Kutokana na mvutano wa ushiriki wa senza ktk ya Waislamu na serikali, nimeamua kurejelea moja ya maandiko ya kitabu kiitwacho VITA DHIDI YA UGAIDI kilichoandikwa na Yericko Nyerere (mimi), hii inaweza kutupa taswira ya ujengaji wa hoja kwa upande wa wapinga sensa na serikali,
UHUSIANO WA SIASA ZA DUNIA NA DINI
Historia ya siasa duniani haitengani na historia ya dini. Vitu hivi vimekuwa sambamba na vyenye mafaa kwa jamii yoyote ile duniani, lakini vikileta matatizo makubwa sana katika baadhi ya nchi duniani, matharani ubaguzi wa kiimani umeleta machafuko na uharibifu mkubwa mali pamoja na mauti dhidi ya binadamu.
Vitu hivi imekuwa ni vigumu sana kutenganisha katika dunia ya leo huku machipuko ya kiimani yakija kwa kasi ya ajabu. Kwa upande wa Tanzania mfumo wa siasa umekuwa ni wa kuakisi kutoka mataifa ya Magharibi, na uakisi wake umekuwa ni kinyume. Tukiangalia historia ya binadamu tunaona yakuwa kabla binadamu hajajishughulisha na masuala ya siasa na utawala alikuwa anajishughulisha na maswala ya dini, binadamu akawa mcha-Mungu.Ulipofika wakati wa uteuzi wa kiongozi wa jamii mtu aliyeteuliwa kushika nafasi hiyo alikuwa ni yule aliyeonekana ni mcha-Mungu. Hata katika jamii zetu za kiafrika zilizotuletea kiongozi wa utawala, pia alikuwa kiongozi wa dini. Ni huyu aliyeongoza shughuli zote za utawala na za dini katika jamii.
Itatumika biblia kutoa mifano hai kuthibitisha uhusiano wa dini na siasa. Hakuna ubishi dunia inakubali yakuwa Yesu Kristo ndiye mwanzilishi wa dini ya kikristo. Hii ni kusema kuwa Yesu Kristo alikuwa kiongozi wa dini. Kwaupande wa kabila Yesu alikuwa Muebrania. Alipozaliwa nchini Uyahudi alikuta tayari watu wa kabila lake wanadini yao ya kiyahudi. Viongozi wa dini ya kiyahudi walikuwa pia watawala waliotawala kwa kutumia sheria za kiyahudi zilizomo katika kitabu chao cha sheria kiitwacho TORATI sheria hizo za dini zikawa pia sheria za utawala. Warumi walipoanzisha utawala wao, Wayahudi waliwaruhusu Warumi kufuata sheria zao za dini ambazo pia zilikuwa sheria za utawala wao wa jadi.
Kuhani Mkuu ambaye alikuwa kiongozi mkuu wa dini, alikuwa mwenyekiti wa Baraza kuu la utawala lililoitwa Sanhedrin. Ni baraza hilo ndilo lililotoa hukumu kuwa Yesu auawe (Math 26:65-69). Hata hivyo adhabu yoyote ya kifo iliyotolewa na baraza kuu la wayahudi ilibidi ithibitishwe kwanza na mtawala wa Kirumi kabla haijatekelezwa (Yohana 18:31). Kwa upande wa Yesu Kristo alipoanza kufundisha dini yake mpya alikosoa sheria za kiyahudi ambazo aliziona hazikuwasaidia binadamu kuishi kwa upendo na amani. Aliwataka wafuasi wa dini yake mpya wasiwe na tabia ya kulipa kisasi.
