Nani kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar baada ya kifo cha Maalim Seif Sharif Hamad?

Nani kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar baada ya kifo cha Maalim Seif Sharif Hamad?

kwa jinsi SUK ilivyoanza kazi ndani ya siku 100 maalim alikuwa anakwenda kumtengenezea njia ya ushindi mkubwa bwana hussein mnamo 2025.

maalim hakuwa na nguvu tena ya kuwa mgombea wa uraisi mnamo 2025 hivyo angelikosekana mwanadamu sahihi aliyetoka kwenye system ya serikali mwenye uwezo wa kumchalenge hussein kwenye jukwaa lijalo
hivyo ndivo ilivyo, Hussein Mwinyi kwa njia alizoanza nazo kujaribu kuenda na siasa za usawa ni wazi kuwa asingeweza kushinda uchaguzi ujao bila ya kupata support ya ACT kimakubaliano, bila ya hivo atalazimika kurejesha vurugu za nyuma.
 
Jussa nadhani bilashaka.. Kama hakulainika na kipondo kile, huu ni wakati wake kujipambanua.

BACK TANGANYIKA
 
ukisoma comment za wachangiaji juu ya maalim na uamuzi wake halafu ukaamua kufanya ziara ndogo mitaani unakutana na dunia tofauti...

Hao waliokua wakipiga kelele maalim kasaliti ni wahuni wa JF na twitter, wafuasi wa Maalim hawajawahi kutetereka.
 
huyo Hamad Masoud hafai mkuu, Na siamini kama anaweza kuwemo hata katika watakaopendekezwa.
Juma Duni Haji nadhani experience na age,vitam favour achaguliwe, Mansour anapendwa ila Mwinyi hawezi kumuweka kijana mwenzie kwenye ile position kwa sababu anahitaji mtu wa makamo kuliko yeye na mwenye uzoefu mkubwa wa siasa.
 
Ni wazi kwamba Gwiji la siasa za Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad amefariki ( Apumzike kwa amani ) lakini ikumbukwe kwamba Zanzibar bado ingalipo na itaendelea kuwepo.

Sasa bila shaka Katiba ya Zanzibar inatambua uwepo wa Makamu wa Kwanza wa Rais, je imeeleza chochote jambo kama la kifo linapotokea? Na kama ACT Wazalendo wanaruhusiwa kujaza nafasi ya Maalim Seif unadhani ni yupi awezaye kuvaa viatu hivi?

Anayefaa kuchukua nafasi ya Maalim ni Mhe Juma Duni Haji, no hullabaloo!
 
Jussa anafaa zaidi ili kuleta mawazo mbadala chanya kulingana na mahitaji ya kizazi cha sasa. Hata Maalim Seif(RIP) alianza kuaminiwa akiwa bado kijana ndio maana ameweza kuhimili mikikimikiki ya siasa kwa weledi mkubwa. Hivyo ikiwapendeza wana ACT na Mh. Rais wanaweza kupata mchango mkubwa wa mawazo na fikra pevu mbadala kwa maendeleo ya Wazanzibari wote.
 
  1. nassor mazrui haitowezekana kuwa makamo kwa sababu ameteuliwa kuwa muakilishi na raisi, muda wowote anaweza kuziba nafasi ya uwaziri katika ya wizara mbili walioachiwa ACT. makamo wa kwanza haingii kwenye baraza la wawakilishi
  2. kuhusu Jussa sidhani kama itawezekana kuchaguliwa, nitakupa sababu zangu private kama utahitaji (jussa ni rahisi kumchafua mbele ya jukwaa)
  3. mansour na Duni ndio wabeba maono wa upinzani na wote wameshajijengea mvuto mbele ya hadhira, wote ni wazungumzaji na wahamisishaji wazuri
A person needed is from PEMBA unless otherwise
 
Imeeleza nimesahau ibara na kifungu ila inasema "endapo makamu wa kwanza wa Rais akafa Rais alieko madarakani anaruhusiwa "kuteua"mwingine..
Hivyo baada ya msiba kupita Rais anaruhusiwa kikatiba "ya kwao huko"kuteua makamu wake

Sent using Jamii Forums mobile app
Nadhani hauko sawa. Katiba yao inatambua nafasi ya makamu wa kwanza wa Raisi na kwamba atatoka kwenye chama kilichopata angalau asilimia kumi ya kura kwenye uchaguzi mkuu. Na chama kilichopata ushindi kina nafasi ya kutoa makamu wa pili wa Rais.

Kwa mantiki hii, ACT Wazalendo ndicho chama kilichokidhi hili takwa la kikatiba, kilipata zaidi ya asilimia kumi, na ndiyo maana kilipewa nafasi ya kupendekeza jina la Makamu wa kwanza wa Rais, na Maalim Seif (RIP) akapendekezwa na chama chake, na hatimaye kuapishwa na kuwa makamu wa kwanza wa Raisi wa SMZ.

Nafasi hii ni yao (ACT), kwa vile Maalimu Seif katutoka, ACT watapeleka jina la mwanachama mwingine - Mzanzibari kujaza nafasi ya Maalim baada ya muda utakaporuhusu kikatiba, na si vinginevyo. Hivyo ndo ninavyojua mimi.
 
Back
Top Bottom