Nani yupo nyuma ya Taliban? Miaka karibu 20 ya vikosi vya Marekani na washirika wake Afghanistan ni Bure?

Mada mzuri, wacha kwanza nifanye hili na lile lakini ningependa kuweka kumbukumbu sawa kwamba, Taliban waliingia Afghanistani katikati ya miaka ya 90!

Lakini kwa ufupi ni kwamba, ISI wana mkono wao ndani ya Taliban! Na kwavile enzi zile ISI na CIA walikuwa wanaendesha pamoja covert ops, basi hata hao CIA nao wana mkono wao ndani ya Taliban kwa namna moja au nyingine!!!

Hapo pia huwezi kuiacha Saudi Arabia ambae nae alikuwa anafadhili hizi operesheni financially!!

Saudi Arabia, Pakistan (ISI), na USA (CIA), kila mmoja alikuwa na interests zake!
 
Na sio nchi tu! Bali mataifa kumi yenye nguvu kiuchumi, kijeshi, teknolojia na intelejensia. Tatizo watu wanaamini sana propaganda toka CNN, BBC, CNBC, ITV na wengine wenye maana ya kufanya hivyo.
 
Kwa maoni yangu kuwashinda hao jamaa ni vigumu kwa sababu kadhaa;

1.Hao ni Jihadists yaani kwao vita ni imani,vita ya namna ni ngumu sana kuishinda kwa sababu hao jamaa kupigana vita ni kama ibada hivi,maana yake yeye haogopi kufa akiwa vitani sababu anapigania imani yake na akifa ndio ibada yenyewe,tofauti wa wanajeshi wa Nje ambao kwao pamoja na kupigana lakini hujitahidi sana kukwepa kupoteza wanajeshi wao kwa kuuawa au kujeruhiwa.

2.Kupigana vita ni jukumu la kifamilia,hii ina maana baba na familia yake mzima lengo lao ni moja,hivyo ikitokea baba kauawa au amekamatwa basi mtoto wa kiume wa miaka kuanzia 14 anaweza kuendeleza mapambano hivyo nguvukazi ya wapambanaji inaongezeka,pia familia inashiriki kuficha silaha,taarifa nk,ikiwemo wake zao,hivyo watoto wote ni wapiganaji watarajiwa.

3.Ni vita isiyo na mwisho kwa sababu mwisho wa vita ni kukamilika kwa malengo yao ya kuiteka nchi nzima na kuweka utawala wao wa sheria za Kiislam,hivyo kama lengo lao halijatimia vita haijaisha bado,hii inawia vigumu majeshi ya marekani na washirika wao ambao huweka muda maalum(time frame) ya majeshi yao kukaa huko tena kwa gharama kubwa.

4.Baadhi ya wanajamii na watu kutoka serikalini kushirikiana nao kisirisiri,hii nayo inachangia sana maana kuna watu wanawaunga mkono kichinichini hivyo kufanya mipango yao kadhaa kufanikiwa,hii pia inahusisha kujichanganya na raia.

4.Uzoefu wa eneo la mapambano,kumbuka hawa jamaa ni wazawa wa Afghanistan hivyo wanalijua eneo lao vizuri,hasa kutumia milima na mapango kujificha na kufanya mashambulizi kitu ambacho jeshi geni sio rahisi kujua 'machimbo' na mbinu zao.(kumbuka Osama alivyowasumbua wamarekani).

Mwisho,kupata fedha huenda wanafadhiliwa na watu tofauti tofauti wenye itikadi zinazofanana kutoka nchi zingine au hata ndani lakini bado bajeti zao haziwezi kuzidi ya Wamarekani na washirika wao ila kikubwa zaidi kwao ni ile ari(Spirit ) ya kupigana kama nilivyoeleza hapo juu maana hata silaha wanazootumia sio advanced ukilinganisha na Majeshi ya kigeni, ukiangali hata usafiri mara nyingi wanatumia pikipiki ,viatu Makobazi,Uniform hawana,bunduki za kawaida tu,ila ari yao usipime.
 
