Nani yupo nyuma ya Taliban? Miaka karibu 20 ya vikosi vya Marekani na washirika wake Afghanistan ni Bure?

Nani yupo nyuma ya Taliban? Miaka karibu 20 ya vikosi vya Marekani na washirika wake Afghanistan ni Bure?

Waarabu wana hela sana - ndiyo wanaowafadhili hao jamaa.
Nchi hiyo ..Taifa hilo lina wanaume wengi kuliko wanawake... Tazama vizuri!!
Wana reserve ya Mafuta kwa hadi miaka 300 ijayo.
Wamarekani na nchi za Ulaya zipo hapo wafiwa na silaha za kisasa na nguvu zote za kijeshi na intellijensia sasa miaka 20..... nia yao nini???
Waarabu Lazima wajikinge..Na waJilinde ili moto usiwafikie!! tafakari
 
Taleban wazee wa Pashtun, khost, Peshawal-Pakistan, wazee wa handas Kabul na Kandahar.

hahahahaha, nchi ngumu sana ile pamoja na ule ukanda wote kuanzia kashmir kuja mpaka Islamabad to Karachi - Pakistan.
Bila kusahau Helmand Province,kule Muingereza alipelekwa udenda ulimtoka 😀 😀
 
[emoji3] [emoji3] [emoji3] Mugabe alinukuliwa akisema "Siku mbu akitua kwenye korodani zako, ndipo utakapojua kwamba kuna wakati unaweza kutatua matatizo bila kutumia mabavu"
Alikuwa Mao Tse tung
 
Taleban wazee wa Pashtun, khost, Peshawal-Pakistan, wazee wa handas Kabul na Kandahar.

hahahahaha, nchi ngumu sana ile pamoja na ule ukanda wote kuanzia kashmir kuja mpaka Islamabad to Karachi - Pakistan.
Kitu kimoja ninacho kikumbuka personaly kuhusu hapo Peshawar Pakistani ni ukarimu wa watu wake hasa kwa wageni.
 
Vita nzima ya Afghanistan imekaa kisiasa na kibiashara zaidi kuliko lengo kuu la kuwamaliza Taliban,Marekani walipoingia mwaka 2001 walifamikiwa sana kuwaondoa Taliban maeneo muhimu kama kabul,kandahar,Helmand na kuwasogeza mbali kusini mwa nchi.
Ghafla ndi kampeni za kumuondoa Sadam Hussein zikaanza,wanajeshi wengi wa marekani na vifaa walipelekwa Iraq kwa ajili ya vita kubwa kumuondoa Saadam Hussein,.Huku nyuma ikawa mission ya Nato.
Lengo kuu la vita ya Afghan kwa maoni yangu
1.Marekani alilenga kupata advance base kwa ajili ya logistic kuelekea Iraq,vifaa vingi na wanajeshi walitokea Afghanistan kwenda Iraq,yaani ilitumika kama njia kueleaa Iraq,ndio maana baada ya kumalizika kwa vita ya Iraq marekania alipoteza kabisa interest na vita ya Afghan
2.Pili lengo kuu ilikuwa ni ushawishi tu hapo middle east,yaani kupata uwanja kueneza policies zake na influence hapo middle east
3.Tatu ilikuwa ni kufanya biashara na makampuni ya ulinzi binafsi na silaha marekani,kipindi cha vita makampuni binafsi ya ulinzi kama Black water, Tripple canopy walipata tenda nyingi sana kutoka wizara ya ulinzi marekani.Ndio maana hata vita imechukua muda mrefu ili haya makampuni yaendelee kunyonya pesa za walipakodi wa marekani kwa maslahi yao.
4.Nne ni issue ya Opium au Popy,hii sina uhakika nayo sana ila ni moja ya sababu ambayo watu wengi wanaongelea kwamba marekani na nchi nyingine walitumia mwanya wa vita kuendeleza zao la Opium na kufanya biashara.
Ni maoni tu mawazo yangu sio sheria,yanaweza kupingwa pia.
 
Inaitwa Afghanistan the graveyard of Empires

USSR walikuwepo miaka ya 80 wakashindwa na Mujahdeen (wakisaidiwa na USA)

Taliban wakaingia mwishoni mwa miaka ya 90 ikawa rasmi sasa ni Unstable, Rogue state, safe heaven for radical, extremist terror group kama Alqaeda wakajitanua mpk maeneo ya Pakistan - Pashtun.

