Leo katika kucheki Mwanachi ya leo nikakuta habari nzuri isemayo MAMA AJIFUNGUA WATOTO 5! Nilifurahi sana nikasema hana haja ya kuongeza watoto wengine wametosha.
Nilipoendelea kusoma newz hii, huyu mama ni uzazi wake wa 10! Pia ameshawahi kujifungua mapacha mara 6,jumla ana watoto 20 now!!!
Hivi hili ni kosa la nani hasa Baba au Mama? Jamani 2punguze offside uwanjani!!!
Mama ajifungua watoto watano
Send to a friend Monday, 13 December 2010 20:47
Shija Felician, Kahama
MWANAMKE mmoja mkazi wa Kijiji cha Bulungwa kilicho wilayani Kahama amejifungua watoto watano, wakiwemo watatu wa kike na wato wanaendelea vizuri.
Mama huyo, Shija Maige, 33, ambaye anatokea Kata ya Bulungwa, amejifungua watoto hao katika uzazi wake wa kumi na mara sita kati ya hizo alijifungua watoto mapacha.
Habari zimeeleza kuwa Maige alijifungua watoto hao juzi katika kituo cha afya cha Bulungwa, lakini baadaye alihamishiwa Hospitali ya Wilaya ya Kahama kwa huduma zaidi.
Kwa mujibu wa habari hizo, mama na watoto hao wote sasa wanaendelea vizuri hospitalini hapo.
Wauguzi wa hospitali hiyo ya wilaya waliliambia gazeti hili jana kuwa mwanamke huyo alifikishwa hospitalini hapo saa 12:00 alfajiri juzi na gari la wagojwa.
Walisema gari hilo lilienda kumchukua baada ya uongozi wa kituo hicho cha afya kutoa taarifa za tukio hilo kwenye uongozi wa wilaya.
Mganga mkuu wa Wilaya ya Kahama, Leonard Subi alisema mwanamke huyo alianza kupatwa na uchungu na kuanza kujifungua akiwa nyumbani kwake.
"Baadaye familia yake ikaamua kumkimbiza kwenye kituo hicho cha afya cha Bulungwa kwa ajili ya huduma za kitaalamu," alisema Dk Subi.
Dk Subi alisema baada ya kufikishwa katika kituo hicho cha afya, wauguzi walianza kutoa huduma kabla gari hilo la wagonjwa kufika. Baada ya gari hilo kufika alihamishiwa hospitali ya wilaya.
"Jambo la kwanza alipofika, aliongezewa damu iliyopungua kutokana na harakati za kujifungua," alisema mganga huyo.
Mganga huyo alisema mama huyo alijifungua salama, lakini uzito wa watoto wake haukuwa wa kawaida.
"Uzito wao ni kuanzia kilo 1. 250 hadi kilo 1.700. Uzito huo uko chini sana kwa vile wastani mzuri wa watoto kuzaliwa hapa kwetu Tanzania ni uzito wa wastani kuanzia Kilo 2.5.
Mama huyo aliwaambia waandishi wa habari hospitalini hapo kuwa mimba hiyo aliyojifungua watoto watano ni ya kumi.
Alisema aliwahi kujifungua mapacha katika
mimba ya sita na kwa uzao huo wa sasa, idadi ya watoto wake
imefikia 13.
Maige alieleza kuwa ameolewa na anaishi na mume wake aliyemtaja kwa jina la Charles Marco.
Hata hivyo, ameomba msaada kutoka kwa wasamaria wema na mashirika mbalimbali ili kuweza kuwalea watoto hao.