Marekani!
 
Wakati mwingine mabavu hayasaidii hata kama wewe ni super power,ona sasa US na Nato wametolewa jasho na kikundi chenye silaha duni kabisa.
Sidhani kama wakubwa wamewakatia tamaa, shida yao kubwa ilikua ni Osama ambaye tayari waliisha muua so hawana interest na Afganistan any more.

Back to the topic; nadhani watu wenye misimamo mikali ya kidini, upiganaji unaanzia moyoni, umlipe usimlipe yeye anajua anapigana halafu mola wake atamlipa, ogopa sana mtu wa namna hiyo, hakati tamaa cause yeye hata ukimuua, anajua kuna maisha mengine baada ya kifo na anajua kua kwasababu atakua kafia kwenye kupigania huyo mungu wake then mungu wake huyo huyo atamlipa huko aendako so kwake kifo is nothing
 
RIP Jemedari John Joseph Pombe Magufuli
 
Pakistan inahusika,vile vile Mimi huwa najiuliza kikundi kama Taliban wanapataje humvee(USA made)za kivita?
Wale ISIS walikuwa wanapata wapi Landcruiser mkonga Tena mpya?
Vita ni biashara kubwa,hapo makampuni ya USA na UK yanauza siraha za kutosha.hii ni proxy war,wanaopigana mbele,Wana wengine wanaowapa msaada nyuma,Russia,China,Hawa wanapenda USA atoke Afghastan,na wapo tayari kuipa msaada Taliban,Ili ishikishe adabu serikali iliyowekwa na USA na washiriki wake,Taliban wameishakutana na China,ni Swala la muda,China atakuwa ndio mbabe mashariki ya Kati,
 
wazungu wanatufanya sisi wakaazi wengine wa dunia wajinga sana..ukifatilia tangia marekani (na haswa CIA) waingine rasmi Afghanistan basi zaidi ya asilimia tisini (90%) ya dawa za kulevya Opium (pia yenyewe ni malighafi kuu ya dawa za kulevya heroin ) inatoka Afghanistan. Hizi dawa zinasambazwa kote masharaki ya mbali (haswa wakiielenga China, Urusi na Korea Kaskazini ili kuzidhoofisha jamii hizi manake kijeshi ni vigumu kupambana nazo ), lakini pia zikisambaa sehemu mbali mbali duniani na ikiwaletea marekani (CIA) faida ya mamilioni ya dola ambazo zinatumia kufadhili efedhuli wao mahala kwa mahala hapa ulimwenguni...Talibani nao ni washirika wakubwa sana wa hii biashara na ndo wanakopatia faida kubwa (pamoja na vyanzo vingine kama kutoza kodi nk)..
 
Ahaa kumbe shida ilikua Osama.nina wasiwasi baada ya US kuondoka wataleban watatengeneza wakina Osama wengine,sasa sijui itakuwaje uko mbeleni.
 
Lakini inasemekana marekani ndiyo soko kubwa zaidi la madawa ya kulevya duniani
 
Taleban wazee wa Pashtun, khost, Peshawal-Pakistan, wazee wa handas Kabul na Kandahar..

hahahahaha, nchi ngumu sana ile pamoja na ule ukanda wote kuanzia kashmir kuja mpaka Islamabad to Karachi - Pakistan..
Handas Kabul [emoji1]
 

In return nao wanapewa Opium maana ndio zao kubwa wanalopigania huko
Middle East ni mafuta na Afghan ni drugs hakuna kingine zaidi ya maslahi hayo
Na Taliban ndio wanaofhulumu na kulinda mashamba hayo na kuwapa wazungu

Eti wanasafisha Taliban really?
Miaka yote hiyo wanajeshi wao wangapi wamekufa
Ukiangalia kwa upana hapo ni maslahi tu ya poppy
Nchi ambazo hakuna maslahi hawaendi
 
Talibani wapo Afghanistan tangu 1976.... Urusi alishakula kipigo cha mbwa koko akapoteza 15,000 soldiers.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…