Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
WASIFU WA JULIUS NYERERE: NANI ATAKUWA NA UJASIRI WA KUISAHIHISHA KAULI YA MWALIMU PALE ALIPOKOSEA TAARIFA KATIKA HISTORIA YA TANU NA MAISHA YAKE MWENYEWE?
Nasoma kitabu cha historia ya Mwalimu Nyerere na kuna mengi nimejifunza ambayo kwa hakika nilikuwa siyajui lakini pia kuna mengi ambayo nimekutananayo ambayo nayajua kwa kuyasoma kabla katika Nyaraka za Sykes na haya ninayosoma leo baada ya miaka 30 kupita wakati mwingine hayashabiani na ushahidi wa nyaraka hizo nilizosoma.
Unawezekana muda ukalaumiwa kwa kupoteza kumbukumbu za binadamu.
Kutegemea mtu akaeleza historia yake tena katika hotuba baada ya zaidi ya miaka 70 kukosea si jambo la ajabu ila bei yake inakuwa aghali mno.
Kurasa za mwanzo tu katika kitabu cha pili cha Wasifu wa Julius Nyerere panaelezwa mkutano wa mwanzo ambao Nyerere alifanya Mbeya na katika mkutano ule wazee aliozungumzanao Mwalimu walionyesha hofu yao ya kudai uhuru kutokana na yale yaliyotokea katika Vita Vya Maji Maji iliyosababisha unyama mkubwa kutendeka dhidi ya wananchi walionyanyua silaha kupambana na Wajerumani.
Mwalimu katika hotuba yake ya kuaga aliyotoa Ukumbi wa Diamond mwaka wa 1985 kayaeleza haya na waandishi wa maisha yake na wao katika kuanza kueleza mwanzo wa harakati za Mwalimu kuwaamsha watu kujikusanya katika umoja kudai uhuru wameanza na hii hofu ambayo Mwalimu aliikuta kwa wazee alipowatajia jambo la kudai uhuru.
Mkutano wa kwanza wa Mwalimu Nyerere kuzungumza na wazee haukuwa Mbeya bali ulikuwa Morogoro ambako alikwenda na Zuberi Mtemvu mwezi August, 1954 mwezi mmoja tu baada ya kuundwa kwa TANU.
Mtemvu alimuomba baba yake Mzee Mwinshehe Manga Mtemvu awakusanye wazee wenzake ili wafanye mkutano wa ndani kuhusu TANU.
Bahati mbaya mkutano huu haukufanikiwa.
Mtemvu akamwandikia barua Ally Sykes kumfahamisha mambo mawali.
Jambo la kwanza alimweleza Ally Sykes yale yaliyowakuta yeye na Nyerere Morogoro kwa kumwambia kuwa ‘’Waluguru ni wagumu,’’ kwa maana kuwa wazee wa Kiluguru wameshindwa kuupokea ujumbe na wito wa TANU.
Jambo lingine alimfahamisha Ally Sykes kuwa amezungumza na Ali Mwinyi Tambwe kuhusu TANU na Ali Mwinyi amekubali kuwaunga mkono.
Barua hii Zuberi Mtemvu kaiandika kwa penseli (Zuberi M.M. Mtemvu to Ally Sykes, 15 th August, 1954).
Yawezekana haya maneno ya hofu ya kuwakuta wana TANU kama yale yaliyowakuta wapiganaji wa Maji Maji, Mwalimu aliyasikia Morogoro na ndiyo haya Mtemvu aliyomweleza Ally Sykes kuwa ‘’Waluguru ni wagumu.’’
Hofu hii ya Vita Vya Maji Maji Mwalimu bila wasiwasi aliisikia Lindi na Mikindani kwani huko kusini ndiko vita vile vilipopiganwa kwa wakati ule, kiasi cha miaka 50 tu iliyopita.
TANU haikufika Mbeya haraka hivyo.
Katika historia ya TANU hofu ya wananchi kuwafika yaliyowafika wapiganaji wa Maji Maji ilikuwa ikitumika sana Southern Province, sehemu za Lindi, Mikindani, Masasi na Nachingwea.
Wamishionari walikuwa wanawatisha waumini wao wakae mbali na TANU wasije wakafikwa na yale waliyowafika wazee wao baina ya mwaka wa 1905 na 1907 wakati wa vita vile.
Kupambana na propaganda hii waasisi wa TANU Lindi, Suleiman Masudi Mnonji, Yusuf Chembera na Salum Mpunga wakatuma ujumbe wa watu wawili, Salum Mpunga na Ali Ibrahim Mnjale, TANU HQ Dar es Salaam ambao ndiyo walikuwa wajumbe wa mkutano wa kwanza wa TANU 1955 wabaki nyuma baada ya mkutano wawafahamishe viongozi wa TANU propaganda inayopigwa Southern Province kuwazuia wananchi wasiunge mkono TANU kwa hiyo Nyerere aende haraka akazungumze na wananchi.
Mwalimu Nyerere alikwenda Lindi akifuatana na Ali Mwinyi Tambwe na alifanya mkutano mkubwa Golf Ground ambao haukupata kuonekana.
Ilikuwa huko Southern Province ndiko Mwalimu alipoelezwa hofu hii ya watu kunyongwa iliyokuwa inaenezwa kuwazuia wananchi wasijiunge na TANU kudai uhuru.
Mwalimu alifanikiwa kuvunja propaganda ile na TANU ikaenea kote - Lindi, Mikindani, Masasi na Nachingwea.
Ukiruka historia hii ya wana TANU wa Southern Province na propaganda ya Vita Vya Maji Maji ukaingia Mbeya kwa muasisi wa TANU Fatima bint Matola historia muhimu sana inakuwa imepotezwa.
Picha ya kwanza nyumba ya Ahmed Adam Mikidani aliyolala Mwalimu Nyerere katika safari yake ya Southern Province (Picha kwa hisani ya Adam Ahmed Adam).
Picha ya pili ni Salum Mpunga na ya tatu Yusuf Chembera.