Nani yupo sahihi,Afande Sele au Mrisho Mpoto?

braza mbona mgumu kuelewa, wamerekani asili ni watu kama millioni 5 tu huku 98% ni wahamiaji kule hivyo kusema kila sekta itashikwa na wazawa ni uongo.

sasa kuendelea kunipa mfano toka marekani unapoteza muda maana kule karibu wote ni wahamiaji

je huku kwetu hali ikoje, kwa nini umuondoe mtanzania na kumpa mgeni(umeupimaje uzalendo wake)
 

Huyo prof shivji namueshimu sn kwa cv yake iliyotukuka ila alichotufanyia kwenye katiba mpya Mungu amsamehe huenda maslahi yalimpenda zaidi akaweka usomi wake mfukoni
 
MANYWELE PEKUPEKU YUPO SAHIHI KWA FIKRA ZAKE. NI MSALITI MNAKUMBUKA ALIVYOJITANGAZA NI MKENYA KWENYE ONESHO FULANI HUKO MAJUU!?
Hapa alichemka sana na sikuwahi kuamini matango pori aliyotulisha kuwa alikuwa hajui jinachoendelea aseme njaa aka pesa ndo ilimfanya awe hivo
 

Haya masanii yote ni ya ccm bei zao zinajulikana corridor za lumumba
 
Ni ngumu sana kutofautisha uzalendo na asili ya mtu
 
Christian bella ametoa mchango mkubwa kwenye tasnia ya muziki nchini kuliko huyo bwana sele
 
wote wawaili ni kenge kwasababu naamini UZALENDO hauhamasishwi, ni hisia.
 
Reading from here, Mpoto ameijibu vzr! Watanzania wenyewe baadhi c wa nchi hii kiuhalisia.

My dad ni wa mashariki ya kati, but I am a Tanzanian die hard! Am I not mzalendo kwa defn ya Sele?
 
wote ni marasta wala nyama, ndo maana wanabishana, kisa utofauti wa siasa na vyama, hawatoacha kulumbana
 
Mkuu kwnye hili naomba nipingane na wewe unless kama umeanza kusikiliza mziki miaka ya 2012
Nimeanza kumsikia sele wakati wacha kupiga mayowe inatoka.kwenye chorus inasikika sauti ya jay moo.hakuna kipya alichokileta kwenye game.maudhui ya nyimbo zake nyingi ni kukosoa wasanii wenzie.hata wewe nkikuuliza unitajie nyimbo kali ya bwana msindi aliyowahi imba peke yake bila kumshirikisha msanii mwengine sijui utanitajia wimbo upi.


The nigga was/is overated na ufalme wa rhymes feki wa gazeti la udaku.hivi kweli jamaaa anaweza kuwekwa kwenye kundi la washairi kweli?.kwa punchlines zipi,flow ipi,metaphors zipi,wordplay ipi,vina vipi?.
 
Mrisho ni bonge la mnafiki ondoa maneno yasio na tija TENA kwenye uzani hayafiki haya robo gram unajitetea kwa unafiki uliotenda hatuwezi kukuelewa labda ukamueleze mwanao nae ata itika na sio kukubali
 
Huwezi waacha wasanii wazawa ukawachukua wageni huo ni unafiki.

Sele yupo sahihi 100%.
 
Nachokiona mkuu humkubali Sele, lakini naamini kama kweli tunaangalia watu ambao wameweka msingi wa huu mziki wa bongo jamaa naye hatuwezi kudharau mchango wake. Ni kweli jamaa hakuwa na sauti nzuri ya kuimba chorus kiasi ilibidi ashirikishe watu wa kumuimbia chorus. Jamaa ana heat song nyingi; ukiachana na hiyo mayowe kuna mkuki moyoni, mtu na pesa, darubini kali, dini tumeletewa, mtazamo, uwanja mpya, karata dume, ndugu zangu,usinichukie et al, zote hizo zilileta changamoto.

Bella ni mwanamziki mzuri lakini kusema Bella ana mchango mkubwa kwa muziki wa bongo kumzidi Msindi sidhani kama ni sawa. (Mleta uzi atatusamehe kwa kuingiza uzi wetu ndani ya uzi wake)
 


Binafsi naiona chuki tu hapa
 
Mabishano yote yapo juu ya jambo la kijinga hivyo wote wajinga tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…