Nani Mkali kati ya Diamond na Chris Brown?

Nani Mkali kati ya Diamond na Chris Brown?

Furaha kusoma Chibu ameandikwa na kufikiriwa kufananishwa na wasanii wa nje.
 
Hii inawezekana ni kweli Diamond yuko level za Chris Brown. Kama JLo alimkimbia Shilole studio kwenye kurekodi wimbo inashindikana vp diamond kumkimbiza Brown? Mtoto wa Tandale ni upenyo tu wa kuingia media za USA hajapata. Habari za chinichini inasemekana ni haters wa USA wanamkwamisha.
 
Eminem na nani sasa? labda na FidQ, sidhani kama huyo Eminem atawafikia kina Profesa Jay na Mr. Two kwa sasa jamaa wanavuta mpunga kibao bungeni kwa sasa?
Ndiyo mkuu, huna habari kuwa wameshinda ubunge hawa?

kwa taarifa yako Jay ni mbunge wa mikumi na Mr. 2 ni wa Mbeya mjini.
Eminem yeye si atakuwa anategemea show tu? na recently hana hata kibao kinachovuma.

Hapa ndio nilipoamini kua bangi za kuvutia chooni sio nzuri kwa afya ya ubongo wako.
 
Acheni kufananisha chill sauce na pilipili manga.. nyambafu, lini diamond aka linganishwa na chris brown????
 
Ni sawa na kubishania kuwa kati ya sinza dares salaam.na mchamba wima zanzibar wapi kuna watu wengi
 
BARNABA, BEN POL, RAMA DEE, hawa ndio wana imba RNB... na sio DIAMOND, ALIKIBA NA OMMY DIMPOZ.
 
Nisawa na kumlinganisha r kelly na buju banton kwenye category ya r n b... Halafu buju banton ashinde.... Diamond anaimba anaimba zuku,taarab,singeli,mnanda na jamii inayofanana na hiyo, wakati chris brown anaimba rnb na wakati mwingine huwa anarap. Sasa unaposema diamond ni mkali kwa kitu asichokifanya unakuwa haueleweki ndugu...
 
kabla ya kwenda kote huko ungeanza diamond na chameleon,au hata nyoshi el saddat!
 
Eminem na nani sasa? labda na FidQ, sidhani kama huyo Eminem atawafikia kina Profesa Jay na Mr. Two kwa sasa jamaa wanavuta mpunga kibao bungeni kwa sasa?
Duh mkuu hata ujielewi kwanza show moja anayo piga eminem unganisha malupulupu yote ya ubungr wa sugu na mr 2 hawamfikii, jmaa ni producer yupo mbali sana kwenye malipo anayopata kwenye production licha ya hiyo check net worth yake hata hawa mafisadi wa hawamfikii itakuwa hao wakina sugu
 
Daaah tengua kauli Chris brown na diamond?,,,,,,kua serious basi
 
ishu hapa ni sauti yakuimba mkuu...
Diamond mpambanishe na Harmonize,maana kwa sauti hamfikii Christian Bella au Ali Kiba,kumpambanisha na Chris Brown ni kosa unalotakiwa kujuta wewe mngese
 
ishu hapa ni sauti yakuimba mkuu...
1453132581070.jpg
 
Diamond mpambanishe na Harmonize,maana kwa sauti hamfikii Christian Bella au Ali Kiba,kumpambanisha na Chris Brown ni kosa unalotakiwa kujuta wewe mngese
mkuu mbona unajibu kwa jazba?ebu relax kidogo ikiwezekana suuza nafsi na coca baridi apo grocery ya jirani...
huyo kiba na bella sauti zao zimewafikisha wapi?huyo unaesema hawafikii hao kwa sauti pia muangalie yupo wapi,licha ya kuwa na sauti mbaya?
kiba na bella wanaweza kuwa na sauti nzuri lakini diamond ana sauti tamu aise,acha kabisa!
 
Back
Top Bottom