September 11 2003 wakafanya yao. Bush kaanzisha military campaign dhidi yao, imeridhishwa kwa Obama, Trump, Biden leo miaka karibu 20. More than 2 trillion $$ zimetumika.

Leo troops za US & UK wanafungasha virago Taliban wamerudi. Wanateka miji kama wanatembea nani ana sponsor hawa jamaa?
Russia na Iran
 
[emoji3] [emoji3] [emoji3] Mugabe alinukuliwa akisema "Siku mbu akitua kwenye korodani zako, ndipo utakapojua kwamba kuna wakati unaweza kutatua matatizo bila kutumia mabavu"
Hahahahaaa! Mugabe alikuwa ni kiboko ya Mabeberu! [emoji16][emoji16]
 
Watu wengi hamjui kuwa hizo crisis zote zimesababishwa na Westerners (US na washirika wake) hata hayo makundi ya kigaidi wanayojidai kupambana nayo wao ndio wanaowapa support ili kuleta mfarakano kwenye nchi hizo za Mashariki ya Kati ili wao wapate mianya ya kuchuma mali asili zilizopo na kikubwa ikiwa ni crude oil.

Dunia hii inaendeshwa tofauti sana na watu wengi tunavyojua au tunavyodhani.

Mataifa ya magharibi wakishaona nchi ipo kwenye third world na ina rasilimali wanazotaka kama madini, mafuta n.k watakuja kwa njia za kilaghai kujidai wanataka kuwasaidia kwa mikataba ya kinyonyaji.

Mkiwa na viongozi wanaojielewa wakiwakazia wao lazima watafute namna ya kuleta machafuko kwa ku fadhili makundi ya waasi/magaidi halafu machafuko yakitokea wanajidai kuleta troops wakijidai kuja kuleta/kulinda amani kumbe ndio muda wao wakuwapiga.

Angalia nchi kama Libya ilivyokuwa stable kipindi cha Gadaffi. Lakini mzungu akaona kuwa hawezi kuinyonya Libya mpaka watafute njia ya kumuengua Gadaffi. Wote tunajua kilichotokea na tunajua Libya ipo katika hali gani sasa.

Hapo mainstream media zinawajaza habari za tofauti (misinformation). Hizo ni propaganda za Westerners

Tumefichwa mengi.
Dah akili kubwa sana hii MKUU

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
 
Sio rahisi kupigana na ideology.
End off........Umemaliza mjadala
The rest is conspiracy theory..........
Soviet walikimbia Mujaheedin wa Afghanistan japo walikuwa na special forces wao "Spetnaz" waliobobea katika fani ya brutal survival skill duniani .
US pia walikimbia Ideology ya VietCong waliokuwa wanamuabudu Ho Chi Minh.......
History always repeat it self, Taliban ni morden day "Mujaheedin",
Russia is behind this though........
 
Nashangazwa sana hapo Afghanista sioni hata mwanamke barabarani.. Jee ,vipi hawa jamaa?
 
Inaitwa Afghanistan the graveyard of Empires

USSR walikuwepo miaka ya 80 wakashindwa na Mujahdeen (wakisaidiwa na USA)

Taliban wakaingia mwishoni mwa miaka ya 90 ikawa rasmi sasa ni Unstable, Rogue state, safe heaven for radical, extremist terror group kama Alqaeda wakajitanua mpk maeneo ya Pakistan - Pashtun.

September 11 2003 wakafanya yao. Bush kaanzisha military campaign dhidi yao, imeridhishwa kwa Obama, Trump, Biden leo miaka karibu 20. More than 2 trillion $$ zimetumika.

Leo troops za US & UK wanafungasha virago Taliban wamerudi. Wanateka miji kama wanatembea nani ana sponsor hawa jamaa????

mstari unao tenganisha makundi ya kigaidi na marecani ni mdogo sana,
 
Kuna watu wapo nyuma yao mimi niliwahi kuongea na raia mmoja ambaye ni muafghan anasema wengi wa wapiganaji wa Taleban siyo raia wa Afghanistan ni kutoka nje kama Pakistan na baadhi wanatoka nchi nyengine kama za ulaya wanakuwa wanalipwa kama kazi ya kawaida. Mshahara na wanaambiwa wakiteka mji kila kitu yaani mali ni halali zao wanawabaka wanawake.

