Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 25,252
- 36,513
Hotuba ya jana tarehe 17 Septemba 2024 imenipa simanzi sana. Lakini nimeokota neno moja linalotumiwa kule Kizimkazi. Neno hilo ni MHULUKUTABU na lilitolewa ufafanuzi kuwa ni mtu ambaye akiona kuna utulivu lazima aibue hekaheka. Rais aliwalenga wapinzani na wahanga wa utekaji na mauaji ya raia.
Hebu tujiulize hapa kidogo
Je Tanzania inaongozwa kwa mujibu wa sheria au kwa amri za rais?
Je haki ya raia nj kutendewa lolote na dola hata kama ni unyama kisha ashukuru aende zake?
Soma pia: Rais Samia Kwa Mabalozi: Hatupo hapa kuelekezwa nini cha kufanya kwenye nchi yetu
Niliwaambia mwaka 2022 na leo narudia tena. MUNGU AMEONDOA KAULI VINYWANI KWA VIONGOZI na hakuna wa kuzuia anguko kubwa linalofuata hivi punde
Hebu tujiulize hapa kidogo
- Raia wanapiga kelele kuwa wsnamalizwa na tuhuma zinawaendea vyombo vya usalama
- Rais na wasaidizi wake wanasema hizo ni drama na hakuna utekaji. Wameenda mbali zaidi kuwa watu wanajiteka wenyewe wakitumia refference za polisi ambao ni watuhumiwa namba moja
- Baadhi ya walionusurika kuuawa na ambapo Rais anatoa fedha HAZINA kuwatibia (e.g. SATIVA) wanawatambua watesi wao kwa majina na sura
- Viongozi wa CCM kada mbalimbali wanasimama kusema watawateka na kuwapoteza wapinzani na kuwataka polisi wasiwaingilie. Na polisi wanatii hakuna kesi ya kutekwa na kuuawa iliyowahi kukamilika
- Wasaidizi wa Rais ambao ni Waziri na DC wanasimama hadharani kukiri namna wanavyoshiriki kubaka demokrasia na haki za kuishi. Lakini wanastaafishwa ambapo inaleta tafsiri kuwa kosa lao ni kutoa siri hadharani
- Rais na wasaidizi wake wanapiga KIMYA kirefu sana hadi leo
- Utekajj unafanyika mchana kweupe tena mbele ya raia wengi na kisha mhanga kuuawa na kutupwa.
- Rais anapeleka rambirambi kwa wafiwa as if roho ya marehemu inathaminishwa kwa pesa.
- Wananchi wanademand haki yao ya kuishi na kulindwa lakini inafasiriwa ni uvunjivu wa amani. Mfano ni kule Busega ambapo polisi walipuuza matukio ya wananchi kutekwa na kuuawa na walipoandamana wkaishia kutupiwa risasi za moto na kumuua mtu mmoja.
- Rais jana amesema kuwa wananchi watakaodai haki yao ya kuishi inayovunjwa na vyombo vya dola hao ni wavunja amani na washughulikiwe. Ameenda mbali zaidi kuwaita watu hao MAHUKUKUTABU.
Je Tanzania inaongozwa kwa mujibu wa sheria au kwa amri za rais?
Je haki ya raia nj kutendewa lolote na dola hata kama ni unyama kisha ashukuru aende zake?
Soma pia: Rais Samia Kwa Mabalozi: Hatupo hapa kuelekezwa nini cha kufanya kwenye nchi yetu
Niliwaambia mwaka 2022 na leo narudia tena. MUNGU AMEONDOA KAULI VINYWANI KWA VIONGOZI na hakuna wa kuzuia anguko kubwa linalofuata hivi punde