Nani msemaji wa elimu aliyebaki Bungeni? Naona walimu wa private wananyanyaswa sana

Si ungemtaja huyo mbunge Humu . Sasa unaficha Ficha nini

Sent from my CPH1937 using JamiiForums mobile app
 
Kwahiyo wanafunzi ndiyo wanatakiwa kula chakula cha ajabu?
 
siku watanzania mtakapoacha kuwa wanyonge na kujisimamia kutetea haki zenu basi hapo ndio mtakuwa mmejiokoa..
 
dogo komaa hata na iko kilaki 2, graduates wamejaa huku mtaani mpaka sio vizuri
Manyanyaso kawaida, lasivyo kajiajiri
 
Mshahara ni mapatano baina ya mwajiri na mwajiriwa, kama mlipatana mlipane laki mbili, hapo hakuna cha kulaumu...
Huu ni mtazamo finyu, usiojali maslahi ya wengine na maslahi mapana ya Taifa. Makubaliano kati ya mwajiri na mwajiriwa yapo lakini hayapaswi kuwa yenye ukandamizaji na ndio maana baada baadhi ya nchi zina sheria zinazoongoza viwango vya mishahara kwa kila kazi. Ukiruhusu waajiri wapange mishahara kwa sababu wanaohitaji ajira wapo wengi, ipo siku wote watakubaliana walipe elfu hamsini kwa mwezi. Je walimu wote waache kufanya kazi wakafanye mambo mengine? Wadogo zetu na watoto zetu atawafundisha nani?

Na kama watumishi wote wa umma wakiamua kuacha hizo kazi zao kwa sababu ya maslahi madogo, ukandamizaji kazini, na sheria kandamizi kisha wakaamua kuwa wakulima ama wajasiriamali, majukumu yao atayatimiza nani? Au unaona wanachokifanya hakina msingi?

Watu wanapolalamikia unyanyasaji kazini kimbilio lisiwe kuwaambia waache kazi bali kutafuta suluhu kwa kuweka sheria bora zinazolinda maslahi na haki zao. Kutokuwepo kwenye hizo kazi haimaanishi kuwa hufaidiki nazo.
 
Hujiewi na hujui kazi ya wizara ya elimu. Nenda kenya private ni kama serikali kuna kima cha chini na cha juu cha mshahara kilichopangwa na serikali na lazima mwajiri ufate la siyo unakuwa liquidated.

Haki zote za mfanyakazi ni lazima siyo ombi na anaweza kukupeleka mahakamani na huna gats za kumfukuza. Nenda kenya ujionee acha mawazo mgando ya kidictator.
 
Kuna shule inaitwa Macmillian nay hazilipi mishahara walimu wake hata kwa miezi 4
 
Wanaopaswa kuwatetea ndio wamiliki wa shule. Hata Ndalichako mwenyewe walimcharukia kama mbogo alipotaka kuzuia wanafunzi kusoma mwaka mzima bila ya likizo.
Kukosekana kwa taasisi imara kumepelekea vigogo na waliofungamana na CCM kuamua watakavyo.
 

Umetaja shule na mahali ilipo, na kusema ni ya mbunge, mbona huyo mbunge hujamtaja? Arusha ni kubwa, sema ni Arusha wilaya gani, na jina la huyo mbunge mmiliki ili tumuanike, na kuhamasisha wazazi wasipeleke wanafunzi kwenye hizo shule za madhalimu.
 
Umetaja shule na mahali ilipo, na kusema ni ya mbunge, mbona huyo mbunge hujamtaja? Arusha ni kubwa, sema ni Arusha wilaya gani, na jina la huyo mbunge mmiliki ili tumuanike, na kuhamasisha wazazi wasipeleke wanafunzi kwenye hizo shule za madhalimu.
Alichukua nafasi ya esta matiko.
 
Kaka usiwe mbishi, pita pita mashulen huko kaangalie, hali n mbaya sana, wala usibishe, jamaa anachosema ni kweli kabisa, na hao walimu sio wa tempo km unavyohisi, ni professional kabisa Mkuu na waajiriwa.
 
Siwajui wabunge wengi wa ccm maana hawakuchaguliwa na wananchi. Taja jina lake acha uoga bana. Unatumia fake Id ila bado unakuwa muoga! Ndio maana wanawapelekesha hapo shuleni.
Michael kembako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…