA KWA KATIBU KIONGOZI. MMESAHAU YALIYOTOKEA KWA MALIASILI WAKATI WA MKURUGENZI ALIYEKATAA UHAMISHO WA WAZIRI NA KATIBU MKUU KISA KULINDWA NA KATIBU MKUU KIONGOZI.

KWA HAKIKA KASI WALIYOANZA NAYO WAZIRI DIALLO NA KATIB U MKUU SALEHE PAMBAPALE MALIASILI ILIKUWA KALI NA LEO HI MALIASILI ZETU ZOTE ZINGEKUWA MIKONONI MWETU, LAKINI ALIWAKATISHA TAMAA MWENYEWE. HATA HAWA ATAKAOWATEUA SASA ATAWAKATISHA TAMAA PIA.
 
Itakuwa kher kwa Watz kama Magufuli atavikwa hilo rungu, huyu jamaa ana sifa ya kutoangalia uso wa mtu na husema ndiyo akimaanisha ndiyo na hapana kwa maana ya hapana. Anafanana na Dr Slaa kwa mbali ila kasoro yake ni kwamba yupo ndani ya pakacha la samaki wengi waliooza(ccm). Bali hata hivyo haiwezekani kwa Magofuli kwani habari kutoka chanzo cha kuaminika zinajuza kuwa waziri mkuu ni Sofia Simba (MB) na wizara ya mambo ya ndani atapewa Lyatonga Mrema (MB).
 
Kwakuwa Chama cha chaka chua matokeo kilishaanzisha mpango wa kuwajali wakina mama, mpango wa kumpa u PM mama Tibaijuka kilikuwa sahihi.
Mama huyu ana uwezo mkubwa sana ila sijui kwa mafisadi kama angefanya kwa amani.
 
Pinda anaendelea. Hakutamka wala kufanya yale yanayofanana na ya Sitta. Tatizo liko kwenye wizara nzito kama Mambo ya Nje ni Membe au Tibaijuka? Katiba na Sheria ni Chikawe au Sitta? Mambo ya Ndani ni Mrema/ Shamsi Vuai Nahodha au Ngeleja?

Shamsi Vuai Nahodha - naomba elimu hapa, huyu bwana kwani yupo ktk wabunge wamuungano kutoka visiwani au?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom