Nani Mwenye Kosa hapa!?

Nani Mwenye Kosa hapa!?

Egyps-women

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2010
Posts
497
Reaction score
107
Based on true true story!
Ann na Brenda Ni mashort wa siku nyingi sana urafiki wao uligeuka na kuwa undugu hata kuziunganisha family zao
..Ann alikuwa muwazi sana kwa mwenzie lakini Brenda alikuwa mkimya sana na alipenda kuongea mambo ya masomo maisha na dini kwa ujumla huku akisisitiza anawachukia sana wanaume na pia kumsisitiza sana Ann asome kwa bidii na aachane kabisa na swala zima la mapenzi .

Kijana Mike aliondokea kumpenda sana Brenda na kuamua kumtuma rafiki yake Ann amfikishie msg hii ,Ann alikaa na jambo hili akiwaza na kuwazua namna ya kuanza kumwambia Brenda lakini ilimchukua kama mwaka mzima hajaweza kusema.
Alimsisitiza sana Mike amwambie mwenyewe kwani yeye anaijua misimamo ya Rafikie Brebda ..ingawa Mike alikuwa akimsalimia Brenda anaitikia na kuendelea na mambo yake.
Ann alijikuta ameingia kwenye penzi zito sana na Mike na kupeana ahadi za ndoa mara mambo yao yakikamilika..

Kumbe Brenda nae alikuwa na penzi zito sana kwa Mike toka amemuona ila kwa aibu zile za kike hakuweza kuzisema hisia zake .

Mwisho wa siku Brenda Baada ya kugundua Mike alimtuma Ann kwake na hakumwambia lolote walianza uhasama na chuki ambayo hakuna anayeweza kuizima mpaka leo.
Jamani nani mwenye kosa kati ya hawa marafiki wawili na huyu Mike wao
Na nini kifanyike kuwasaidia!!:A S-rose:
 
Mpigieni makofi shangazi! Nani kakufundisha hadithi hii? Kakwambia ina maana gani? Nenda kakae
 
Kimsingi kama ni kosa wa kwanza kulaumiwa ni Mike,yeye kama mwanaume kwanini asimwambie Brenda?Kosa la pili ni Brenda kusema chuki zake waziwazi zilizopelekea Ann asimwambie alichotumwa,Annie hana makosa hapo.Solution ni Brenda kukubaliana na hali halisi na kumuomba radhi rafikie na waendelee na maisha!
 
Huyo Brenda alikuwa 'akisisitiza hapendi wanaume' sasa mwenzake kajisevia kiulaini yeye awe mtulivu na kuendelea kuwachukia wanaume.
 
Mh...ngoma droo hakuna mwenye makosa! tena Brenda amshukuru Mungu hakupata khabari mapema maana angeweza kuwa heart broken pale ambapo Mike angekuja kugundua alichokuwa anakaiona kwa Brenda (on the outside) is not who Brenda really is.

Tena speaking from experience, nilitokea kumpenda msichana mmoja tukiwa sekondari, yani nilionaga bila yeye maisha hayaendi, na alikuwa mpole na mkimya sana nikashindwa njia ya kumweleza. Nikawa namtumia rafiki yake kuwasiliana, to cut the long story short, i came to realize (after 7 years) her true colors.

What is beneath that silence, yeye bado yupo chuo ila what she is doing?

Mh. Sorry, nimeanzisha topic..nitaiweka kwenye thread yake...but hope ujumbe umeupata.
 
Kimsingi kama ni kosa wa kwanza kulaumiwa ni Mike,yeye kama mwanaume kwanini asimwambie Brenda?Kosa la pili ni Brenda kusema chuki zake waziwazi zilizopelekea Ann asimwambie alichotumwa,Annie hana makosa hapo.Solution ni Brenda kukubaliana na hali halisi na kumuomba radhi rafikie na waendelee na maisha!

Inakuaje mkubwa?? hujakutanaga na wadada kama hawaee? yani wao wanajifanya mwanaume ni kama simba kwao au shetani mdogo..kumbe ndani wanaugulia...Mike hakuwa na makosa kabisa, alimwona from outside akaona solution ni kumwomba rafiki yake amsaidie..!!!
 
Hakuna mwenye kosa hapo..Brenda aanze ustaarabu tu wa maisha yake asimchukie mwenzie
 
Kimsingi kama ni kosa wa kwanza kulaumiwa ni Mike,yeye kama mwanaume kwanini asimwambie Brenda?Kosa la pili ni Brenda kusema chuki zake waziwazi zilizopelekea Ann asimwambie alichotumwa,Annie hana makosa hapo.Solution ni Brenda kukubaliana na hali halisi na kumuomba radhi rafikie na waendelee na maisha!

Mi nikiongeza neno hapo nitaharibu.
 
Kimsingi kama ni kosa wa kwanza kulaumiwa ni Mike,yeye kama mwanaume kwanini asimwambie Brenda?Kosa la pili ni Brenda kusema chuki zake waziwazi zilizopelekea Ann asimwambie alichotumwa,Annie hana makosa hapo.Solution ni Brenda kukubaliana na hali halisi na kumuomba radhi rafikie na waendelee na maisha!

Hilohilo ndo nilikuwa naliwaza, umegusa palepaleeeeeee!!
 
Back
Top Bottom