Nani ungependa awe Mwanasheria Mkuu mpya wa Serikali ya Rais Mpya ?

Wasilisha jina lako kabla muda haujaisha
 
yaani Mwanasheria mkuu mnataka awe mzee wa MIGA??
Yaani mnataka yule aliyesema KISHERIA MADINI SI YETU ndo mumkabidhi nafasi kufanikisha MADINI KUTOKUWA YETU??

Yaani nafasi nyeti hivyo mumpe mtu asiyejua kuwa TRENI YA MPANDA ipo??
ACHENI ùtani wa mambo ya nchi na vijiwe vya kupigishana soga
 

Mimi ningependelea mmojawapo kati ya watu wafuatao awe mwanasheria mkuu wa serikali;

(1) Audax Vedasto Kaendaguza

(2) Francis Kwilabya Stolla

(3) Alex Mgongolwa
 
Mtu ambaye anatakiwa kuwa mwanasheria mkuu wa Tanzania kwa kipindi hiki tulichopo watanzania ni lazima awe mtaalamu wa sana wa katiba na sheria za kimataifa: hasasa kwenye tafiti, usuluhishi wa migogoro, baishara za kimataifa, uwekezaji na rasilimali.Hivi vipengele viwili vya sheria ndivyo vimeshikilia mfumo mzima wa mwenendo wa nchi yetu hasa kwenye kipindi hiki cha utandawazi.

Profesa Kilangi mbali na kutotimiza kigezo cha muda, lakini ni moja kati ya wanasheria ambao wanazifahamu vizuri sana sheria za kimataifa na kuzifanyia kazi. Binafsi nashauri Raisi aendelee kumtumia huyu msomi wetu hata kama atateua mwanasheria mkuu mwingine. Nafasi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ni kubwa sana, lakini sijui kwanini kwetu hapa tunakuwa tunafikiria kwamba kila mwanasheria anaweza kuipata.
 
Aliyeingia kinyume cha sheria anawezaje kuwa mwanasheria mahiri ?
 
Wewe umahiri wa mwanasheria unaupima kwa kutumia vigezo gani ???
Tuanze hapa ili tuwe ukurasa mmoja.
Moja ya umahiri wa Mwanasheria ni kuweka sheria zinazochochea haki kupatikana , si sheria kandamizi
 
Hili suala muachia Samia. Hata hivyo, msitegemee mabadiliko makubwa hasa ikizingatiwa kuwa rais alikuwa akishirikiana naye kuwateua hawa waliopo japo si wote.
 
Hili suala muachia Samia. Hata hivyo, msitegemee mabadiliko makubwa hasa ikizingatiwa kuwa rais alikuwa akishirikiana naye kuwateua hawa waliopo japo si wote.
Ashirikiane na nani ? Thubutu !
 
Kwahiyo anahusika siyo ?
Serikali nzima inahusika, wadau mbalimbali wanahusika, vyama vya upinzani vinahusika, mashirika binafsi n.k
Uhusika wa AG ni kuishauri serikali kuhusu masuala yote ya sheria, lakini yeye hatungi sheria.
Pia hana kura ndani ya Baraza la Mawaziri hivyo maamuzi siyo yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…