Davidmmarista
JF-Expert Member
- Apr 11, 2024
- 1,367
- 2,451
Habari zenu wadau wa JamiiForums!
Leo nimekuja na mada 🔥 inayogusa maendeleo yetu kama Waafrika. Tumeona dunia ikibadilika kwa kasi kutokana na teknolojia, lakini swali ni moja: Kati yetu Waafrika na mataifa mengine ni nani mwenye teknolojia zaidi?
Tukitazama historia, Afrika ilikuwa na teknolojia zake asili kabla ya ukoloni mifumo ya kilimo, ujenzi wa miji kama Timbuktu, na hata matumizi ya sayansi katika tiba pia baadhi ya sehemu kama misri ilikuwa na teknolojia kama pyramid.
Ila leo, tunashuhudia mataifa ya Magharibi na Asia yakiongoza kwa teknolojia za kisasa kama AI, blockchain, biotechnology, na uchunguzi wa anga(aerospace).
Je, sisi Waafrika tuko nyuma kwa sababu ya ukoloni, uongozi mbovu, au ni kwamba tunahitaji kubadilisha mtazamo wetu wa kiteknolojia? Kuna mafanikio mengi Afrika kama M-Pesa, makampuni ya tech kama Andela, na matumizi ya drone katika sekta ya afya, operating system ya computer kama Ubuntu(Linux). Je, haya yanatosha kutupeleka mbele?
Wadau, naomba mawazo yenu:
1. Afrika inahitaji kufanya nini ili kuwa kinara wa teknolojia duniani?
2. Je, tuna rasilimali za kutosha kuzidi mataifa mengine?
3. Ni teknolojia gani ambazo tunapaswa kuwekeza zaidi?
Karibuni kwenye mjadala! Twende tukaijenge Afrika yetu kwa maarifa na technology!