Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,307
- 25,932
Yale yaliyofichuliwa ndani ya CHADEMA sasa yanajidhihiri kwatika namna ifananayo ndani ya ACT-Tanzania. Kuna mgogoro mkali unafukuta hasa kuhusu uongozi. Wahusika mbalimbali wanaojiita Kamati Kuu, wenyeviti na nafasi nyingine wanatokeza kila kukicha wakidai kufanya vikao halali na kutoa maamuzi halali ya kiuongozi.
Hadi sasa kumekuwa na Kamati Kuu mbili. Kamati Kuu hizi zote zimedai kufanya vikao halali na kutoa maamuzi halali. Kimsingi,vikao na maamuzi husika yanabaki kuzunguka kwenye uongozi na mamlaka kama ilivyoshtukiwa ndani ya CHADEMA na wahusika kutimuliwa chamani.
Cha ajabu na faida, mtu kama Samson Mwigamba alitajwatajwa CHADEMA kwenye kile kilichokuwa kikijulikana kama Mkakati wa Mabadiliko. Sasa anatajwatajwa ACT-Tanzania. Mwenyekiti wa muda wa ACT-Tanzania-Bwana Limbu na timu yake anapambana na Mwigamba na timu yake. Demokrasia iko wapi? Ama kweli CHADEMA waliona mbali.
Naomba kujua,ndani ya kadhia hii ya ACT-Tanzania MM,MM1,MM2 na MM3 ni akina nani?
cc Nyakarungu
cc Mwl.Kaijage

Last edited by a moderator: