Nani yupo sahihi,Afande Sele au Mrisho Mpoto?

Afande sele amekuwa mtu wa kutafuta kiki sana siku hizi.
 
Mpoto kwa kulinganisha kushangiliwa kwa wakongo walawiti wa watoto na kumuingiza mkongo kwenye wimbo kachemka. Sele kwenye hili yuko sawa.
 
Jameni ee ule wimbo ni uzalendo kwa ccm na sio nchi, yaani lundo lote wasanii music ndio kamuona huyo mkongo, labda na yeye ni walewale si wa kigoma yule huenda ni mrundi kwa kwake siyo shida.
 
Maneno yenye busara.
 
Mrisho sio mtu ninaemkubali sana, Afande Sele ni kati ya wasanii naowakubali.

Lakini Mrisho anazo hoja za maana zaidi na mifano yenye nguvu sana sijui kama Afande ataweza jibu
 
Kuimba tu si uzalendo nadhani uzalendo una maana pana sana
 
Afande sele yupo sahihi ila mrisho mpoto ana hoja madhubuti...

Jibu lolote linaweza kuwa sahihi ama si sahihi kutegemeana na sababu za jibu lako.
 
Mrisho alichofanya ni kucheza na fikra kwa kutumia muda mrefu kuandaa jibu. Afande ametoa hoja sahihi kabisa na ina mashiko huwezi kuimbia taifa uzalendo kwa kuacha wasanii wazawa na kumchukua mtu wa taifa jingine ambae si mzawa wa nchi hiyo wakati nchi ina wasanii wazawa. Mrisho amechukua muda mwingi na mifano kutetea hoja na anaonekana kama ameshinda kwa kuwa ameweka na mifano na uenda ameshirikisha hata watu wengine kuandaa jibu kwa Afande.

My take Mrisho kuwa mzalendo kwa kuboost watanzania wenzako huyo mcongo atabaki kuwa mcongo na ata kizazi chake bado kitaitwa wacongo tupeane fursa na kataa kuwa kaa
 
nilicho gundua ni bora kusoma stori za Beira Baby Boy kuliko kusikiliza mawazo ya humu.

yaani mmoja akisema mpoto yuko sahihi basi wafuatao kuchangia wako mkondo huo huo, akianza kwa kusema afande yuko sahihi basi wote afande afande.

sasa mlipewa vichwa vya nini? mpoto analeta mifano ya che guevara kuipigania cuba eti ndo uzalendo pumbavu kabisa. che kazipigania nchi nyingi hadi kongo. sio kwamba alikuwa mzalendo wa nchi izo bali hakupenda utawala wa kibepari yeye ni mzalendo kwa itikadi ya ujamaa (alikuwa tayari kuifia katika nchi yoyote)

mpoto kakosea, aliupima vp? uzalendo wa bella dhidi ya afande ama hao alio watoa. kama tu siamini yule mzalendo # 1 tunamuona ni muharibifu leo tunaanzaje sema eti bella ni mzalendo kuliko walio ondolewa
 
y
yaani akili zako na mpoto ni sawa, unataka jeshi la marekani liwe na wahindi wekundu (wenyeji wa kule ambao ni asilimia 2% huku 98 ni wahamiaji.

unaongelea ufaransa wanao amini kwenye assimilation pilicy na kuwaona watu toka makoloni yako kuwa sawa na wafaransa asili

mbona mnakuja na mifano ya kijinga jinga ko wataka twambia tz wakongo ni wengi kuliko watanzani, wataka tukuamini wakongo ni sawa na watanzania asili

acheni mambo hayo mrisho kachemka kafata umaarufu wa bella ila sio uzalendo. kwanza mwenyewe tu uzalendo wake unatia shaka vp kuhusu bella.
 
tatizo unapowatoa wazawa kwenye shughuli za Taifa lao na kuwaweka wageni Unatumia kigezo gani..........? lengo ni nini.......? Wazawa walioenguliwa wanajisikiaje......?
 
Kama nilivotangulia kusema awali hii dhana ya uzawa ni dhana ya watu wabinafsi kupindukia na most of them ni kutoka mataifa duni kupindukia justin bieber sio mmarekan anold schwazniger sio mmarekan celine dion pia ni mkanada unless kama case study yako ni north korea au somalia mpoto yuko sawa kabisa unless kama hilo shavu angempa fally ipupa ila mzee wa masauti tuko nae mitaani uku na punde anaukana uraia wake wa kongo nyie bado mnamuona sio mzalendo
 
Kwanza hakuna Ras kati yao, hzo rasta ni symbol tu ya USANII wao. Pili hakuna aliye sahihi kwa jinsi nilivyosoma. Kama alivyoeleza mpoto hoja za afande zinakosa mashiko kwa vigezo alivyotumia UZALENDO, UZAWA nk. Lkn Km kuna wanamziki watz Mpoto aliwatoa alipaswa aeleze sababu za kiufundi za kuwatoa kwan nao walikuwa na haki ya kushiriki labda km bela alihitajika sana vocally. Otheryz Mpoto alifanya uhuni kwa sababu za kiswahiba. Haya mengine ya kusema Prof. shivji ni asian me napingana nayo ni low sana, ni sawa na kusema Akon ni mgana. Mtu akishakuwa raia wa kidumu wa nchi fulani kuwa mzalendo ni wajibu wake, so mifano kuwa wakina prof shivji wanapigania nchi, ni uzushi tu. Yeye km msomi na mwanazuoni anafanya wajibu wake na ndivo wasomi wengi wanapaswa kufanya hvo, kuonyesha njia, kukosoa nk
 

Amemjibu vizuri sana na kiungwana
 
Mrisho mpoto ni mnafiki mchumia tumbo,

Kwahiyo anataka kuuaminisha umma yule nyoso ni mzalendo kuliko waliachwa,

Kwanza uzalendo haumasishwa uzalendo unatoka moyoni
Hii imenikumbusha alivowakilisha kenya uko nchi za watu kwenye tamasha la kiswahili japo alijitetea sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…