Hivi vita vingi nyuma kuna maslahi ya watu waliotaka waipeleke demokrasia wameikimbia nchi baada ya kujaribu miaka 20 kwa aibu kubwa wamewaachia nchi yao.Wameenda iraq fujo tupu haikaliki na Libia nayo haikaliki.

Marekani anaipiga iraq amuondoe Sadam Hussein iran alikuwa upande anafurahi Saudia yupo pembeni. Saudia anampiga myemen mmarekanj yupo na Saudia Iran anakasirika anawaunga mkono wahuthi na hivyo hivyo Siria wamarekani wanawafadhili waasi Mrusi anamlinda Bashar Assad asiondoke na mpaka leo yupo. Nenda libia Ghedafi kaondolewa waasi wakishirikiana na Marekani na Nato machafuko yameibuka sasa kuna serikali sijui ni mbili ama ngapi moja inaungwa mkono na warusi na nyengine uturuki kiujumla mambo ya siasa ni uchawa tu.

Wee miaka ishirini yote waliyoyafanya huko Afganistan yanapotea yoote ndani ya mwezi sifikirii itafika mwaka hawa jamaa nchi yote wataichukua. Ikiwa wanaimiliki asilimia 65% ya nchi. Marekani na washirika wake waache kwenda nchi ambazo zina utamaduni wao toka karne na karne kueneza itikadi zao mwisho matokeo yake ni haya amani hakuna. Wangekuwa wanafanikiwa basi wanaacha amani kama wanavyodai wenyewe lengo ni demokrasia. Sasa demokrasia bila amani wapi na wapi mpaka sasa nchi tatu karibu dunia yote imejifunza wameshindwa kupeleka hiyo democrazia na amani wameacha vurugu tu.

Huu ni wakati sasa kila nchi ijiamulie mambo yake yenyewe na isipangiwe na Wengine ili mradi isihatarishe usalama wa nchi nyengine.Upande mwengine Korea ya kaskazini na rais wao Kim wanaweza kuonekana ni wehu kwa kutengeneza kwa silaha za nyuklia, Silaha za nyuklia wakati mwengine siyo unazitengeneza ili umpige adui hapana inakuwa kama ni chombo ambacho unaweza kukaa mezani na mataifa haya makubwa na ukaongea nayo yakakusikiliza. Kama korea kaskazini asingekuwa na hii kitu wangeshammaliza kitambo.Silaha za nyuklia hazina udogo wa nchi madhara yake ni makubwa tu.
Katika jeshi lenye discipline ni Wataleban, wale hawabaki wanawake maana wana discipline kubwa ya uislamu
 
Pia sijui kama wengi mnafahamu kuwa Wataleban ambao majority wanatoka kwenye kabila la PASHTUN wanasema kuwa wao ni miongoni mwa Makabila 10 ya wana wa israel yaliyopotea. Wao walipokuwa introduced kwa Uislamu waliupokea mara moja maana unaendana na mila zao za asili

Cheki hii documentary:
 
Ile vita ni ngumu kwa sababu Taliban sio jeshi rasmi (kwamba lina uniform rasmi na makazi yanayojulikana), ila ni kikundi cha watu ambacho wamechanganyikana na raia wa kawaida kabisa. Hawa hupanga mashambulizi including kwenye miji mikubwa kabisa ya Afghanistan. Kikundi kilitengenezwa na USA makusudi kuwakomoa Warusi, sasa kimekuwa kikubwa beyondo control. Kimefika mpaka Georgia, Armenia nk.

Zaidi ya yote, rasilimali (asset) yao kuu ni utayari wa kufa. Kwao kifo ni “raha” tu na malengo yao ni ya kidini zaidi. Vita ya kiimani (jihad) ni fursa adhimu ya kuelekea peponi.

Unawezaje kuwashinda vichaa aina hiyo. Labda uwapige bomu la nyuklia kama ilivyokuwa Hiroshima na Nagasaki Wajapani walipoanzisha mashambulizi ya Kamikaze. Tatizo hizi ni enzi nyingine na Taliban si nchi wala taifa.
 
Taleban wazee wa Pashtun, khost, Peshawal-Pakistan, wazee wa handas Kabul na Kandahar.

hahahahaha, nchi ngumu sana ile pamoja na ule ukanda wote kuanzia kashmir kuja mpaka Islamabad to Karachi - Pakistan.
Bila kusahau Mapango ya Torabora..

Sent from my SM-A405FN using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom