Nani Mtani Jembe: Simba Vs Yanga

Nani Mtani Jembe: Simba Vs Yanga

wakimataifa

JF-Expert Member
Joined
Nov 16, 2014
Posts
942
Reaction score
168
Nawauliza wadau wa mpira au TV yoyote hapa nchini mechi hiyo, tv ipi itaoneshwa live


MASHABIKI-1-4-620x400.jpg


Jumamosi, December 13 jibu la nani mkali kati ya Simba na Yanga, watani wa jadi katika soka la Tanzania, litafahamika. Simba itaingia uwanjani siku hiyo ikiwa na kumbukumbu ya ushindi wa mabao 3-1 katika mechi ya msimu uliopita wa kampeni ya Nani Mtani Jembe.

Yanga itacheza kwenye mtanange huo kama kifaru aliyejerehuwa, ili tu kuhakikisha kuwa historia haijurudii.

Isitoshe, vijana hao wa Jangwani wamekuwa wakitamba kuwa Simba haitotamba awamu hii. Simba wao, wamesikika pia wakisema Yanga haina lolote na lazima historia ijirudie.


Na ndio maana wekundu hao wa Msimbazi walimsajili mshambuliaji wa wa Gor Mahia ya Kenya, Dan Serunkuma ili kuboresha safu yake ya ushambulizi.


Nao Yanga walimsajili Mbrazil, Emerson De Oliveira Neves Roque kwa madhumuni hayo hayo, kuimarisha kikosi chake. Ni wazi kuwa mechi ya Jumamosi kati ya mahasimu hao wa Tanzania itakuwa ya kukata na shoka na si ya kukosa.

KiliLager.com
================

UPDATES

VIKOSI VYA LEO YANGA VS SIMBA

YANGA:
Deo Dida
Abdul Juma
Oscar Joshua
Nadir Haroub
Kelvin Yondani
Mbuyu Twite
Haruna Niyonzima
Emerson Roque
Simon Msuva
Kpah Sherman
Coutinho

SIMBA:
Ivo Mapunda
Nassor Chollo
Mohammed Hussein
Hassan Isihaka
Juuko Murishid
Jonas Mkude
Rama Singano
Awadh Juma
Elius Maguri
Simon Sserunkuma
Emmanuel Okwi

Dk 2, Okwi anapiga mkwaju wa faulo lakini unadakwa vizuri na Dida.
Dk 3, Yanga wanafanya shambulizi, Sherman anampa pasi nzuri Msuva anapiga shuti linadkwa na Ivo
Dk 5, Sserunkuma Jr anatolewa nje anatibiwa baada ya kugongwa na Yondani
Dk 7, Sherman anawachambua mabeki watatu wa Simba lakini anashindwa kumalizia
Dk 11 Emerson anapiga krosi safi lakini Coutinho anaukosa mpira
Dk 13 vurugu zinazuka, lakini mwamuzi anachukua maamuzi magumu na kutotoa kadi...ubabe unatawala
Dk 17, Okwi anawachambuamabeni wawili wa Yanga lakini anaangushwa na kuwa faulo, anaipiga Okwi...goal kick

Dk 23, Sherman anagongeana vizuri na Msuva na kutoa pasi nzuri....lakini hakuna mmaliziaji
Dk 25 Sherman anampa pasi nzuri Msuva naye anaachia shuti kali lakini linapiga nyavu za nje.
GOOOOOOOOOOOOO DK 30, Awadhi Juma anauwahi mpira wa faulo wa Okwi na kuukwamisha wavuni ilikuwa ni baada ya Dida kuutema.

Dk 33, Coutinho anapiga shuti saafi lakini linatoka nje sentimeta chache
Dk 40, Yanga wanamtoa Twite aliyeumia, nafasi yake anachukua Hassan Dilunga
GOOOOOOOO Dk 41 Maguri anaifungia Simba bao baada ya kuunganisha mpira wa kurusha wa chollo ambao uligonga mwamba, mabeki wa Yanga wakazubaa, akarudi na kufunga tena.

