Nimemsikiliza vizuri huyo "vunjabei" na kutokana na maongezi yake anaonekana atafanikiwa akipata msaada toka serikalini, Simba na wapenda michezo kwa ujumla. Kwa maelezo yake inaonekana anajua wakina nani huwa wanaleta jezi feki na sehemu wanapozitengeneza hizo jezi feki huko China. Na kwakua amefanya biashara muda mrefu China na hata bongo anaijua vizuri basi ni jukumu la TRA na vyombo vya dola kumsaidia pale atakapoleta taarifa za uhakika ili watuhumiwa wakamatwe na mizigo yao itaifishwe/iharibiwe ikikamatwa bandarini. Kwa kufanya hivyo serikali itakuwa inapata kodi stahiki kutoka kwa wafanya biashara halali kama "vunjabei" na vilabu vyetu vyote vitapata udhamini unaostahili kutokana na mauzo ya jezi na bidhaa nyingine kwa kupitia nembo za vilabu.
Kuna watu hapa wanabisha na kuona udhamini wa bilioni mbili kuwa ni mkubwa. Kiuhalisia kabisa kwa timu kama Simba au Yanga udhamini wa kutengeneza bidhaa kupitia nembo ya vilabu hivi viwili haupaswi kuwa chini ya bilioni 10 iwapo kutakuwa na usimamizi sahihi na kuzuia bidhaa feki zisiingie sokoni. Hizi timu inakadiriwa kila moja kuwa na wapenzi/mashabiki wasiopunguwa milioni 20. Je tumeshawahi kujiuliza kuwa iwapo wapenzi/mashabiki milioni 2 tu wakinunua jezi za juu tu kwa kati ya TZS 25,000 mpaka 35,000 ni kiasi gani kitapatikana kama faida baada ya kuondoa gharama? Hapo bado hujakutana na wale wapenzi/mashabiki wehu kama laki 5 hivi hao wakanunua bidhaa nyingine zote kama skafu, cover za simu, kofia n.k.
Ni wakati sasa wa kuwapa sapoti badala ya kuwakatisha tamaa watu waliojilipuwa kama "vunjabei" ili wakifanikiwa vilabu vyetu vitafaidika na serikali nayo itapata kodi stahiki.