Faana
JF-Expert Member
- Dec 12, 2011
- 38,657
- 44,759
Ningependa kujua ni nani mwenye wajibu wa kulinda transfoma za TANESCO dhidi ya wezi wa mafuta ya machine hizo? Imetokea mara kadhaa (zaidi ya mara nne kwa mujibu wa wahanya/ wateja) transforma iliyowekwa kwenye pori na TANESCO katika mtaa wa Vespo Kihonda Morogoro kuibiwa mafuta yake nyakati za usiku na kusababisha wakazi wa eneo husika kukosa umeme kwa muda mrefu.
TANESCO wakifika kwenye eneo la tukio huwaambia wakazi wanaotumia transfoma hiyo wachangishane na kuweka ulinzi, wananchi nao wakiiwaambia TANESCO waweke taa pamoja na uzio katika eneo hilo, wanasema si jukumu lao.
Nawauliza TANESCO nani hutakiwa kulinda transfoma zao? Kama wateja hulipa bili inakuwaje watakiwe kuchanga fedha za ulinzi wa transfoma ambayo wao wenyewe wameiweka kwenye pori? Na kwanini wananchi wanapowaambia wajengee vizuizi na kuweka taa kwenye transfoma hiyoTANESCO wanakwepa? Je tukisema TANESCO wana ubia na wezi wa mafuta hayo tunakosea?