MAPUMZIKO
Yanga wanamtoa Coutinho wanamwingiza Danny Mrwanda
Dk 46 Simba wanamtoa Murishi wanamwingiza Joseph Owino
Dk 48, Msuva anapiga shuti kali lakini mpira unazuiwa
Dk 49, Sherman anawaacha mabeki wa Simba, wanamuangusha, inakuwa faulo inayookolewa na mabeki wa Simba

Dk 52 Yondani anafanya kazi ya ziada kuokoa mpira mbele ya Messi Singano. Simba bado wanatawala katikati ya uwanja

Dk 56, Yanga inamuingiza Salum Telela na kumtoa Mbrazil, Emerson
Dk 63, Mliberia Sherman anatoka nje mwenyewe baada ya kuumia. Awali alirudi, lakini anaonekana kuzidiwa
Dk 65 Yanga wanamuingiza Mrisho Ngassa kuchukua nafasi ya Mliberia Sherman aliyeumia
Dk 66, Mrwanda anapiga mpira langoni kukiwa na mabeki tu, Owino anaruka juu na kuokoa kwa kichwa.
Dk 65, Simba wanamtoa Tshabalala Mohammed Hussein aliyeumia, nafasi yake inachukuliwa na Issa Rashid 'Baba Ubaya'

Dk 72, Simba wanamtoa Messi na nafasi yake inachukuliwa na Said Ndemla
Dk 76, Ngassa anapiga krosi lakini inaishia mikononi mwa Ivo Mapunda
Dk 78 Yanga inamtoa Juma Abdul na kumuingiza Javu
Dk 84 Simba wanamtoa Maguri, nafasi yake inachukuliwa na Danny Sserunkuma. Mwamuzi anampa Maguri kadi ya njano kwa kupoteza muda

Dk 86, Simba wanamtoa Simon Sserrunkuma na kumuingiza Shabani Kisiga
Dk 87, mashabiki Yanga wanaanza kutoka uwanjani, Simba wanawazomea
Dk 89, Mrwanda anaangushwa, Niyonzima anapiga lakini Ivo anadaka kiulaiiinii
Zimeongezwa dakika nne.

Mpira umekwishaaa!

Full time: Yanga 0-2 Simba
.
 
ndugu zangu njooni tu uwanjani muangalie mechi.Hadi sasa hakuna makubaliano ya kurusha live mchezo huo.

Jamal hizi mechi za kugombea mbuzi huwa mara nyingi zimejaa vurugu tu....

Kama wasipoonesha tutasikiza hata kwa redio...
 
Hata wasiporusha kwani hasara ya nani?,tutazikiliza radio
 
Kichwa Cha Habari Kimeshajieleza Na Najiamini Kwa Asilimia Zote100 Kwani Tumeshamaliza Kila Kitu. Na Yanga Mkifungwa Wa Kuwalaumu Ni Wachezaji Wenu Hawa Watatu Nadir Haroub, Kelvin Yondan Na Simon Msuva.........Kwanini SIRI NINAYO Mwenyewe......Kila Tajwa Hapo Juu Lazima Atatoa Boko Moko Kwa Simba Hivyo Mtafungwa Idadi Ya Magoli Ya Wachezaji Tajwa Hapo Juu.....................NIMEMALIZA na Nawasilisha!
 
Bahati mbaya sana ujumbe wako utaishia hapa hapa JF...

Na mwisho wa siku utatamani uzi huu ufutwe lakini ndio mtakuwa mshachezea nakozi...
 
Kichwa Cha Habari Kimeshajieleza Na Najiamini Kwa Asilimia Zote100 Kwani Tumeshamaliza Kila Kitu. Na Yanga Mkifungwa Wa Kuwalaumu Ni Wachezaji Wenu Hawa Watatu Nadir Haroub, Kelvin Yondan Na Simon Msuva.........Kwanini SIRI NINAYO Mwenyewe......Kila Tajwa Hapo Juu Lazima Atatoa Boko Moko Kwa Simba Hivyo Mtafungwa Idadi Ya Magoli Ya Wachezaji Tajwa Hapo Juu.....................NIMEMALIZA na Nawasilisha!
Toa huu utumbo hapa.
 
Tena mwambie kabisaaaa huyooo.... kwenye kilaji washakaa sasa watakaa na uwanjani... wakacheze vigodoro ndo wanaweza.. ILA MI MISI YU SAANAA

Haaaaaaaa eti wakacheze vigodoro.....,

Mi mwenyewe miss u mbaya kitambo sana
 
Una uhakika? au ulitaka nawe uonekane umeanzisha uzi?
 
Simba Timu funga kandambili hao goli za kutosha.
 
Yanga wanazidi kuongeza mamluki, DANNY MRWANDA? mtajuta!
 
Wadau zikiwa zimebaki dakika nyingi kipenga kipulizwe,huu ni mpira mkubwa kupigwa taifa kati ya Mnyama majeruhi na Watoto wa Jangwani wazee wa "importation made in Brazil".Game hii naileta kwenu hapa JF kwa ushirikiano wa wadau wote. Karibu tuione Simba ya Sserunkuma na Yanga ya Mbrazili.Karibuni sana
 
Back
Top Bottom