Kwamfano sheria za kiyahudi zinasisitiza kauli ya jicho kwa jicho na jino kwa jino. Katika (Math 5:38-41) tunasoma yakuwa Yesu hakutaka sheria hizo, alisema, Mmesikia kwamba imenenwa jicho kwa jicho na jino kwa jino, lakini mimi nawaambia msishindane na mwovu lakini mtu akupigae shavu la kuume mgeuzie na la pili na mtu atakaye kushitaki nakuitwaa kanzu yako mwachie na joho. Uongozi safi wa kidini wa Yesu Kristu uliwavutia wayahudi wa kawaida hata wakaona anafaa kuwa kiongozi wa utawala, wakataka kumfanya awemfalme. Lakini Yesu hakuwa tayari kujiingiza mno katika masuala ya siasa na utawala (Yohana 6:15) alizoea kusema ufalme wake sio wa ulimwengu huu (Yohana 18:36) Katika mafundisho yake, Yesu hakuwahi kuwaambia wafuasi wake wasichanganye dini na siasa.
Hata hivyo aliwataka wawe waangalifu katika kuyashughulikia masuala hayo mawili. Alisema, Ya Kaisari mpeni Kaisari na ya Mungu mpeni Mungu. (Luka 20:25). Hakuwahi kuwataka wafuasi wake washughulike na mambo ya mungu (dini) tu na wasijishughulishe na siasa. Katika hali hii niwazi kuwa kiongozi wa dini hatakiwi kuhubiri siasa katika jengo la ibada akaacha mambo ya mungu. Vilevile anapokuwa nje ya jengo la ibada hana mwiko wakutokuzungumzia masuala ya siasa na utawala. Baada ya kufa Yesu, wafuasi wake waliendelea kujihusisha na masuala ya dini na siasa, mambo ya utawala yakiendelea kuhusishwa na dini. Iliaminika kuwa mamlaka yote yanatoka kwa Mungu (Warumi 13:1).
Katika hali hiyo kiongozi wa Katoliki duniani Papa wa Roma alipewa mamlaka makubwa ya utawala, eneo lake la Vatican likapewa hadhi ya utawala wa nchi. Eneo hilo likapewa mamlaka kamili yakupokea mabalozi wakigeni. Hatua hiyo ilichukuliwa kutokana na imani ileile iliyojengeka siku nyingi kuwa kiongozi wa dini ndiye anayefaa kuwa kiongozi wa utawala pia maana kwanjia hiyo atakuwa nanafasi nzuri ya kupambana na maovu. Lakini wakati Papa wa Roma anashughulikia zaidi masuala ya dini kuliko ya siasa na utawala, kuna viongozi wengine wa dini wamewahi kupewa madaraka kamili ya kushika utawala wa nchi. Mfano Askofu Mkuu Makarios wa kisiwa cha Cyprus ambaye aliwahi kutembelea Tanzania.
Wakati huohuo kuna nchi duniani ziliamua siku nyingi kuwa nchi za dini mfano Uingereza ni nchi ya kikristo ambapo mishahara ya maaskofu hulipwa na serikali. Pia nchi za Saud Arabia, Moroco na Libya ni nchi za kiislamu. Si hivyo tu pia kuna nchi ambazo vyama vya siasa vya kidini vinaruhusiwa mfano Ujerumani Christian Democratic Union (CDU). Kwa upande wa Tanzania nchi iliyozoea mapokeo, ni vigumu sana kupembua ni falsafa iliyotumika kutenganisha dini na siasa. Kwakuanzia watawala wetu, wameshikilia kuwa dini na siasa ni vitu viwili tofauti kabisa, wanasema tusichanganye dini na siasa. Wanasema nchi yetu takatifu haina dini lakini watu wake wanadini. Huu ni ulaghai wa kimtazamo na kifikra, itakuwaje nchi isiwe na dini halafu watu wake wawe na dini?.
Kunaumuhimu gani wa kuiombea mema nchi hii inayoaminika kuwa mungu aliiteua kuwa kisiwa cha amani na utulivu duniani ilihali wakaazi wa nchi hii wako mlengo wa kushoto na minajili ya munyazi mungu. Inafahamika yakuwa dini ilikuwepo hata kabla ya Yesu kristu na Mtume S.A.W hawajazaliwa. Kuna kitu kipo ndani yake, bora tuwe wawazi tuuambie umma kuwa Tanzania haina dini rasmi kama ilivyo na lugha rasmi ya Kiswahili. Fikra za Mwalimu J.K Nyerere na wasaidizi wake ni vigumu sana kubeza kwani zilichambuliwa kwanza kabla ya maamuzi na ndiyo maana zinakuwa na mafaa mbele ya Tanzania yenye mshikamano, upendo, amani, utulivu na isiyo na udini wala ukabila katika kizazi hiki cha nyoka.
Inaaminika kuwa mfumo uliotumika katika jambo hili ni fumbo la imani, na ndiyo siri ya amani na utulivu wa kisiwa hiki ambacho hakijawahi kuonja mtutu wa bunduki tangu enzi za akina Kinjekitile na akina Mkwavinyika (Mkwawa) kwani hata uhuru ulipatikana kwa sound (demokrasia). Inatia simanzi na kufanya nyoyo za waungwana ziende kasi kanakwamba mtoa rohokashagonga hodi, pale inapodhihirika kuwa wale wanazuoni tuliowapa kibali cha kusimamia lile fumbo la imani, wanasimamia kinyume na maagano ya Mtakatifu Julius K. Nyerere. (Nimtakatifu kwasababu zilizo wazi). Aliwaamini, aliwapenda, akawapa elimu yakimagharibi bure kwa jasho la wananchi, lakini leo wamemsaliti! Wanataka kujua nini kilicho ndani ya fumbo la imani! Wanataka kujua uimara wa imani ya mtanzania!
Tuliwapeleka wakasome magharibi, tena kwakuuza migomba na kuku huku tukijitunuku mshikamano na umoja wetu tukitumia dhana ileile iliyotupatia uhuru ya hakuna udini wala ukabila, leo wanakuja kufanyia field (mafunzo kwa vitendo) kwetu tena katikati ya mwamko wakiimani ya kila mmoja. Kunaulazima wa kuwa na mahakama ya kadhi? Je mahakama zilizopo hazikidhi haja? Je kunaulazima wa mahakimu kujua biblia, au msahafu kuliko kujua sheria za nchi? Maswali yote hapo juu jibu lake wanalo wanazuoni.
Leo wanazuoni hawa wanajaribu kila liwezekanalo kuisilimisha Tanzania, kwa shinikizo la Maulamaa wa umangani!, hii ni aibu na fedheha kubwa, Majuto yapo kwa wananchi tuliotoa leseni kwa wanazuoni hawa kutuongoza Shime! Watanzania tufikiri kabla yakuridhia majaribio ya wanazuoni hawa. Lakini wanazuoni wajue kuwa imani ya mtu haijaribiwi. Inasadikika na kuaminika kuwa Tanzania kuna dini kuu mbili, ambazo ni Uislamu na Ukristo. Kinadharia na kivitendo hakuna dini ambayo ndiyo kioo cha Taifa kama ilivyo Lugha ya Kiswahili.
Kujiunga na Jumuiya za Kiislamu (Afrika na Duniani) nikuzika umoja tulionao, Amani tuliyonayo na baadaye kuzalisha chuki na Udini ndani ya nyoyo zilizo katikati ya muhimili mkuu wa kiimani. Waislamu na Wakristo tusibariki majaribio haya, kwani wahanga wa machafuko ni makabwela, kwakuwa baada ya hali ya hewa kuwa mbaya, wanazuoni hawa utawaona wakiwa katika meza pana ya kutafunia kuku wakijinasibu kwa mapatano mseto, wakati tuliovunjika viuno tukiwa tunaugulia bila ruzuku wala kifuta jasho. Kwanadharia hiyo wanazuoni wanaandika barua za kuacha kazi! Kwaheshima na taadhima, Nguvu ya umma izijibu barua hizo kwa kuweka ugoko juu ya mchakato mgando wa
Kuisilimisha TZ. Uwezo tunao, Nia tunayo na Sababu tunayo!!!!!!
NB
Bado naamini kuwa hakuna ubaya wa kipengele hicho kuwepo au kutokuwepo, jambo jema nikukaa kama taifa nakufanya uchaguzi (kujadiliana kwa amani)
Imeandikwa kuwa "mamlaka zote zimewekwa na mungu", la mimi Yericko Nyerere naamini kuwa kuna mamlaka zingine zimewekwa na SHETANI